Haiwezekani Mungu asimuue Shetani halafu aamuru Watu waue wanaofanya mambo ya kishetani; Haiingii akilini

Mungu sio Kiongozi.
Mungu Muumbaji hapati chochote Kutokana na maamuzi yako. Maamuzi yako hayamuumizi Kwa chochote.

Mwanadamu ni mfano WA Mungu, vile ujionavyo ndivyo Mungu alivyo, Ila vile alivyo Mungu sivyo tulivyo sisi
Kama maamuzi ya mwanadamu hayamuumizi kwanin analishusha moto sodoma na gomora, kama maamuzi ya mwanadamu hayamuumizi kwanin kuna ziwa la moto kwa wale watakaokufa katika dhambi
 
Umejuaje kwamba hawazi sawasawa na kundi lake?

Ikiwa viongozi wametokana na jamii hiyo hiyo?
Jibu ni rahis mambo unayotegemea kwa akili zako za kibadamu afanye hafanyi anafanya kwa namna yake hio ni ishara hawazi sawa sawa na wewe na mwanadamu

Ndo maana wewe siku unayozaliwa huijui na siku ya kufa huijui hiyo ni ishara nyingine hafikiri sawa sawa na wewe mwanadamu ndo maana hutakaa umjue Mungu kwa akili zako za kibinadamu, wanaojaribu wote mwisho wa siku wanaishia kusema hamna Mungu
 
Ku question kila kitu ni tatizo
 
Kama maamuzi ya mwanadamu hayamuumizi kwanin analishusha moto sodoma na gomora, kama maamuzi ya mwanadamu hayamuumizi kwanin kuna ziwa la moto kwa wale watakaokufa katika dhambi

Kwa hiyo Mungu wa Sodoma na Gomora na huyu WA sasa hivi ni tofauti?
Dhambi za Sodoma na Gomora ni nzito kuliko dhambi za Watu wa sasa?

Mungu hawezi umizwa na viumbe wake. Huyo sio Mungu labda miungu.
 
Kwa hiyo Mungu wa Sodoma na Gomora na huyu WA sasa hivi ni tofauti?
Dhambi za Sodoma na Gomora ni nzito kuliko dhambi za Watu wa sasa?

Mungu hawezi umizwa na viumbe wake. Huyo sio Mungu labda miungu.
We unatatizo la kifikra Mungu wa sodoma na gomorah ndo yule yule wa leo, kwamba Mungu anabadilika hiki ni kituko kingine basi utakua unamuongelea Mungu mwingine sababu wako wengine kumbuka mim namuongelea Yahweh

Mungu alivyoadhibu sodoma na gomorah usitegemee atumie adhabu ile ile zama zinabadilikab nikusaidie hutakaa umjue Mungu kwa akili zako za kibinadamu na wewe sio wa kwanza kuja na hizo hoja dhaifu wako wengi mpaka kitabu wakatoa

Isaya 55
Njia zangu sio njia zenu mawazo yangu sio mawazo yenu,
 

🤣🤣🤣
Sawa tunajadili huyohuyo Yahweh Kwa sababu Yahweh pia anasifa za kibinadamu na ishathibitika kwenye vitabu Biblia.
Moja ya tabia za binadamu ni Wivu, hasira, kupenda, kuchukia, kughairi, kupumzika, kupendelea,

1. Yahweh WA zamani alikuwa anaua Watu hovyohovyo, Yahweh WA sasa hafanyi hivyo.

2. Yahweh WA zamani inasemakana alikuwa anatuma Malaika na kuongea na watu. Huyu wa sasa hatumi Malaika na wala haongei na watu.

3. Yahweh wa zamani Watu wake walikuwa Wayahudi. Yahweh's wa leo amewatelekeza Wayahudi.

4. Yahweh anasifa za kibinadamu kama kuwa na miguu, nywele zenye mvi.
Humohumo Mungu Muumbaji hafanani wala hafananishwi na chochote.

Yahweh anabadilika badilika na ishathibitika hivyo.
Ndio maana nikakuuliza Yule Mungu(Yahweh) aliyekasirishwa na Dhambi za Sodoma na Gomora na yupo wapi Zama hizi ambazodhambi ni zilezile zilizofanywa Sodoma na Gomora. He kabadilika?
 
Siwez thibisha kwenye kitabu chake cha biblia hakuna sehemu anabadilika au wamesema amebadilika
Wewe ndo umesema amebadilika alafu unalazimisha watu wakuamin huon kama ni kituko

Unashindwa kutofautisha agano jipya na la kale adhabu ziko pale pale tofauti zimehamia kwenye spiritual world kutoka kwenye mwili

Hatuwez amin maneno yako matupu, tunaamin biblia
 

Hiyo Biblia unayoisema hakuna agano la Kale wala jipya.
Watu ndio wameamua kutenga hivyo
Embu tuambie agano jipya linasemaje na agano la zamani linasemaje.

Mungu aliwahi kufanya maagano yafuatayo ni wanadamu Kwa kauli yake Mwenyewe Kwa mujibu wa Biblia;
1. Agano la Nuhu na Mungu, ishara ikawa ni upinde wa Mvua.
Mwanzo 9
17Mungu akamwambia Nuhu, Hii ndiyo ishara ya agano nililoliweka kati yangu na wote wenye mwili walioko katika nchi.

2. Agano la Ibrahim na Mungu, Ibrahim akaambiwa atahiriwe.

BHN


MWANZO 17​

Agano na tohara
9Kisha Mungu akamwambia Abrahamu, “Kwa upande wako, wewe utalishika agano langu, wewe binafsi, wazawa wako na vizazi vyao vyote. 10Hili ndilo agano utakaloshika kati yangu na wewe na wazawa wako: Kila mwanamume miongoni mwenu lazima atahiriwe. 11Mtatahiriwa kwa kukata magovi yenu, na hii itakuwa ndiyo alama ya agano kati yangu nanyi
3. Agano la Mungu na Musa, kupitia Torati ambalo ndio agano la milele.
Hili linaitwa Agano la Sinai. Utasoma kuanzia Kutoka Sura ya 19- Sura ya 24.
Hapo Mungu akampa Musa mkataba na Sheria zilizowekwa kwenye Sanduku la Agano

Embu tuambie Hilo agano jipya ni lipi. Lilikuwa baina ya Nani na Nani?
Na tunaomba Kauli ya Mungu moja Kwa Moja.
 

Mungu wa kwenye Biblia alisema endapo Adamu akila tunda atakufa, ni kweli anakufa.
Alafu baadaye kidogo anabadilika anasema MTU akifa hafi moja Kwa moja Bali atafufuliwa kwaajili ya hukumu, wapo watakaoenda Mbinguni na wapo watakaochomwa.
Hapo huoni kama Mungu kabadilika? Nazungumzia Mungu wa kwenye Biblia sio huyu Mungu muumbaji ambaye hajawahi kuonekana wala kuzungumza POPOTE pale
 
BIla kutaja vifungu vya bible na hiyo Quran ni blah blah tu za kawaida, kama ulivoita story za vijiweni.

ILa ni vizuri umewaza nje ya box.
 
Kwenye biblia kuna Mungu mmoja hayo ya wawili umesema wewe na unalazimisha tukuamini
 
Kwenye biblia kuna Mungu mmoja hayo ya wawili umesema wewe na unalazimisha tukuamini

1 Wafalme 11
5. Kwa kuwa Sulemani akamfuata Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni na Milkomu, chukizo la Waamoni.

Huyo pia yupo kwenye Biblia,
Yupo pia Dagoni Mungu wa wafilisti.

Rejea kifungu hiki kinachoonyesha miungu Ipo mingi.
Kutoka 20:3
[3]Usiwe na miungu mingine ila mimi.
Thou shalt have no other gods before me.

Unaposema kwenye Biblia yupo Mungu mmoja ni kwamba unajizima Data. Huyo Mungu wa kwenye Biblia (Yahweh) anatambua Ipo miungu mingine mingi tuu.
Sasa wewe na Yahweh Nani mkweli?
 
miungu iko mingi na kuna Yahweh mbona iko wazi, hao waliowataja hatuwafuati

Na amri ya kwanza yahweh anasema usiwe na Miungu mingine ila mim, amri ya kwanza Mungu ana aknowledge miungu mingine sasa wewe unashangaa nin sasa

Yahweh ndo aliyeumba dunia na ndo tunaomfuata na mtoto wake ni Yesu
 

Sasa mbona ulisema kwenye Biblia kuna Mungu mmoja Wakati huyo Yahweh anatambua Ipo miungu mingi?

Kila mungu anatamba hivyo kuwa aliumba Dunia.

Yahweh wapi alisema kuwa Yesu ni Mtoto wake
 
Huu Uzi unaonyesha ni kwa jinsi gani walio wengi hasa ndugu zetu upande WA pili bado hawajui concept ya kuumbwa kwao,!!! Na pia hata ukiwaelimisha bado wanakuwa wagumu kuamini!

Wanachokiona hakuwezekani kwa akili zao basi wanaona hakipo na nidharia tu.

Akili zao zipo ktk vitu vinavyoonekana na wao wanachokitafuta Duniani ni Hela ili wapate wanawake wazuri ,wanywe pombe ,kamari,nguruwe na umri wao uishie hivyo.......
 
Sasa mbona ulisema kwenye Biblia kuna Mungu mmoja Wakati huyo Yahweh anatambua Ipo miungu mingi?

Kila mungu anatamba hivyo kuwa aliumba Dunia.

Yahweh wapi alisema kuwa Yesu ni Mtoto wake
Tunamwabudu Mungu mmoja ambaye ni Yahweh
Ntajie hao miungu waliosema waliumba dunia tofauti na Yahweh kwenye biblia
 
Tunamwabudu Mungu mmoja ambaye ni Yahweh
Ntajie hao miungu waliosema waliumba dunia tofauti na Yahweh kwenye biblia

Kwa hiyo umeshahimisha swali na umekubali kuwa kwenye Biblia kuna miungu mingine mingi?

Quran inasema aliyeumba Dunia Ni Allah na sio Yahweh.
 
Jibu swali acha ngonjela
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…