Haiwezekani Air Tanzania iwe na ndege inayotoza Tsh. 100,000/- kwa safari za ndani?

Laki 1 ni only Dar to Znz…

Arusha to Dar laki 1 famchezo nini [emoji23]

Wacha tusafiri na bus usiku… kesho naijaribu safari ya usiku.

Utuletee experience yako hapa. Uelekeo wap tafadhari
 
Hongera mleta mada, umetoa hoja nzito na nikwambie tu hilo linawezekana kama tusingekua na viongozi wabinafsi na katili kwa Wananchi wao, wapo kimaslahi sababu ni wafanyabiashara pia (wanamiliki mabasi)

Wangeruhusu ushindani katika sekta ya Anga ungeshangaa hizo bei zake.
 
AIRLINK imekuja juzi tu imechukua route ya kwenda kwa madiba
Hata sijui walikuwa wapi wakati watanzania wanajaza ndege kila siku kwenda south.
Mbona fast jet iliweza na ilikuwa campuni tu ya kishkaji?
Ukweli nawaelewa sana private sector.....hawana longo longo....
 
usingesoma ungemuelewa mtoa mada kwa kuwa umelishwa ujinga huwez kumuelewa..

Una uhakika gani kwamba sijaelewa au kwa vile nimeandika mtazamo tofauti na wewe?

Usiwe mwepesi kutoa matusi ya rejareja kwa watu kwa sababu unaamini unajua sana kuliko watu/mtu mwingine

Broo nauli laki 2 wamepanda watu sita alafu nauli laki wamepanda watu sitini.. Kwa akili yako ya shulen nan anapata pesa ndefu...

Naona wewe kama ilivyo kwa mleta mada, fikra yenu imebanwa kwenye dimension moja tu ambayo ni ya kihisabati zaidi wakati bei za tiketi za ndege hazipangwi kwa mtazamo kama huo...

"Airlines aren't in the business of filling seats - they're in the business of making money and getting as much as possible for the entire flights", hii ni nukuu ya Scott Keyes ambaye ni CEO wa Going mtandao unaosaidia wateja kupata tiketi za ndege za bei nafuu...

Maamuzi ya bei ya tiketi ya ndege kwa mashirika yote hutegemea vitu vingi, na katika hivyo vitu vingi hakuna sababu kama hii unayotaja ya kwamba, "nauli ikiwa ndogo basi shirika litapata wasafiri wengi zaidi"

Siwezi andika mambo yote shughuli zangu binafsi zaningoja hapa, kama unataka kuelewa zaidi hayo niliyoaandika unaweza ukagoogle, "how does airline pricing work".
 
Kila usafiri una mahitaji yake na aina ya watu. Laki moja ni kwenda na kurudi kwa mtu wa kawaida. Tz ina watu wa kawaida.
 
Sawasawa 👍 👍
 

Fastjet wao business model yao ni low-budget airline na sio model inayotumiwa na national carriers kama ATCL...

Kwa sababu ya kutaka kuendesha biashara ya ndege kama vile kuendesha biashara ya mabasi au bajaj, Fastjet Tanzania na Mozambique waliishia kufa kibudu kwa sababu ya wingi wa madeni kwa suppliers wao, high OPEX kiasi cha kushindwa kuzifanyia maintenance ndege zao...

Na ndio maana biashara iliwashinda Tanzania na Mozambique, kwa sasa wamebakia kuoperate Zimbabwe pekee...
 
Nauli ya basi Dar -Mwanza = 60,000 TSH ndege ndio watoze 100,000/= acha kujidhalilisha dada
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…