Hajatokea na hatatokea Manipulator kwenye siasa kama Mobutu Seseko ila ngebe zake zote zilikoma baada ya Nyakati kumkataa

Lord Denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
23,491
Reaction score
57,973
Alitengeneza mamia ya vyama vya siasa ili kuidanganya dunia kuwa Congo kuna demokrasia na vyama vingi. Vyama vya siasa vya kidalali vilikuwa vinajifanya kushindana nae kwenye uchaguzi alafu vinatangaza kumuunga mkono.

Alitegeneza machawa wa kumsifia kila kona na kwenye kila jambo kiasi kwamba ulikuwa ukiona anavyosifiwa unaweza kudhani kuwa Wacongo ni Matajiri ambao hawana umasikini hata kidogo.

Alihonga vyombo vya habari vyote kuandika habari nzuri kuhusu yeye. Hakukuwa na chombo cha habari kilichothubutu kuandika habari mbaya. Vilivyojaribu vilifungiwa au wahariri wake kupotezwa.

Alihonga wanamuziki wa Congo kutunga na kuimba nyimbo za kumsifu. Kuanzia kwenye chama chake hadi mitaani. Congo nzima ziliimbwa nyimbo za kumsifu na kumuabudu.

Mobutu aifanya haya yote huku akiua, kuteka na kupoteza wapinzani wake wa kisasa. Mobutu alifanya haya yote huku akiwa amefanya mauaji ya Patrice Lumumba aliyekuwa mpinzani wake mkuu.

Kikubwa, nyakati zilipomkataa Mobutu hakuweza kupambana nazo. Aliondolewa madarakani kwa aibu.

Pichani chini ni Chief Hangaya.
20250605_141359.jpg
 
mabutu alikuwa anatembea na funguo za kila aina utazani askari wa magereza yani alikuwa na funguo mpaka za ofisi za wizara zote,na idara zote yani akiondoka kwenda nchi za nje mjue ofisi funguo anazo yeye.
 
Bi yenu anatumika na wazee wachache wenye maslahi yao binafsi.

Ningekua chawa wake ningemshauri achukue chochote anachoweza atimkie Dubai akale uzee wake kwa amani, Soon jumba bovu linaenda kumwangukia mtu na Wakati wa kulikwepa ndo huu.
 
Mobutu hakuwa mfumo, alikuwa mtu, hakujenga system, alijijenga yeye, hakujenga nchi alijijenga yeye. Huu mfano unaonyesha akili zako ziko chini ya wastani halafu gawa kwa mbili
 
Nani kakwambia Mobutu hakuwa Mfumo? Nani kakwambia hakujenga system?

We endelea kulamba viatu vya Amos Makalla hapo UVCCM. Uzi umekuzidi sana akili huu
 
Bi yenu anatumika na wazee wachache wenye maslahi yao binafsi.

Ningekua chawa wake ningemshauri achukue chochote anachoweza atimkie Dubai akale uzee wake kwa amani, Soon jumba bovu linaenda kumwangukia mtu na Wakati wa kulikwepa ndo huu.
Ni kikundi cha watu wachache sana wasiozidi 200 wanaolifanya hili Taifa liwe la hovyo namna hii.
 
Mobutu alikuwa ana advantage moja, kuwa yeye ndie alikuwa muamuzi wa kila kilichokuwa kinatokea, kwamba alikuwa ni ana full control.

Mwingine yeye sababu ya umbumbumbu wake wa asili mixer kukosa elimu amejikuta anazungushwa kama pia, kwa manufaa ya wachache anatumika kama chambo. Mwisho wa siku jumba bovu linakuja muangukia yeye.

Kuna usemi wa Akili za kuambiwa changanya na zako yeye ulimpita pembeni maana zake hana hivyo kubeba kila analoambiwa/shauriwa.
 
Kuota kumtoa rais aliyeapa hadharani halafu akakagua majeshi baada ya kiapo ni kupoteza muda.

Mungu pekee ndiye mwenye uwezo wa kumuondoa Rais pale ikulu nguvu zake zisizoonekana huzidi chochote anachokipanga binadamu.
 
Stay tuned.

Umesoma jarida la jana la African Report kuhusu walipofikia ICC kwenye kumkamata huyo muuaji wenu na washirika wake?

Au unaropoka ropoka tu hovyo humu?
 
Kumbe nguvu yako yote ya kufungua uzi kuhusiana na ICC inategemea majarida ya huko nje!!.

Pole sana, EU waliikatia misaada Tanzania baada ya October 29, juzi wamesema wanaendelea kushirikiana na serikali.

Kumbuka amri anayoitoa Rais ipo ndani ya katiba ya JMT, anaapa kulinda raia na mali zao. Kwa hiyo nyinyi na kuchoma kwenu mali za watu mlitegemea mpokelewe kama mashujaa mkipewa maua mekundu na mkipita juu ya zulia?.

Mnajua biashara ngapi zimefilisika kabisa kwa ule upumbavu wenu mlioufanya siku ile?.
 
Nakuonea huruma maana chanzo chako cha taarifa ni mpumbavu mwenzako Kenan Kihongosi.

Tunajua wewe ni mpumbavu ila kama kuzidi kuwa mpumbavu. Hakuna mahali kwenye Katiba panapompa mamlaka Rais au mtu yeyote kutoa amri kwa majeshi kuuwa watu
 
Alitengeneza mamia ya vyama vya siasa ili kuidanganya dunia kuwa Congo kuna demokrasia na vyama vingi. Vyama vya siasa vya kidalali vilikuwa vinajifanya kushindana nae kwenye uchaguzi alafu vinatangaza kumuunga mkono.

Alitegeneza machawa wa kumsifia kila kona na kwenye kila jambo kiasi kwamba ulikuwa ukiona anavyosifiwa unaweza kudhani kuwa Wacongo ni Matajiri ambao hawana umasikini hata kidogo.

Alihonga vyombo vya habari vyote kuandika habari nzuri kuhusu yeye. Hakukuwa na chombo cha habari kilichothubutu kuandika habari mbaya. Vilivyojaribu vilifungiwa au wahariri wake kupotezwa.

Alihonga wanamuziki wa Congo kutunga na kuimba nyimbo za kumsifu. Kuanzia kwenye chama chake hadi mitaani. Congo nzima ziliimbwa nyimbo za kumsifu na kumuabudu.

Mobutu aifanya haya yote huku akiua, kuteka na kupoteza wapinzani wake wa kisasa. Mobutu alifanya haya yote huku akiwa amefanya mauaji ya Patrice Lumumba aliyekuwa mpinzani wake mkuu.

Kikubwa, nyakati zilipomkataa Mobutu hakuweza kupambana nazo. Aliondolewa madarakani kwa aibu.

Pichani chini ni Chief Hangaya.
View attachment 3356674
Mbona kavaa nyeusi katikati ya Nyeupe?🤔
 
Back
Top Bottom