MUNGU kama ulivyomuelezea hapo mwanzo kuwa hana Mwanzo na wala hana Mwisho. Yeye ni wa enzi wala hazuiliwi na Muda /nyakati...ni yeye ndiye aliyeumba Muda. Mungu hana Jana, leo wala kesho.
Tukija kwa Iblis , yeye ni kiumbe kilichoumbwa na Mungu na kabla ya Iblis tayari kuliwa na majini walikuwa wakiishi katika ardhi hii tunayoishi sisi, walifanya ufisadi mkubwa ardhini ,hivyo wakaja kupigwa vita na jeshi la malaika , wengi wakakimbilia visiwani, mapangoni ,majangwani na misituni.
Iblis ni jini kwani asili yake ni moto na mwanadamu asili yake ni Udongo. Ibilis alipata bahati ya kulelewa katika kundi la malaika huko mbinguni toka yungali mchanga mara baada ya uasi mkubwa uliofanywa na majini wenzake waliomtangulia hapa ardhini, alipewa elimu na alikuwa mchamungu sana. Mungu alipotaka kuumba kiumbe mwingine, malaika walipata shaka kidogo kuwa isije ikawa hawa wanadamu wakaja kufanya ufisadi kama waliofanya majini ardhini ikiwamo na umwagaji wa damu, Mungu alishaamua jambo lake na akawaambia kuwa hawajui yale anayoyajua yeye.
Mwanadamu baada ya kukamilika na kupuliziwa roho, akapewa mtihani pamoja na kundi la malaika akiwapo na jini (Iblis). Malaika na iblis walishindwa mtihani huo ila Adam alifaulu, hivyo out of respect to Adam wakaamriwa wamsujudie. Malaika walikubali kutii amri huku iblis akigoma na kuasi amri ya Mola wake kwa kigezo cha kuwa yeye ni bora kuliko Adam kutokana na kuumbwa kwa moto huku adam akiumbwa kwa udongo.
Kwanini MUNGU hakumuua Iblis tu mara baada ya kuasi?
Hii ni sawa na kuhoji kwa nini Mungu hawaui wanaadamu leo hii pale tu wanapofanya makosa?? Kwanini Iblis auawe na wewe usiuawe wakati wote mnatenda dhambi?
Jibu ni kuwa Mungu ameweka kila jambo katika wakati wake, Mungu ni mwenye subira na huwa hana haraka kwasababu kwanza hazuiliwi na Muda.
Iblis mara baada ya kuasi aliomba ombi moja kwa Mungu, nalo ni kupewa Muda mrefu wa kuishi mpaka pale ulimwengu utakapotamatika. Mungu alimkubalia ombi lake kwa kumjaalia kuwa ni miongoni mwa wale watakaoishi umri mrefu mpaka muda na wakati utakapofika nae atakufa.
Lengo la iblis lilikuwa ni nini katika ombi lake hili?
Iblis alikuwa tayari na uadui na mwanadamu kutokana na Mwanadamu kupewa cheo kikubwa mbele ya Mungu kuliko yeye, hivyo alishajenga uadui.Lengo lake lilikuwa ni kuja kupoteza uzao wa Adam wote ili aingie nao motoni.
Ila Mungu alimwambia kuwa utaingia motoni na wale tu watakaokufuata ila hana mamlaka na waja wake.