CyberTz
New Member
- Jun 14, 2024
- 4
- 3
Kumekuwa na wimbi kubwa la wahitimu wa vyuo vikuu na vya kati kuhitimu elimu zao bila kuwa na ujuzi wa kivitendo katika taaluma walizozichagua. Hali hii imesababisha changamoto kubwa mitaani, hasa katika mchakato wa kutafuta ajira.
Nitazingatia zaidi upande wa kada za teknolojia. Hii ni mojawapo ya fani zinazokua kwa kasi sana, lakini ukiangalia mazingira ya mafunzo, bado haionekani kama wahitimu wanatoka wakiwa na ujuzi wa kutosha wa vitendo.
Sehemu kubwa ya mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi hutegemea Industrial Practical Training (IPT), maarufu kama field. Kwa uhalisia, siioni kama muda huu unatosha kuwajengea wanafunzi ujuzi wa kina, kwa sababu muda mwingi wanaoutumia vyuoni ni mrefu zaidi kuliko wa field. Hii inapunguza nafasi ya kujifunza kwa vitendo kwa kiwango kinachotarajiwa.
Aidha, baadhi ya maeneo ya field ambayo wanafunzi hupelekwa, badala ya kuwapa uzoefu wa kitaaluma, hubadilika kuwa kazi za kawaida kama kuhamisha mafaili au kufanya kazi ndogo zisizohusiana moja kwa moja na taaluma zao. Hivyo, baadhi ya sehemu hizi ambazo zinapaswa kuwa msaada wa kujifunzia, badala yake zinakuwa hazina mchango mkubwa.
Nikitazama zaidi kada za sayansi na teknolojia, vyuo vina nafasi kubwa ya kuhakikisha wahitimu wanatoka wakiwa na uwezo mzuri wa vitendo, endapo vitakuwa tayari kuwekeza katika miundombinu na mazingira bora ya kujifunzia.
Kwa mfano, mwanafunzi anayesoma Computer Science, Network Engineering, Cyber Security au IT anaweza kuhitimu bila hata kufanya basic configuration ya switch au router, hata katika mazingira ya simulation kama Cisco Packet Tracer. Hili linafanya iwe vigumu kwa mhitimu huyo kuingia moja kwa moja sokoni akiwa tayari.
Ni muhimu kwa vyuo kuanzisha na kuimarisha maabara (labs) na workshops za kutosha kulingana na kila fani. Pia kuwe na ratiba maalum ya mafunzo ya vitendo ndani ya chuo, ili wanafunzi wajifunze kwa ku-practice zaidi kuliko kusikiliza nadharia tu.
Mfano mzuri ni baadhi ya vyuo kama UDOM, ambavyo vina Huawei Lab, Cisco Lab na nyinginezo. Hii inawasaidia wanafunzi ku-experience mazingira ya karibu na ya kiuhalisia. Hata hivyo, bado kuna vyuo ambavyo havijawekeza vya kutosha katika vifaa na vitendea kazi, jambo ambalo linawadhoofisha wanafunzi kitaaluma, Unakuta mwanafunzi mpaka anamaliza kozi ya miaka 3 au 4 hajawahi kuona Server au Switch halisia inafananaje, Hajawahi hata kitedesign SLocal Area Network na unatarajia aingie mtaani apate kazi, Kweli?.
Lakini pia, vyuo vinaweza kuanzisha kozi za ziada (soft skills na practical short courses) kama sehemu ya lazima au option B, ili kuwajengea wanafunzi ujuzi wa ziada unaoweza kuwasaidia kujiajiri au kuanza kazi haraka. Mfano wake ni graphics design, CCTV installation, access control systems, na nyingine nyingi. Hizi ni fani ambazo mtu anaweza kuanza kuzitumia hata bila kuajiriwa rasmi, na kumsaidia kujijengea network na uzoefu wa kazi.
Kwa ujumla, tatizo si elimu yenyewe, bali ni pengo kati ya nadharia na vitendo. Ikiweza kuzibwa, wahitimu wengi watakuwa na uwezo zaidi wa kujiajiri na kushindana katika soko la ajira.