HAITOTOKEA: Msimu Pekee Ambao Yanga SC Ilikubali Kupoteza Ubingwa Ili Simba SC Asishuke Daraja

HAITOTOKEA: Msimu Pekee Ambao Yanga SC Ilikubali Kupoteza Ubingwa Ili Simba SC Asishuke Daraja

Hakuna kitu kama hicho, hakunaga upendo wa dzaini hiyo kwenye hizi d3rby

Hapa tu, tulipo bado tunaombeana kufungwa na timu za nje katika mashindano ya kimataifa

Tunaombeana dua timu zitolewe mapema na timu za nje ili mradi tu kumuona mtani wako ana safa

Niambie huo upendo wa Yanga kumuachia Simba amfunge ili asishuke daraja unakujaje?

Wakati hata hapa kuna watu wanataka timu ishushwe daraja ili wao watambe

Katika huo mwaka ambao mtoa mada kautaja siku ya hiyo mechi ilikuwa inamtegemea Yanga kutangazwa ubingwa endapo atashinda au kutoa sare

Dakika ya 21 simba alipachika bao lakuongoza kwa mchezaji Edward Chumila

Kumbuka hapo simba alihitaji matokeo ya ushindi ili kuweza kusalia ligi kuu

Yanga wakaja kusawazisha dakika ya 36 na kufanya mpira uende mapumziko kwa droo ya moja moja

Dakika ya 58 kuna player wa simba alijulikana kama zigzag huyu alitupia kamba bao la pili la kuongoza na hili ndio lilidumu mpaka mwisho wa mchezo

Sio kweli kuwa Yanga aliisaidia simba isishuke daraja kwasababu kichapo walichopigwa Yanga kiliwafanya wakose ubingwa ambao nao walikuwa wanautegemea

Kongole ya mtu aliyeinusuru Simba isiweze kushuka daraja ni huyo zigzag kwa kufunga bao la pili, the rest ni kujipa ujiko ambao wote tunajua haiwezekani hata kwa namna yeyote Yanga kumsaidia Simba
Hizi timu haziwezi kushuka daraja kwani nje ya burudani ya soka, zinasaidia sana kuweka amani na utulivu,
Na pia kuimarisha umoja wetu, unaweza kukuta watu hawajuani hata majina lkn
Wanafurahi na kutaniana kisa Simba na Yanga,
 
Achana na stori za Kahawa ile mechi mtani alipigwa kihalali hakuna cha nini wala nini..
 
Baada ya mechi mashabiki wa Yanga walikasirika sana mpaka kipa Sahau Kambi akang'olewa jino..nilikuwa chalii lakini kumbukumbu hiyo ninayo manake pale nje ya uwanja yalikuwa yanarushwa mawe. Kipindi hicho kulikuwa na jamaa aliyetrend sana wa kuitwa Maumba.
Maumba ana uhusiano gn na mechi hyo?

Huyo maumba alikuwa mlawiti watoto wa kiume.
 
Vijana wengi mtakuwa hamna kumbukumbu ya huu msimu.

Yanga ilikubali kufungwa na Simba mechi ya mwisho ili simba isishuke daraja na kwa kufungwa huko Yanga ikakosa ubingwa.

N.B kwa new school aka "soccer Google" nawakumbusha "zamani" game moja ilikuwa na pointi 2 ukishinda!

Upendo huu haujawahi kutokea na haitokuja kutokea tena.

Mtu na Mai Wake [emoji172][emoji169]

View attachment 2230677
Utopolo Msijifiche kwenye kichaka cha huruma.

Hii gemu mlifungwa kihalali na Simba na wala hamkuwa na suala lolote la kuisaidia Simba isishuke daraja.

Nakumbuka Yanga walikuja na Ngoma pamoja na kinyago aliyejipaka masizi uso mzima,
Pia walishaandaa t-shirts za yanga bingwa -1988..

Yote hayo yalikuwa ni maandalizi ya kusheherekea ubingwa ..

Matokeo yake kinyago alisubiri Giza liingie ndy aweze kuondoka.,na Ngoma zilifuatwa siku ya pili.
Hyo ni baada ya lile genge zima la kikundi cha mdundiko wa maleft kusambaratika,na kutelekeza vifaa vyao na kukimbia kusikojulikana.

Hizo t-shirts zao za ubingwa walizivaa nyumbani kama night dress..

Nakumbuka kama sio John makelele( zig zag)
Au Edo boy ndy aliyepeleka kilio kwa utopolo.

Yanga alifungwa sababu ya kujiamini kwake..

Simba waliondoka kishujaa huku mashabiki wao wakisukuma bus la wachezaji hadi Msimbazi ,
Makao makuu ya Simba sports club.

Sasa hebu fafanua vizuri,
Ilikuwaje timu iliyopanga kuiokoa Simba ijiandae na mambo yote hayo?
 
Back
Top Bottom