Haiwezekani Mungu asimuue Shetani halafu aamuru Watu waue wanaofanya mambo ya kishetani; Haiingii akilini

Wewe unaweza kutengeneza roboti alafu ukalipa mtihani kisha roboti likifeli unaliadhibu. Wakati huohuo unajua matokeo kuwa litafeli au litafaulu.

Hiyo kitu inakuingia akilini kweli?
Yes inaingia akili. Ulipokua ukisoma mwalim wako alipokufundisha 1+1=2 kweny mtihan ukaweka jibu 11 nin kilitokea?
 
Swali la msingi, if shetani exists at all, aliwezaje kutenda dhambi sehemu takatifu? Uovu uliingia vp patakatifu? Kama iliwezekana uovu kupenya basi hiyo sehemu haikua takatifu to begin with.
 
HATA MAPEPO YESU HAKUYAUWA aliyaamuru yatoke!!!
Nashangaa leo watu wanataka wachawi wauwawe!!!

Watu wanataka mashoga wauwawe???
 
Swali la msingi, if shetani exists at all, aliwezaje kutenda dhambi sehemu takatifu? Uovu uliingia vp patakatifu? Kama iliwezekana uovu kupenya basi hiyo sehemu haikua takatifu to begin with.
Kosa la shetan ni kutaka kujifananisha na MUNGU, na yeye aabudiwe.
Ndipo alipotolewa akashushwa duniani. Elewa hakupunguziwa nguvu au uwezo Bali alipewa transfer kuja duniani na hii ndio sifa ya MUNGU.

MUNGU akikupa uwezo au nguvu flan amekupa, mfano Daudi mfalme hata baada ya Suleiman kuoa huku na huko agano la kuzamiwa YESU kwa hiyo familia lilitimia.

Mchungaji au nabii akipewa uwezo flan na Mungu huo uwezo utaendelea kuwepo haijalishi atakula kondoo.
MAANA YAKE ATANUTANA NA MUNGU at the end
 
Kwa mujibu wa maandiko dhambi inafanyika sehemu iliyokosa utakatifu, kama shetani aliweza kutenda dhambi mbinguni Ina maana mbinguni isn't perfect sio otherwise hata wazo la kutenda dhambi asingepata.
 
HAIWEZEKANI MUNGU ASIMUUE SHETANI ALAFU AAMURU WATU WAUE WANAOFANYA MAMBO YA KISHETANI; HAIINGII AKILINI!

Anaandika, Robert Heriel
Kuhani

Kwenye nyumba za ibada tangu tukiwa Watoto tulifundishwa kuna Wahusika Wawili mahasimu, wakwanza anaitwa MUNGU na wapili anaitwa SHETANI.

Mhusika Mungu huyu tuliambiwa ndiye Muumbaji wa Mbingu na Nchi, na ndiye Baba yetu (Chanzo chetu). Huyu tukaambiwa pia ni Mwema, mwenye upendo, nguvu na uweza. Chanzo chake hatujaelezewa, na hata wanaotuelezea habari zake hawajawahi kumuona. Hii ni kumaanisha hawajui anafananaje.

Mhusika Shetani huyu amepewa uhusika mbaya Kwa kusemekana alimuasi Mhusika MUNGU, asili ya Shetani wapo waliosema ni Jamii ya Malaika waitwao Makerubi, ambaye jina lake ni Lucifer. Wakati wengine wakidai Shetani au Ibilisi asili yake ni Kutoka Koo za majinni. Hii ni kusema Shetani ni kiumbe kilichoumbwa na Mungu. Ingawaje Stori hizi mbili hazijakamilika na zinaacha maswali mengi kuliko kilichoelezwa.

Lusifa kama aliasi, aliasi sheria ipi miongoni MWA sheria za Muumba wake huko Mbinguni?

Kabla hajaasi hiyo sheria ilitamka kuwa adhabu ya kuasi ni ipi?

Stori za Shetani zimeanzia juujuu na kuishia juujuu kama Stori za masela WA vijiweni. Yaani Stori imeanzia Kati na kuishi katikati.

Tukirudi kwenye Hoja.
Wasimulizi WA hizi dini zakuletwa na Waandishi wa vitabu vyao ambavyo vimeandika habari za huyo Mungu na Shetani Kwa uchache Mno, wakaja na sheria, ni kama sheria za biashara ya Market zile za Qnet. Unawekeza Kwa Imani pasipo kuuliza maswali yenye kufikiri, ATI hivyo ndio namna ya Kupata faida kwenye biashara.

Vitabu vya Dini vinaeleza kuwa Shetani ndiye chanzo cha dhambi, inakazia zaidi kuwa kila dhambi ifanywayo na binadamu chanzo chake ni Shetani kwani Shetani ndiye anayeshawishi Watu au viumbe kufanya Uasi.

Ukisoma kwenye Quran au Biblia yapo Makosa MTU akifanya anatakiwa kuuawa kama adhabu.
Mfano WA Makosa hayo ni kama kuua, kuwa Shoga au msagaji, kulala na mnyama, kuzini na mama mzazi au Baba mzazi au mkwe au mtoto wako. Kumkufuru Mungu na kuwa mchawi au mshirikina. Na Makosa mengine mengi yenye kustahili adhabu ya kifo Kwa mujibu wa vitabu vya Dini.

Swali linakuja, Ikiwa mhusika Mungu wa kwenye vitabu hivyo vya Dini, aliamuru Watu kuwaua Watu wenzao wanaofanya Makosa au dhambi nzito kama zilivyotajwa, ni Kwa nini huyu Mungu asingeshughulika na Shetani mwenyewe ambaye ndiye anawafanya Watu WAUE, wawe mashoga, na kufanya zinaa chafu ya kiwango cha juu?

Kwa sababu kama kweli Mungu hakutaka Dunia iwe na uovu kama ni kweli Kabisa basi ni dhahiri angedili na chanzo ambacho vitabu vya Dini vinamtaja ni mhusika Shetani.

Haiingii akilini badala ya kumuua Shetani ambaye ndiye chanzo cha Watu kufanya uovu mkubwa, ATI uwaamuru hao Watu wawaue Watu wenzao wanaofanya Matendo ya kishetani yaani wanaomfuata Shetani ambaye wamezaliwa wamemkuta na watakufa watamuacha. Hakuna mantiki kabisa ya Jambo Hilo.

Nafikiri Vitabu vya Dini vinashindwa kueleza ukweli Kati ya huu;
1. Binadamu ndio Shetani wenyewe. Lakini wametafuta Shetani bandia asiyeonekana ili wamsingizie.
Hoja hii haina nguvu Kwa sababu Mwanadamu hawezi kupambana na Mungu au Shetani yaani hawezi kupambana na matamanio yake yaliyomo katika Akili yake. Kwani matamanio na utashi ndio humuongoza MTU.

2. Mungu na Shetani ni Mhusika mmoja. Yaani Mungu ndiye Shetani na Shetani ndiye huyohuyo Mungu.
Vitabu vya Dini vinashindwa kuelezea ukweli huu labda Kwa kuogopa kuyafanya Maisha yataonekana hayana maana. Jambo ambalo nikweli kuwa Maisha ni ubatili.

Kama Mungu ndiye muumba wa yote na muweza WA yote tafsiri yake Ipo wazi kabisa.
Hii ni kusema, Mungu hawezi kumuua Shetani Wakati yeye ndiye huyohuyo Shetani. Na Shetani hawezi kumuua Mungu Wakati yeye ndiye huyohuyo Mungu.

Hoja hii inanguvu Kwa sababu, hata vitabu vya Dini vinaeleza kuwa Mungu aliumba Mema na Mabaya (ushetani) lakini akamwambia Mwanadamu achague Mema ili aweze kuishi.

Kumaanisha upande mzuri au Mwema wa Muumbaji wetu ndio wanadini waliuita Mungu na upande Mbaya wa Muumbaji wetu wakauita Shetani. Ni kama vile USO na kisogo ambavyo vyote vipo Kwa mhusika mmoja.

Haiwezekani Lusifa Awe Muasi hivihivi, lazima tujiulize huo Uasi ulitoka wapi ikiwa sio Kwa Muumbaji wake? Kwa sababu kiumbe hakina uwezo wa kuumba Jambo lolote liwe zuri au liwe Baya.

Taikon pumzika sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Mwenyezi Mungu Muumba wa Dunia na universe nzima haulizwi swali kwa maamuzi yake.... Knowledge yake ni massive no humans nor any other creation itashindana nae. Yeye hajibu maswali yetu, Sie ni viumbe wake na wafuasi. Mitume wote wamesema sana juu ya hili lakini humans are stubborn na hawataki kusikia.

Mwisho wetu tutasimama kujibu hoja zetu. Hiyo akili aliyokupa sio uitumie against HIM.. He's absolute, the owner and the fashioner.... Hujauliza swali, naona ni una push your own agendas about the creator.... Ni yeye tu atakayekujibu but in mean time, soma Bible yako, soma Q'uran Ina majibu yote na zaidi pia omba msamaha... Yaani unauhitaji haswa, no kidding!
Kosa kubwa lisilosameheka ni kumuhusisha na viumbe vyake, na umejitahidi kumu undermine na kumlinganisha na sheitwan 😢
 
Kwa mujibu wa maandiko dhambi inafanyika sehemu iliyokosa utakatifu, kama shetani aliweza kutenda dhambi mbinguni Ina maana mbinguni isn't perfect sio otherwise hata wazo la kutenda dhambi asingepata.
Lol... Hii inaongelea duniani baada ya sheitwan kutolewa...
 
Shetani anatoa wapi nguvu na utajiri?

Jibu lako ndio litahitimisha mada Hii kuwa Muumbaji ndiye huyohuyo Mungu na Shetani katika uhusika mbili tofauti ndani ya mhusika mmoja
Chunga ndimi Bro.. Usimfananishe Muumba wako na sheitwan... Be careful! Malipo yake ni mapana.
 
Hell is empty and all the Devils are here on earth.

Kiranga Akisemaga "Mungu Hayupo" watu hubisha sana na kumpinga hoja zake ..

Sasa naona baadhi yenu mmeanza kumwelewa huwa ana maanisha nini.
 
HAIWEZEKANI MUNGU ASIMUUE SHETANI ALAFU AAMURU WATU WAUE WANAOFANYA MAMBO YA KISHETANI; HAIINGII AKILINI!

Anaandika, Robert Heriel
Kuhani

Kwenye nyumba za ibada tangu tukiwa Watoto tulifundishwa kuna Wahusika Wawili mahasimu, wakwanza anaitwa MUNGU na wapili anaitwa SHETANI.

Mhusika Mungu huyu tuliambiwa ndiye Muumbaji wa Mbingu na Nchi, na ndiye Baba yetu (Chanzo chetu). Huyu tukaambiwa pia ni Mwema, mwenye upendo, nguvu na uweza. Chanzo chake hatujaelezewa, na hata wanaotuelezea habari zake hawajawahi kumuona. Hii ni kumaanisha hawajui anafananaje.

Mhusika Shetani huyu amepewa uhusika mbaya Kwa kusemekana alimuasi Mhusika MUNGU, asili ya Shetani wapo waliosema ni Jamii ya Malaika waitwao Makerubi, ambaye jina lake ni Lucifer. Wakati wengine wakidai Shetani au Ibilisi asili yake ni Kutoka Koo za majinni. Hii ni kusema Shetani ni kiumbe kilichoumbwa na Mungu. Ingawaje Stori hizi mbili hazijakamilika na zinaacha maswali mengi kuliko kilichoelezwa.

Lusifa kama aliasi, aliasi sheria ipi miongoni MWA sheria za Muumba wake huko Mbinguni?

Kabla hajaasi hiyo sheria ilitamka kuwa adhabu ya kuasi ni ipi?

Stori za Shetani zimeanzia juujuu na kuishia juujuu kama Stori za masela WA vijiweni. Yaani Stori imeanzia Kati na kuishi katikati.

Tukirudi kwenye Hoja.
Wasimulizi WA hizi dini zakuletwa na Waandishi wa vitabu vyao ambavyo vimeandika habari za huyo Mungu na Shetani Kwa uchache Mno, wakaja na sheria, ni kama sheria za biashara ya Market zile za Qnet. Unawekeza Kwa Imani pasipo kuuliza maswali yenye kufikiri, ATI hivyo ndio namna ya Kupata faida kwenye biashara.

Vitabu vya Dini vinaeleza kuwa Shetani ndiye chanzo cha dhambi, inakazia zaidi kuwa kila dhambi ifanywayo na binadamu chanzo chake ni Shetani kwani Shetani ndiye anayeshawishi Watu au viumbe kufanya Uasi.

Ukisoma kwenye Quran au Biblia yapo Makosa MTU akifanya anatakiwa kuuawa kama adhabu.
Mfano WA Makosa hayo ni kama kuua, kuwa Shoga au msagaji, kulala na mnyama, kuzini na mama mzazi au Baba mzazi au mkwe au mtoto wako. Kumkufuru Mungu na kuwa mchawi au mshirikina. Na Makosa mengine mengi yenye kustahili adhabu ya kifo Kwa mujibu wa vitabu vya Dini.

Swali linakuja, Ikiwa mhusika Mungu wa kwenye vitabu hivyo vya Dini, aliamuru Watu kuwaua Watu wenzao wanaofanya Makosa au dhambi nzito kama zilivyotajwa, ni Kwa nini huyu Mungu asingeshughulika na Shetani mwenyewe ambaye ndiye anawafanya Watu WAUE, wawe mashoga, na kufanya zinaa chafu ya kiwango cha juu?

Kwa sababu kama kweli Mungu hakutaka Dunia iwe na uovu kama ni kweli Kabisa basi ni dhahiri angedili na chanzo ambacho vitabu vya Dini vinamtaja ni mhusika Shetani.

Haiingii akilini badala ya kumuua Shetani ambaye ndiye chanzo cha Watu kufanya uovu mkubwa, ATI uwaamuru hao Watu wawaue Watu wenzao wanaofanya Matendo ya kishetani yaani wanaomfuata Shetani ambaye wamezaliwa wamemkuta na watakufa watamuacha. Hakuna mantiki kabisa ya Jambo Hilo.

Nafikiri Vitabu vya Dini vinashindwa kueleza ukweli Kati ya huu;
1. Binadamu ndio Shetani wenyewe. Lakini wametafuta Shetani bandia asiyeonekana ili wamsingizie.
Hoja hii haina nguvu Kwa sababu Mwanadamu hawezi kupambana na Mungu au Shetani yaani hawezi kupambana na matamanio yake yaliyomo katika Akili yake. Kwani matamanio na utashi ndio humuongoza MTU.

2. Mungu na Shetani ni Mhusika mmoja. Yaani Mungu ndiye Shetani na Shetani ndiye huyohuyo Mungu.
Vitabu vya Dini vinashindwa kuelezea ukweli huu labda Kwa kuogopa kuyafanya Maisha yataonekana hayana maana. Jambo ambalo nikweli kuwa Maisha ni ubatili.

Kama Mungu ndiye muumba wa yote na muweza WA yote tafsiri yake Ipo wazi kabisa.
Hii ni kusema, Mungu hawezi kumuua Shetani Wakati yeye ndiye huyohuyo Shetani. Na Shetani hawezi kumuua Mungu Wakati yeye ndiye huyohuyo Mungu.

Hoja hii inanguvu Kwa sababu, hata vitabu vya Dini vinaeleza kuwa Mungu aliumba Mema na Mabaya (ushetani) lakini akamwambia Mwanadamu achague Mema ili aweze kuishi.

Kumaanisha upande mzuri au Mwema wa Muumbaji wetu ndio wanadini waliuita Mungu na upande Mbaya wa Muumbaji wetu wakauita Shetani. Ni kama vile USO na kisogo ambavyo vyote vipo Kwa mhusika mmoja.

Haiwezekani Lusifa Awe Muasi hivihivi, lazima tujiulize huo Uasi ulitoka wapi ikiwa sio Kwa Muumbaji wake? Kwa sababu kiumbe hakina uwezo wa kuumba Jambo lolote liwe zuri au liwe Baya.

Taikon pumzika sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Nakuona moyo wako una uchungu kama nyongo, kwa uchungu huo moyo wako umejaa kufuru kwa kudhani kuwa kukufuru huko kutapunguza maumivu na uchungu wa moyo wako!! Unaikalia hukumu ya kutisha ya MUngu ambayo nafsi yako inajua kabisa kuwa unastahili hukumu!! Lakini nina habari njema kwa ajili yako!! ni kwamba YESU anakupenda na yuko tayari kukusamehe dhambi zako zote kama ukikubali kuja kwake na kutubu uovu wa moyo wako wote! Ukitubu na kumkaribisha Yesu kwenye moyo wako atakusamehe dhambi zako zote na ataingia moyoni mwako kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako!! Atakupa furaha, amani na burudiko la moyo ambalo hujawahi kulipata japo umelitafuta sana!! Vinginevyo hayo makufuru utowayo kwa muumba wako hayatakusaidia siku ya hukumu ambayo dhamiri yako inakushuhudia daima kuwa unastahili hukumu!!

Kama uko tayari kutubu omba kwa dhati sala hii ya toba: Bwana Yes, naja kwako, mimi ni mwenye dhambi. Ninakuomba unisamehe dhambi zangu zote ninazozijua na nisizozijua, ninazozikumbuka na ambazo sizikumbuki. Tangu sasa namkataa shetani na kazi zake zote. Ninamkubali Yesu na kumkaribisha moyono mwangu awe Bwana na Mwokozi wa maisha yangu. Bwana Yesu naomba ulifute jina langu kwenye kitabu cha hukumu na uliandike kwenye kitabu cha uzima. Asante Yesu kwa kunisamehe na naomba unipe nguvu ya kuishi maisha matakatifu. Ninaomba katika Jina la Yesu-Amina..

Kama umeomba sala hiyo ya toba kwa moyo wa dhati, haya ndiyo maombi yangu kwa ajili yako: Baba katika Jina la Yesu Kristo, namleta kwako ndugu huyu aliyetubu mbele zako. Ninaomba mkono wako wa uweza umguse na damu yako ya thamani imwoshe dhambi zote. Namwombea rehema zako zilizo nyingi sana! Ninavunja nguvu za giza ndani yake kwa Jina la Yesu Kristo, na minyororo ya uovu iliyomtesa kwa miaka mingi ikatike na awe huru kukuabudu na kukutukuza. Yalinde maisha yake tangu sasa na ujidhihirishe kwake katika namna utakayoona vema. Ninaomba katika Jina la Yesu -Amina.

Nenda zako kwa amani na Mungu akubariki. Nakukaribisha kwenye kanisa la TAG (Tanzania Assemblies of God lililo karibu na wewe kwa msaada zaidi na mafundisho. Nenda kajitambulishe hapo na Mungu atakubariki!!
 
Naona sasa watu wana anza kumwelewa Kiranga anaposema "Mungu hayupo"

Watu wanafunguka kiakili sasa, Ila mwanzoni walikuwa wabishi kweli[emoji23][emoji23]
 
ikiwa hayanihusu kwa nini unayaleta katika jukwaa huru? unataka nani asome! ukiandika upuuzi kubali kukosolewa la hutaki kukosolewa, wagawie upuuzi wako watu wa ukoo wako ambao nao si ajabu watakutema mate. maana ulichoandika ni ujinga na upuuzi mtupu.
Linapokuja swala la imani za watu emotions zinazidi upeo wa kufikiri.

Na mfano mzuri ni wewe.

Una ita huu Uzi ujinga kwa vile ume enda against imani yako na fikra zako.

By the way, mleta mada yuko huru kuleta mawazo yake, No matter yako against imani au mawazo yako..
 
Hell is empty and all the Devils are here on earth.

Kiranga Akisemaga "Mungu Hayupo" watu hubisha sana na kumpinga hoja zake ..

Sasa naona baadhi yenu mmeanza kumwelewa huwa ana maanisha nini.
Mungu hayupo, hizo habari za kuwepo Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote ni hadithi za uongo kuridhisha wasiotaka kuhoji mambo kwa kina kimantiki.

Ukianza kuhoji kimantiki kidogo tu unagundua huyo Mungu katungwa na watu, tena kijingajinga tu.
 
Nakuona moyo wako una uchungu kama nyongo, kwa uchungu huo moyo wako umejaa kufuru kwa kudhani kuwa kukufuru huko kutapunguza maumivu na uchungu wa moyo wako!! Unaikalia hukumu ya kutisha ya MUngu ambayo nafsi yako inajua kabisa kuwa unastahili hukumu!! Lakini nina habari njema kwa ajili yako!! ni kwamba YESU anakupenda na yuko tayari kukusamehe dhambi zako zote kama ukikubali kuja kwake na kutubu uovu wa moyo wako wote! Ukitubu na kumkaribisha Yesu kwenye moyo wako atakusamehe dhambi zako zote na ataingia moyoni mwako kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako!! Atakupa furaha, amani na burudiko la moyo ambalo hujawahi kulipata japo umelitafuta sana!! Vinginevyo hayo makufuru utowayo kwa muumba wako hayatakusaidia siku ya hukumu ambayo dhamiri yako inakushuhudia daima kuwa unastahili hukumu!!

Kama uko tayari kutubu omba kwa dhati sala hii ya toba: Bwana Yes, naja kwako, mimi ni mwenye dhambi. Ninakuomba unisamehe dhambi zangu zote ninazozijua na nisizozijua, ninazozikumbuka na ambazo sizikumbuki. Tangu sasa namkataa shetani na kazi zake zote. Ninamkubali Yesu na kumkaribisha moyono mwangu awe Bwana na Mwokozi wa maisha yangu. Bwana Yesu naomba ulifute jina langu kwenye kitabu cha hukumu na uliandike kwenye kitabu cha uzima. Asante Yesu kwa kunisamehe na naomba unipe nguvu ya kuishi maisha matakatifu. Ninaomba katika Jina la Yesu-Amina..

Kama umeomba sala hiyo ya toba kwa moyo wa dhati, haya ndiyo maombi yangu kwa ajili yako: Baba katika Jina la Yesu Kristo, namleta kwako ndugu huyu aliyetubu mbele zako. Ninaomba mkono wako wa uweza umguse na damu yako ya thamani imwoshe dhambi zote. Namwombea rehema zako zilizo nyingi sana! Ninavunja nguvu za giza ndani yake kwa Jina la Yesu Kristo, na minyororo ya uovu iliyomtesa kwa miaka mingi ikatike na awe huru kukuabudu na kukutukuza. Yalinde maisha yake tangu sasa na ujidhihirishe kwake katika namna utakayoona vema. Ninaomba katika Jina la Yesu -Amina.

Nenda zako kwa amani na Mungu akubariki. Nakukaribisha kwenye kanisa la TAG (Tanzania Assemblies of God lililo karibu na wewe kwa msaada zaidi na mafundisho. Nenda kajitambulishe hapo na Mungu atakubariki!!

Huko nilishatoka miaka mingi Mkuu. Safari yangu inaendelea na sasa Niko mbali Mno. Siwezi kurudi nilipotoka.
Mawazo uliyonayo nilikuwa nayo miaka kumi na tano iliyopita. Nikiwa nasoma SEKONDARI.
 
Back
Top Bottom