Haji Manara alistahili kufukuzwa Simba kitambo

Haji Manara alistahili kufukuzwa Simba kitambo

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
[*]Haji huyuhuyu anaelalamikia uongozi wa Simba, alikuwa analipwa 700k bila vyeti

[*]Manara huyuhuyu ambaye kabla ya Simba hakuwa maarufu shida zake kubwa zilitatuliwa na MO kifedha kama kijana wake

[*]Manara huyuhuyu aliwahi kumtusi maneno mazito na kumdharau CEO wa Simba kwasababu za uanamke wake

[*]Manara huyuhuyu aliyekuwa hajulikani na dunia alikuwa akidhaminiwa na club hata katika mambo yake binafsi.

[*]Manara huyuhuyu aliyebebwa na brand ya Simba, alipewa mkataba wa 3mil, usafiri na house allowance kibao akagoma kwa kutaka awe huru kufanya kazi za inje pia.

[*]Manara huyuhuyu anaelalamikia Simba alitumika kama dalali kuihujumu timu kwenye baadhi ya mechi za derby na ile ya Keizer chief south kwa kupenyeza mrungula kwa baadhi ya wachezaji wacheze chini ya kiwango

[*]Manara huyu ndiye aliyetengeneza mkataba wa kubumba (300mil) ili kumshinikiza Mo avunje mkataba kwa bei kubwa zaidi (janja janja).. Ndiyo maana hakutaka kumpa Mo aushike zaidi ya kumuonesha kama kitambulisho na kurudisha mfukoni

[*]Kiufupi Manara hana shukrani alifika mahali masikio yake yakazidi kichwa kilichoyabeba!

[*]Manara alijiona ni sehemu ya muwekezaji simba hivyo alitaka kugawana faida jambo ambalo halipo kwa wawekezaji duniani kote!

INASHANGAZA SANA MANARA KUUSHUTUMU UONGOZI ULIOMBEBA PAMOJA NA MAKANDO HAYO.

Hivyo Manara popote alipo asisomeke wala kufanya press kwa brand ya Simba!

Manara alivalishwa brand ya Simba, Manara kavuliwa brand ya Simba, Jina la Simba liendelee!

Update!

Leo August 24 /2021 Manara na familia yake kahamia rasmi Yanga!

Hii inadhilisha namna simba
ilivyokuwa imekumbatia mchawi ndani ya club!
2896082_Manara (1).jpg
 
Haji hajatumia busara kabisa,angenyamaza ingependeza zaidi pia akumbuke Kuna kesho maisha yanaendelea.Leo anawakashifu watu kama moo lakini akumbuke kesho atawahitaji haohao wamsaidie.
Yaani anaanika siri za ofisi halafu kesho anategemea kufanya biashara na watu, yaani mtu awe tayari kufanya biashara na mtu mropokaji asiye na siri. Halafu kesho anategemea aingie kwenye siasa zenye siri lukuki za chama. sitaki kuamini albino wana shida kichwani
 
Kupitia kuropoka kwa haji manara ndo nimegundua umuhimu wa kile kiapo wanachosemaga viongozi wa serikali kwamba sitotoa siri za serikali kumbe kina mantiki kubwa sana na hapa haji inabidi ajiandae kuanguka kibiashara kwa promo zake kwani hakuna bosi atakaekuwa tayari kufanya nae kazi kwani anawaza kama ameweza kumzungumza mo kwa mabaya jee atashindwaje kunianika na mimi pindi tukishindwana
 
Back
Top Bottom