Haiwezekani Mungu asimuue Shetani halafu aamuru Watu waue wanaofanya mambo ya kishetani; Haiingii akilini

Mungu ni mjuzi wa yaliyopita na yajayo. Anajua matendo watakayotenda viumbe wake kabla hata ya kuwaumba.

Wanaadamu na majini wameumbwa ndani yao wakiwa na Roho na Nafsi. Nafsi ndio mimi na wewe....hii nafsi imepewa uchaguzi wa kutenda iwe mema au mabaya, kuamini au kukufuru.

Mungu alichofanya ni kuibainishia nafsi matendo mabaya na mazuri kisha akaipa uhuru wa kuchagua inataka kufata kipi ila akaionya kuwa katika kila chaguzi mwisho wake itakutana na pepo ama moto.

So mwanadamu na jini wana haki ya kutenda wanalolitaka ila mwisho watalipwa kwa yale waliyoyachagua.

Mwanadamu na Majini wamepewa uhuru wa kuchagua mema na Mabaya.
Lakini Mungu anajua hatma ya kila mmoja wao.
Yaani Mungu anajua wewe utachagua mabaya na utakuwa Mbaya.
Huoni maelezo haya ndio yanadhihirisha nilichoandika kwenye mada kuwa Mungu ndiye Shetani.

Hata vile kusema Mungu ni mjuzi WA yote inagongelea msumari kuwa Mungu ndiye Shetani.
Ukisema ujuzi wa yote unamaanisha mabaya na Mema, yawazi na yasirini.
Chanzo cha yote
Yaani maelezo yako yanafungua Watu zaidi ya nilivyo eleza
 
Naomba kujua kwanza

Je unaamini katika uislamu au ukristo

Maana huwezi jadili habari za Mungu na Sheteni ilihali wewe huamini kama kuna Mungu na Shetani!

Na kama unaamini je hujui mipaka ya kuhoji habari za Mungu na Shetani katika dini yako?

Sina Imani Kati ya hizo.
Mimi ni muumini wa Ukweli, Haki na Upendo.
 
Ok sasa kama huna imani na hizi dini kwanini unahoji maandiko matakatifu ya hizo dini?

Wewe umeujuaje huo ukweli,haki na upendo hadi usema ww ni muumini wa hayo mambo matatu?

Namaanisha nini chanzo cha ukweli,haki na upendo.
 
Acha makufuru

wewe ni binadamu tu unayekunya na kuharisha limited with time, you are not worthy of questioning an eternal God's wisdom.

Kwa nini unafikiri Mungu unayemuamini anaakili kama zako kuwa ninayoandika hapa yanamuumiza kama wewe unavyoumia?

Wewe ndio uache kuingilia Mambo yasiyokuhusu. Anayeelezwa hapa ni Shetani na Mungu wewe kinachokuuma ni kitu gani?

Shetani na Mungu ndio wanapaswa kuumia lakini sio wewe
 
Mwanadamu na Majini wamepewa uhuru wa kuchagua mema na Mabaya.
Lakini Mungu anajua hatma ya kila mmoja wao.
Yaani Mungu anajua wewe utachagua mabaya na utakuwa Mbaya.
Huoni maelezo haya ndio yanadhihirisha nilichoandika kwenye mada kuwa Mungu ndiye Shetani.

Hata vile kusema Mungu ni mjuzi WA yote inagongelea msumari kuwa Mungu ndiye Shetani.
Ukisema ujuzi wa yote unamaanisha mabaya na Mema, yawazi na yasirini.
Chanzo cha yote
Yaani maelezo yako yanafungua Watu zaidi ya nilivyo eleza

Sijui usipoelewa ni wapi ila ni concept ndogo tu.

Mungu ndiye Mjuzi wa kila kitu ,yaani elimu yake haina mipaka! Yaani anajua yaliyopita ,ya sasa na yajayo.

Sijui tunakubaliana katika hili?

Pia Mungu ndiye aliyeumba Muda /wakati...hivyo hawi controlled na Muda kama tulivyo viumbe ,yaani sisi tuna jana,leo na kesho... YEYE HANA HILO.

Nimekuelezea uumbaji jinsi ulivyo kuwa Mungu aliiumba nafsi ya jini na mwanadamu kisha akaibainishia nafsi hiyo juu ya mema na mabaya, kisha akaipa uhuru wa kuchagua inataka kufata wapi.

Hivyo Mungu ana prior knowledge ya machaguzi yetu kabla hata hatujaja hapa ulimwenguni, anaijua nafsi yako imechagua njia gani.l na mwisho wake ni wapi..Motoni au Peponi , ila mimi na wewe hatujui...tumeletwa duniani wote tukiwa na equal chance, Mungu hakulazimishi ww utende maovu au mema. Alichofanya ni kutuletea wajumbe (Mitume na Manabii) na vitabu vyake (torati,zaburi,injili na Quran) viwe ni muongozo kwetu...!!

Kwahiyo ni jukumu lako kuviamini au kuvikanusha ila kila chaguzi lako mwisho lina athari kwako mwenyewe kwani utakutana na Pepo au Moto.

Na hutakuwa na wa kumlaumu isipokuwa wewe mwenyewe maana ulipewa macho,masikio na akili ila kutokana na ujeuri na kiburi cha nafsi yako ukaamua kumkana Mungu na kumfuata shetani.

Simple tu.
 
Ok sasa kama huna imani na hizi dini kwanini unahoji maandiko matakatifu ya hizo dini?

Wewe umeujuaje huo ukweli,haki na upendo hadi usema ww ni muumini wa hayo mambo matatu?

Namaanisha nini chanzo cha ukweli,haki na upendo.

1. Ninahoji Kwa sababu hakuna sheria inayonizuia kuhoji Kwa Sisi tusioamini vitu bila kutumia Akili.

2. Ukweli unathibitika, na hautegemei Maoni na mtazamo wa Watu.
Haki na Upendo utaijua Kwa kuepuka Yale ambayo hautaki kufanyiwa usiwafanyie wengine. Na Yale unayotaka kufanyiwa basi wafanyie wengine.

3. Chanzo cha yote hayo ni Asili tuliyonayo wanadamu na Ulimwengu.
Hakuna haja ya Dini kumfanya binadamu awe mkweli, mwenye upendo na mwenye Haki
 
Matamanio ya nafsi yake ndio chanzo chake cha haki.

Quran: Al-Jathiyah 45:23

أَفَرَءَيْتَ مَنِ ٱتَّخَذَ إِلَٰهَهُۥ هَوَىٰهُ وَأَضَلَّهُ ٱللَّهُ عَلَىٰ عِلْمٍ وَخَتَمَ عَلَىٰ سَمْعِهِۦ وَقَلْبِهِۦ وَجَعَلَ عَلَىٰ بَصَرِهِۦ غِشَٰوَةً فَمَن يَهْدِيهِ مِنۢ بَعْدِ ٱللَّهِۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ

Je! Umemwona aliye fanya matamanio yake kuwa ndiye mungu wake, na Mwenyezi Mungu akamwacha apotee pamoja na kuwa ana ujuzi, na akapiga muhuri juu ya masikio yake, na moyo wake, na akambandika vitanga machoni mwake? Basi nani atamwongoa huyo baada ya Mwenyezi Mungu? Hamkumbuki?
 
Kupitia majibu namba 3.

Nieleze asili yako ww mwanadamu na Ulimwengu huu unao ishi.
 
Sijui usipoelewa ni wapi ila ni concept ndogo tu.

Mungu ndiye Mjuzi wa kila kitu ,yaani elimu yake haina mipaka! Yaani anajua yaliyopita ,ya sasa na yajayo.

Sijui tunakubaliana katika hili?

Pia Mungu ndiye aliyeumba Muda /wakati...hivyo hawi controlled na Muda kama tulivyo viumbe ,yaani sisi tuna jana,leo na kesho... YEYE HANA HILO.

Nimekuelezea uumbaji jinsi ulivyo kuwa Mungu aliiumba nafsi ya jini na mwanadamu kisha akaibainishia nafsi hiyo juu ya mema na mabaya, kisha akaipa uhuru wa kuchagua inataka kufata wapi.

Hivyo Mungu ana prior knowledge ya machaguzi yetu kabla hata hatujaja hapa ulimwenguni, anaijua nafsi yako imechagua njia gani.l na mwisho wake ni wapi..Motoni au Peponi , ila mimi na wewe hatujui...tumeletwa duniani wote tukiwa na equal chance, Mungu hakulazimishi ww utende maovu au mema. Alichofanya ni kutuletea wajumbe (Mitume na Manabii) na vitabu vyake (torati,zaburi,injili na Quran) viwe ni muongozo kwetu...!!

Kwahiyo ni jukumu lako kuviamini au kuvikanusha ila kila chaguzi lako mwisho lina athari kwako mwenyewe kwani utakutana na Pepo au Moto.

Na hutakuwa na wa kumlaumu isipokuwa wewe mwenyewe maana ulipewa macho,masikio na akili ila kutokana na ujeuri na kiburi cha nafsi yako ukaamua kumkana Mungu na kumfuata shetani.

Simple tu.

Mimi sina changu,
Yote nimepewa na Mungu,
Ukisema Nafsi yangu unamaanisha nini?
Nafsi, kiburi, Ujeuri vyote sio vyangu, hakuna nilichokimiliki na nitakachokimiliki.
Sasa unaposema Ujeuri au kiburi changu sijui unamaanisha nini?

Ndio hapo nikakuambia Mungu ndiye yote hata hicho kiburi nicha Mungu, Nafsi ni yamungu, hakuna ambacho sio chamungu Kwa sababu vyote aliviumba yeye.
Wapi hauelewi boss
W
S
 
Matamanio ya nafsi yake ndio chanzo chake cha haki.

Quran: Al-Jathiyah 45:23

أَفَرَءَيْتَ مَنِ ٱتَّخَذَ إِلَٰهَهُۥ هَوَىٰهُ وَأَضَلَّهُ ٱللَّهُ عَلَىٰ عِلْمٍ وَخَتَمَ عَلَىٰ سَمْعِهِۦ وَقَلْبِهِۦ وَجَعَلَ عَلَىٰ بَصَرِهِۦ غِشَٰوَةً فَمَن يَهْدِيهِ مِنۢ بَعْدِ ٱللَّهِۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ

Je! Umemwona aliye fanya matamanio yake kuwa ndiye mungu wake, na Mwenyezi Mungu akamwacha apotee pamoja na kuwa ana ujuzi, na akapiga muhuri juu ya masikio yake, na moyo wake, na akambandika vitanga machoni mwake? Basi nani atamwongoa huyo baada ya Mwenyezi Mungu? Hamkumbuki?
Shekh tatizo la huyu jamaa haamini katika Kitabu.

Hivyo basi hata uweke maandiko ya vitabu vyote bado ataoni ni pumba kwake ili hali ni Muongozo usio na shaka.
 
Kupitia majibu namba 3.

Nieleze asili yako ww mwanadamu na Ulimwengu huu unao ishi.

Ndio Mungu huyo ambaye ndiye chanzo cha Mimi.
Nikiwa Mbaya au mzuri yeye ndiye chanzo.
KWA sababu aliweza kuniumba atakavyo
Hata hivi ninavyofikiri sio Mimi Kwa sababu Mimi sina ninachomiliki. Na sina uwezo wa kuumba hata Wazo.
 
1. Ninahoji Kwa sababu hakuna sheria inayonizuia kuhoji Kwa Sisi tusioamini vitu bila kutumia Akili.

2. Ukweli unathibitika, na hautegemei Maoni na mtazamo wa Watu.
Haki na Upendo utaijua Kwa kuepuka Yale ambayo hautaki kufanyiwa usiwafanyie wengine. Na Yale unayotaka kufanyiwa basi wafanyie wengine.

3. Chanzo cha yote hayo ni Asili tuliyonayo wanadamu na Ulimwengu.
Hakuna haja ya Dini kumfanya binadamu awe mkweli, mwenye upendo na mwenye Haki
Kama kila mwanadamu atafuata matamanio yake yanavyomuelekeza kuwa nduo haki na upendo huoni kuwa huu ulimwengu ungekuwa ni wa fujo na ufisadi mkubwa?

Maana kuna wengine wanaamini wewe Robert heriel kuwa na mume ni haki kwako.

Kuna wanaoamini kukuibia na kukuua ni haki kwao

Kuna wanaoamini kuzini na mama zao ni haki kwao!!
 
Ndio Mungu huyo ambaye ndiye chanzo cha Mimi.
Nikiwa Mbaya au mzuri yeye ndiye chanzo.
KWA sababu aliweza kuniumba atakavyo
Hata hivi ninavyofikiri sio Mimi Kwa sababu Mimi sina ninachomiliki. Na sina uwezo wa kuumba hata Wazo.
Mungu yupi unaye mzungumzia hapa huyu wa Injili na Quran?
 
Mimi sina changu,
Yote nimepewa na Mungu,
Ukisema Nafsi yangu unamaanisha nini?
Nafsi, kiburi, Ujeuri vyote sio vyangu, hakuna nilichokimiliki na nitakachokimiliki.
Sasa unaposema Ujeuri au kiburi changu sijui unamaanisha nini?

Ndio hapo nikakuambia Mungu ndiye yote hata hicho kiburi nicha Mungu, Nafsi ni yamungu, hakuna ambacho sio chamungu Kwa sababu vyote aliviumba yeye.
Wapi hauelewi boss
W
S
Kama una amini kila kitu ni cha Mungu kwanini unahoji maamuzi ya Mungu ?

Kwanini unataka kumpangia Mungu nini cha kufanya katika ufalme wake?
 
Ufalme wa mbinguni na Ardhini wote ni wa Mungu, Yeye alishaamua kuumba ulimwengu katika hali hii, na ametupa mtihani wanadamu na majini ili aone ni nani atakayetenda mema miongoni mwetu.

Pia ameweka malipo kwa watakaoamini na kutenda mema kuwa wataingizwa peponi na kupata kila aina ya starehe na imma wale watakaomkanusha na wakatenda maovu bila ya shaka watakutana na adhabu kali.

Hayo ni maamuzi yake Mungu, yeye ndiye amepanga iwe hivyo...huwa haulizwi wala hakosolewi katika maamuzi yake kwasababu yeye ndiye mmiliki wa kila kitu.

Ila sisi viumbe ndio tutakaoulizwa kwa yale tuliyoyatenda.
 
Mimi sina changu,
Yote nimepewa na Mungu,
Ukisema Nafsi yangu unamaanisha nini?
Nafsi, kiburi, Ujeuri vyote sio vyangu, hakuna nilichokimiliki na nitakachokimiliki.
Sasa unaposema Ujeuri au kiburi changu sijui unamaanisha nini?

Ndio hapo nikakuambia Mungu ndiye yote hata hicho kiburi nicha Mungu, Nafsi ni yamungu, hakuna ambacho sio chamungu Kwa sababu vyote aliviumba yeye.
Wapi hauelewi boss
W
S
Kama unaamini Nafsi yako na kila kitu ni vya Mungu basi hivyo hivyo uheshimu maamuzi ya Mungu pale alipoamua kumuumba Iblis kuwa ni mtihani kwetu ili aone nani atakaetenda mema!!

Ni sawa na mtumwa kuhoji/kukosoa maamuzi ya mfalme.
 
Kwa nini unafikiri Mungu unayemuamini anaakili kama zako kuwa ninayoandika hapa yanamuumiza kama wewe unavyoumia?

Wewe ndio uache kuingilia Mambo yasiyokuhusu. Anayeelezwa hapa ni Shetani na Mungu wewe kinachokuuma ni kitu gani?

Shetani na Mungu ndio wanapaswa kuumia lakini sio wewe
ikiwa hayanihusu kwa nini unayaleta katika jukwaa huru? unataka nani asome! ukiandika upuuzi kubali kukosolewa la hutaki kukosolewa, wagawie upuuzi wako watu wa ukoo wako ambao nao si ajabu watakutema mate. maana ulichoandika ni ujinga na upuuzi mtupu.
 
Kuna source of everything. Hiyo SOURCE haina habari ya umungu wala ushetani. Mambo ya shetani na mungu ni akili ya mwanadamu ilianzisha ili kumkandamiza/kumtawala mwanadamu mwenzake.

Mungu ni cheo kama ilivyo shetani. Unayemuita mungu kwako ni shetani kwa mwingine, and vice versa.

Binadamu ni microcosm na source ni macrocosm. Kama source ilivyoweza kuumba kila kilicho ndani ya ulimwengu na wewe una uwezo wa kuumba vilevile.

Kinachoendelea ni kwamba binadamu wengi wameuza uwezo wao wa kuitawala dunia kwa kujikabidhi kwa viumbe vilivyotengenezwa (thought-forms) na wanadamu wenzao na kupewa jina la mungu.
 
Back
Top Bottom