Haiwezekani mtu mmoja kumiliki hisa 49% - Mwakyembe

Aache kuleta siasa kwenye pesa, Tanzania hatuwezi kuendeleza mpira kwa mambobya serikali kuingilia mpira.
 
Inaonesha hawafurahii jinsi Mo anavyowakwepa kwenye upuuzi wao.

Sportpesa watasepa sijui simba itajiendesha vipi
 
Hii ni njama kuihujumu simba. Waziri kaongea leo ili kesho KILOMONI apate nguvu ya kusemea. Hatutakubali
 
Mbon man city anamiliki MTU moja
SHERIA KATI YA NCHI MOJA NA NYINGINE HUTOFAUTINA KULINGANA NA TAMADUNI AU MAZINGIRA. MFANO JAMAICA BANGI NI HALALI ILA HAPA TZ BANGI NI KOSA LA JINAI.
Kwa kumbukumbu zangu zamani kidogo yaan miaka kama 18 nyuma kulikuwa na mshauri wa michezo aliitwa PAPE. Yy alikuwa Mjerumani kipindi hiko TFF ikijulikana kama FAT chini ya NDOLANGA. Hizo sheria ziliwekwa miaka hiyo ili kudhibiti ulanguzi wa kimichezo. Sheria hiyo ilikuwa mahsusi kwa timu za ligi kuu tu. Na pale mtu akitaka kumiliki lazima wawepo angalau watu wa 3. Kwa hiyo basi zinaruhusiwa kumilikiwa na mashirika au makampuni mbalimbali lkn sio mtu mmoja.
Hii ilikuja mara baada ya ALEX KAJIMULO kuimiliki KAJIMULO FC. Hivyo kupelekea maamuzi yasiyo ya kimichezo zaidi juu ya timu yake. Hata azam haimilikiwi na BAKHRESA kama yeye bali kampuni yake ya AZAM hali hiyo pia ni kwa ALLIANCE nayo inamilikiwa na kampuni sio mtu mmoja.
Kuweka mambo sawa ni kwamba MO anachofanya ni kwamba anaichukua timu kama yake binafsi na sio kama MO INTERPRISSES. Hii hairuhusiwi kwa kufikia hizo % anachotakiwa ni kugawana hizo share equally au semi equally na wanahisa binafsi wengine ambao hawako familia moja na yeye.
Yaan yy achukue 17% ANOTINO Achukue 17% MANENGELO 15%.
Nilichoona hapa ni kwamba sheria hii haikutumika ama kwa kutokujua au kwa makusudi ili kufanikisha jambo fulani kisiasa.
All in all MO ameikuta simba as super brand ambayo kupitia hiyo anaweza kutanua wigo wa biashara zake kupitia matangazo ya kwenye jezi kama ilivyokuwa kwa KILIMANJARO PREMIER LAGER. utofauti ni kwamba TBL wao walikuwa wanatoa vifaa vya michezo na pesa kama mdhamini ila Mo yy anafanya kama mmiliki yaan anaandikia as ameadd up CAPITAL. Fluctuation Capital ambapo kila mwaka huziingiza as gharama zake na hutolea wakati anatafuta faida kitu ambacho si sahihi.
Nimechambua kama mwanamichezo na sio kama SHABIKI.
UKITAKA ELEWA USIPOTAKA ENDELEZA USHABIKI MAANDAZI
 
Hilo ndo tatizo la kichanganya siasa na michezo , mimi nampongeza sana raisi wa Kongo kwa kuchagua waziri wa kichezo ambaye alikiwa mchezaji ,hapo mwanzo , huki kwetu mama ntilie anaeza akawa mganga mfawidhi katika hospitali ya rufaa
 
Jamaa nae amejivuta mno weee kuweka mzigo kila siku wanamwambia weka mzigo mara oooh sijui mambo gani hayajakaa sawa mara anavutana na wajumbe wa bodi ona sasa kakutilizwa na mzigo hajaweka kwa hiyo hana la kufanya zaidi ya ku-comply na matakwa ya maelekezo mapya ya serikali. angekuwa ameshaweka mzigo hizo 49 akawa ameziweka mkononi wasingekuja
 
Kama mm ningelikwa ndo MO,ningeachana na mambo ya uwekezaji kwenye mpira instead ningejielekeza kwenye mambo mengne kabisa,haiwezekan kila siku ukiamka au ikifika jion unakuta kuna hichi na hichi,mpra wetu hapa home Tz n changamoto in terms of investment.

Asubuhi njema.
 
Sasa sio kwa jirani kunawaka moto

Kote jangwan na msimbazi moto umewaka
 
Mchakato wa simba kwenye hisa umekaa kisanii,ukiangalia tu ile bodi ya mdhamini imejaa wasanii watupu,halafu hii issue ya kutaka hati ndio umewashtua serikali!
 
Du,kumbe hizi sheria zipo,mie nadhani kuna ujanja labda ilitumika mahala zikafunikwa hizi sheria watu wakajisahau wakamwaga wino,mambo yamefukuta sasa.
 
Kwa kuzingatia nchi ina sheria zake kuhusu Mambo ya uwekezaji.....
Na kwa vile Sheria inasema juu ya Umiliki wa 49/51......

Je...! Kwa issue ya SIMBA, ni Hasara gani Club itapata iwapo itapata mwekezaji mmoja tu ataye own 49%....?

SIMBA itapata faida gani iwapo Wawekezaji 3 au zaidi kama wanavyopendekezwa na Wizara ndo wata own Hizo Hisa 49%....?
 
mh,napo lazima ataonekana amekiuka kasheria fulani!!!
 
BMT nao wamesitisha hatua zote za uwekezaji aysee...hii nchi hii
 
Siasa mbaya sana. Halafu na watanzania hivi vilabu vinawapumbaza akili sana. Wanasahaulishwa mambo ya msingi, kisa yanga au simba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…