Lord Denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 23,491
- 57,973
Nani kakwambia Mobutu hakuwa Mfumo? Nani kakwambia hakujenga system?Mobutu hakuwa mfumo, alikuwa mtu, hakujenga system, alijijenga yeye, hakujenga nchi alijijenga yeye. Huu mfano unaonyesha akili zako ziko chini ya wastani halafu gawa kwa mbili
Ni kikundi cha watu wachache sana wasiozidi 200 wanaolifanya hili Taifa liwe la hovyo namna hii.Bi yenu anatumika na wazee wachache wenye maslahi yao binafsi.
Ningekua chawa wake ningemshauri achukue chochote anachoweza atimkie Dubai akale uzee wake kwa amani, Soon jumba bovu linaenda kumwangukia mtu na Wakati wa kulikwepa ndo huu.
Ni kikundi cha watu wachache sana wasiozidi 200 wanaolifanya hili Taifa liwe la hovyo namna hii.
Stay tuned.Kuota kumtoa rais aliyeapa hadharani halafu akakagua majeshi baada ya kiapo ni kupoteza muda.
Mungu pekee ndiye mwenye uwezo wa kumuondoa Rais pale ikulu nguvu zake zisizoonekana huzidi chochote anachokipanga binadamu.
Kumbe nguvu yako yote ya kufungua uzi kuhusiana na ICC inategemea majarida ya huko nje!!.Stay tuned.
Umesoma jarida la jana la African Report kuhusu walipofikia ICC kwenye kumkamata huyo muuaji wenu na washirika wake?
Au unaropoka ropoka tu hovyo humu?
Nakuonea huruma maana chanzo chako cha taarifa ni mpumbavu mwenzako Kenan Kihongosi.Kumbe nguvu yako yote ya kufungua uzi kuhusiana na ICC inategemea majarida ya huko nje!!.
Pole sana, EU waliikatia misaada Tanzania baada ya October 29, juzi wamesema wanaendelea kushirikiana na serikali.
Kumbuka amri anayoitoa Rais ipo ndani ya katiba ya JMT, anaapa kulinda raia na mali zao. Kwa hiyo nyinyi na kuchoma kwenu mali za watu mlitegemea mpokelewe kama mashujaa mkipewa maua mekundu na mkipita juu ya zulia?.
Mnajua biashara ngapi zimefilisika kabisa kwa ule upumbavu wenu mlioufanya siku ile?.
Mbona kavaa nyeusi katikati ya Nyeupe?🤔Alitengeneza mamia ya vyama vya siasa ili kuidanganya dunia kuwa Congo kuna demokrasia na vyama vingi. Vyama vya siasa vya kidalali vilikuwa vinajifanya kushindana nae kwenye uchaguzi alafu vinatangaza kumuunga mkono.
Alitegeneza machawa wa kumsifia kila kona na kwenye kila jambo kiasi kwamba ulikuwa ukiona anavyosifiwa unaweza kudhani kuwa Wacongo ni Matajiri ambao hawana umasikini hata kidogo.
Alihonga vyombo vya habari vyote kuandika habari nzuri kuhusu yeye. Hakukuwa na chombo cha habari kilichothubutu kuandika habari mbaya. Vilivyojaribu vilifungiwa au wahariri wake kupotezwa.
Alihonga wanamuziki wa Congo kutunga na kuimba nyimbo za kumsifu. Kuanzia kwenye chama chake hadi mitaani. Congo nzima ziliimbwa nyimbo za kumsifu na kumuabudu.
Mobutu aifanya haya yote huku akiua, kuteka na kupoteza wapinzani wake wa kisasa. Mobutu alifanya haya yote huku akiwa amefanya mauaji ya Patrice Lumumba aliyekuwa mpinzani wake mkuu.
Kikubwa, nyakati zilipomkataa Mobutu hakuweza kupambana nazo. Aliondolewa madarakani kwa aibu.
Pichani chini ni Chief Hangaya.
View attachment 3356674