Haiwezekani mtu mmoja kumiliki hisa 49% - Mwakyembe

Haiwezekani mtu mmoja kumiliki hisa 49% - Mwakyembe

siasa na michezo wap na wap maskin Tanzania nchi yangu phd holder
 
Mo nae aachane na hiz timu aende akanunue timu yake hiz timu kuendelea n ngumu kuna akilimali na kuna kilomon hiv vizee Huwa vinatumwa s bure
 
Kwahiyo hoja yako ya Mo kutaka kumiliki timu nzima peke siyo sahihi ?
Uelewa wako ni mdogo sana.. ni hivi ikiwa mmegawana hisa mtu mmoja akapata 49% peke yake na nyie mko 1000 mkapata 51% nani anakuwa na hisa nyingi kwenye umiliki?
 
Na sheria ipi ilitumika mpaka akawa na hisa 49% ?,bodi yao iliamua tu wakapeana hisa ?
Ndio na ndio maana hata ile body iko controlled na MO.. kitu ambacho hakitakiwi kwenye kampuni kama ile.
 
Uelewa wako ni mdogo sana.. ni hivi ikiwa mmegawana hisa mtu mmoja akapata 49% peke yake na nyie mko 1000 mkapata 51% nani anakuwa na hisa nyingi kwenye umiliki?
Mimi uelewa wangu ni mkubwa kuliko ukoo wenu wote.
 
SHERIA KATI YA NCHI MOJA NA NYINGINE HUTOFAUTINA KULINGANA NA TAMADUNI AU MAZINGIRA. MFANO JAMAICA BANGI NI HALALI ILA HAPA TZ BANGI NI KOSA LA JINAI.
Kwa kumbukumbu zangu zamani kidogo yaan miaka kama 18 nyuma kulikuwa na mshauri wa michezo aliitwa PAPE. Yy alikuwa Mjerumani kipindi hiko TFF ikijulikana kama FAT chini ya NDOLANGA. Hizo sheria ziliwekwa miaka hiyo ili kudhibiti ulanguzi wa kimichezo. Sheria hiyo ilikuwa mahsusi kwa timu za ligi kuu tu. Na pale mtu akitaka kumiliki lazima wawepo angalau watu wa 3. Kwa hiyo basi zinaruhusiwa kumilikiwa na mashirika au makampuni mbalimbali lkn sio mtu mmoja.
Hii ilikuja mara baada ya ALEX KAJIMULO kuimiliki KAJIMULO FC. Hivyo kupelekea maamuzi yasiyo ya kimichezo zaidi juu ya timu yake. Hata azam haimilikiwi na BAKHRESA kama yeye bali kampuni yake ya AZAM hali hiyo pia ni kwa ALLIANCE nayo inamilikiwa na kampuni sio mtu mmoja.
Kuweka mambo sawa ni kwamba MO anachofanya ni kwamba anaichukua timu kama yake binafsi na sio kama MO INTERPRISSES. Hii hairuhusiwi kwa kufikia hizo % anachotakiwa ni kugawana hizo share equally au semi equally na wanahisa binafsi wengine ambao hawako familia moja na yeye.
Yaan yy achukue 17% ANOTINO Achukue 17% MANENGELO 15%.
Nilichoona hapa ni kwamba sheria hii haikutumika ama kwa kutokujua au kwa makusudi ili kufanikisha jambo fulani kisiasa.
All in all MO ameikuta simba as super brand ambayo kupitia hiyo anaweza kutanua wigo wa biashara zake kupitia matangazo ya kwenye jezi kama ilivyokuwa kwa KILIMANJARO PREMIER LAGER. utofauti ni kwamba TBL wao walikuwa wanatoa vifaa vya michezo na pesa kama mdhamini ila Mo yy anafanya kama mmiliki yaan anaandikia as ameadd up CAPITAL. Fluctuation Capital ambapo kila mwaka huziingiza as gharama zake na hutolea wakati anatafuta faida kitu ambacho si sahihi.
Nimechambua kama mwanamichezo na sio kama SHABIKI.
UKITAKA ELEWA USIPOTAKA ENDELEZA USHABIKI MAANDAZI
Hebu rudia kusoma hiyo paragraph yako ya tatu mpaka ya nne uone ulichokiandika?
 
Hapana ila ww unakuwa mwenye nguvu regardless ya umiliki wa hisa pungufu ya 50% kwa maana mwenye 49% ni mmoja na wenye 51% ni wengi hivyo basi nguvu kubwa itaenda kwake
Hoja yako ilikuwa kumiliki timu peke yake kwahiyo akiwa majority shareholder anakuwa amemiliki timu peke yake ?
 
Wanaomuabudu "sauti ya ng'ombe" wamecharuka kama wametiwa upupu sehemu zile........[emoji23][emoji23]
 
Mbumbumbu fc leo hawapata usingizi kabisa kisa tu hili tamko la mwakyembe linamlenga mume wao mo
Halafu hawa Mikia Fc wakati Manji anabanwa na serikali, Mikia walikuwa wanachekelea, leo MO kabanwa wanaharisha, wako hoi ICU, sasa mbona hamchekelei kama mlivyochekelea wakati Manji anabanwa?
 
Mo si akaanzishe team yake awaachie Simba yao hao kina Kilomoni na Mwakyembe tuone wapi itaenda? Wenzetu huko duniani huu ujinga walishatupa huko. Team inamilikiwa 100% na mtu mmoja au familia yake. Pure business.
 
PhD yake haikusaidii kwasabb uelewa wako ni wa darasa la pili ..itakuwa ngumu sana kwako kumuelewa mwenye PHD. Ushauri rudi Shule ukuze ufahamu wako
Ndio maoni ya wasomi wetu haya!! Zero kabisa, huyu mtu wa darasa la pili mbona inaonekana anafikiria vizuri kuliko wewe ambaye unajinasibu umesoma.

Hiyo shule unayo mwambia arudi akasome inaonekana hata wewe imeshindwa kuku komboa kifikra.

Msituharibie mpira wetu!
Siasa kafanyieni kwenye majukwaa yenu ya ccm,chadema, cuf,act nk;
 
Ndio maoni ya wasomi wetu haya!! Zero kabisa, huyu mtu wa darasa la pili mbona inaonekana anafikiria vizuri kuliko wewe ambaye unajinasibu umesoma.

Hiyo shule unayo mwambia arudi akasome inaonekana hata wewe imeshindwa kuku komboa kifikra.

Msituharibie mpira wetu!
Siasa kafanyieni kwenye majukwaa yenu ya ccm,chadema, cuf,act nk;
MKUU MO ANAPOWEKEZA HIZO PESA NANI ANACHUKUA AS PART OF CAMPENSATION YA KULOOSE PART YA ILE KAMPUNI.? JE WANACHAMA WOTE WATAPATA GAWIO LA UUZAJI WA HISA? KWA MAANA KWENYE KAMPUNI MWENYE HISA HUAMAMUA KUUZA HISA ZAKE ILI APATE HELA FULANI. JE HUYO MO HIZO PESA NANI ATAMKABIDHI ZILE HASA ZA KUFIDIA UMILIKI WA TIMU? Kama ataweka tu mtaji wake means kwamba simba anaichukua bure kwa maana yy ameweka mtaji tu kama kukuta kibanda hakina mtu ukaanza kuuza bidhaa zako.
MO AACHE UJANJA UJANJA AANZISHE TIMU YAKE KAMA ANAONA RAHISI KUCHUKUA NDOO YA AFRICA
 
Ndivyo inavyotakiwa, safi sana....na uzuri ni kwamba hata ile janja janja ya watu watatu wenye uhusiano kifamilia, kindugu, kirafiki au kwa namna Fulani wanabanwa na sheria kununua hizo hisa kwa lengo la kupata asilimia 49.

Simba ni kubwa sana kuliko mtu moja, lazima hio asilimia 49 iwe na watu hata watano changamoto ziwepo.
 
Hakuna biashara kichaa kama kuwekeza kwenye mpira duniani kote kwani pesa inaanza kurudi sio chini ya miaka mitano tangu senti ya kwanza iwekezwe na wakati mwingine inaweza isirudi kabisa. Matajiri wengi wanaowekeza kwenye mchezo wa mpira wa miguu ni kwa sababu ya mapenzi yao kwenye mpira wa miguu tu na suala la faida huja baadae sana.

Kama ingekuwa ni rahisi kuwekeza kwenye mpira leo Vodacom na Serengeti Breweries wangekuwa na timu zao kwenye ligi kuu na hata timu za TBL (Plisner Dar na Ndovu Arusha) zingekuwa bado zipo na zinacheza ligi kuu. Lakini makampuni yote hayo (Voda na TBL) yaliona ni rahisi kudhamini ligi kuu na Serengeti waliona ni rahisi kudhamini timu ya taifa na si kudhamini vilabu kwani ni gharama kubwa sana.

Napata shida kumwelewa mtu anayesema ni lazima wawekezaji wawe watatu (3) katika asilimia 49. Je akipatikana mmoja tu au wawili tu huo uwekezaji hautaruhusiwa? Kuna makosa yaliwahi kufanyika kwa mkubwa mmoja kufuta michezo mashuleni ilituchukua zaidi ya miaka 10 kurudisha hali ilivyokuwa kabla japo kwenye riadha imeshindikana kabisa kurudi tulipokuwa. Hili la uwekezaji badala ya kuwavutia wawekezaji tunawafukuza sijui itatuchukua miaka mingapi kuwavutia wawekezaji na je wakati huo wawekezaji wenye wazimu na mpira dizaini ya MO watakuwepo?

Kwa sheria ya namna hii na matamko ya hivi karibuni kuwa Mo akaanzishe timu yake ni rasmi kuwa soka la bongo linaenda kaburini kwani sidhani kama wawekezaji makini watakuja kuwekeza kwenye vilabu vyetu na hivyo ligi itadorora na mwisho wa siku hata mdhamini wa ligi atakosekana. Hao wavurugaji wote hawajui kuwa baada ya Simba kufanya vizuri chini ya MO ligi yetu imeaanza kufuatiliwa na watu wengi sana Afrika na nje ya bara la Afrika. Na si hivyo tu wachezaji wazawa na wa kigeni zaidi ya kumi wameuzwa/wamepata vilabu nje ya nchi na hata baadhi ya mawakala wakubwa wa wachezaji wameanza kuiona Tanzania kama chimbo jipya la wachezaji wanaofaa kuuzwa sehemu mbalimbali duniani.

Kwa wanaojua mpira kiukweli Mo alijilipuwa sana kuwekeza kwenye mpira lakini vikwazo alivyowekewa vinatosha. Waliaanza asimiliki asilimia 51 akakubali baadae wamebadilisha kibao eti hiyo asilimia 49 wawe watatu. Aliye karibu na Mo amwambie aachane sasa na Simba pesa akawape tu watoto yatima atapata baraka kwa Mungu na atalipwa thawabu kuliko hizi figisu anazofanyiwa. Timu amuachie Kilomoni na genge la watu walimtanguliza mbele waendeshe timu ila wajue tu mshahara wa Kagere ni milioni 10 kwa mwezi na kuiendesha Simba kwa mwezi haitapungua millioni 300 kwa mwezi kwa hiyo zikiisha pesa za CAF 1.5 billioni wanazozipigia mahesabu itabidi waingie mifukoni mwao kuendesha timu.

Narudia tena aliye karibu na Mo amwambie aachane na soka la bongo atapata presha bure apeleke pesa zake kwa watoto yatima atapata thawabu kwa Mungu. Kichekesho watu wana asilimia 51 hawajaweka hata shilingi moja benki, hawajui timu anasafiri vipi, timu inakula nini, mishahara inalipwa vipi, fedha ya usajili inalipwa vipi eti wamekomaa Mo weka bilioni 20 benki wanasahau kuwa Mo ni mwekezaji mwenza na sio mnunuzi hivyo walitakiwa wao wawe wa kwanza kuweke japo hata billioni 5 tu. Wabongo tupo serious kweli?

Yaani nasikitika sana kuona kuwa ligi yetu itakapokosa msisimiko. Tutarudi tena kufuatilia ligi za wenzetu. Viwanja vitakosa watazamaji, soka letu litaporomoka kwani itakuwa sasa Boxer wa Yanga anamkaba Rashid Juma wa Simba badala ya boxer wa Yanga kumkaba Kagere. Mmiliki wa viwanja Tanzania atapoteza mapato kwa kiasi kikubwa sana n.k. Anyway kwa kuwa ndio tumeamua hivyo twendeni tu.
 
Back
Top Bottom