Haji Manara alistahili kufukuzwa Simba kitambo

Haji Manara alistahili kufukuzwa Simba kitambo

Hahahah Mwamedi bana!....

Analalamika anatumia pesa zake nyingi kwasababu anaipenda simba, si kibiashara, yani hapati kitu, no return, alafu hapohapo kayajaza matangazo kwenye jezi kama notice board!

Mbele mbam! Nyuma mbam! [emoji1][emoji1][emoji23][emoji23]
e88248d7d761e6b4cb749567c54c7747.jpg
 
Alichokifanya manara leo hakina tofauti na mtu ukatongoze mke wa mtu, akukubalie tena bila usumbufu, umpige rungu halafu siku moja ukiwa unapiga rungu afumaniwe na mumewe, aje aachike halafu aje kwako kutaka muishi wote kwa kuwa ameshaachika kwa mumewe kisa ni wewe wakati wewe unawaza kama aliweza kumdangaya mumewe akaja kwangu, jee itashindikana vipi atoke kwangu aende kwa mwingine? Hapo naona mwanaume utasema aaah wapi hapa hakuna mwanamke wa kukaa nae ndo haji manara huo mfano unamuhusu.
 
  • Haji huyuhuyu anaelalamikia uongozi wa simba, alikuwa analipwa 700k bila vyeti
  • Manara huyuhuyu ambaye kabla ya simba hakuwa maarufu shida zake kubwa zilitatuliwa na MO kifedha kama kijana wake
  • Manara huyuhuyu aliwahi kumtusi maneno mazito na kumdharau CEO wa simba kwasabu za uanauke wake
  • Manara huyuhuyu aliyekuwa hajulikani na dunia alikuwa akidhaminiwa na club hata katika mambo yake binafsi.
  • Manara huyuhuyu aliyebebwa na brand ya simba, alipewa mkataba wa 3mil, usafiri na house allowance kibao akagoma kwa kutaka awe huru kufanya kazi za inje pia.
  • Manara huyuhuyu anaelalamikia simba alitumika kama dalali kuihujumu timu kwenye baadhi ya mechi za derby na ile ya keizer chief south kwa kupenyeza mrungula kwa baadhi ya wachezaji wacheze chini ya kiwango
  • Manara huyu ndiye aliyetengeneza mkataba wa kubumba (300mil) ili kumshinikiza Mo avunje mkataba kwa bei kubwa zaidi (janja janja)..ndiyo maana hakutaka kumpa Mo aushike zaidi ya kumuonesha kama kitambulisho na kurudisha mfukoni
  • Kiufupi Manara hana shukrani alifika mahali masikio yake yakazidi kichwa kilichoyabeba!
  • Manara alijiona ni sehemu ya muwekezaji simba hivyo alitaka kugawana faida jambo ambalo halipo kwa wawekezaji duniani kote!
INASHANGAZA SANA MANARA KUUSHUTUMU UONGOZI ULIOMBEBA PAMOJA NA MAKANDO HAYO.

Hivyo manara popote alipo asisomeke wala kufanya press kwa brand ya simba!

Manara alivalishwa brand ya simba, manara kavuliwa brand ya simba, Jina la Simba liendelee!
Shabik maandaz katika ubora wako
 
Poleni sana bodi ya Simba joka mlilofuga wenyewe linaendelea kuwatafuna. Miaka mitatu/minne iliyopita sisi tuliokuwa tunaona mbali tuliwashauri hapa jamvini mumtimue huyo Manara wenu lakini hamkutuelewa na kuna wanajamvi walituzodoa hapa haya sasa yametimia. Lakini hongereni kwa kuchukua maamuzi magumu japo yamechelewa.

Nimemsikiliza Manara leo na kwa uelewa wangu mdogo nimeweza kupambanua mambo yafutayo:-
1. Manara ana hasira/jazba sana na Babra na anaamini kuwa Babra ndio kamuharibia ukaribu wake na Mo na pia Manara amejikuta anajenga chuki na Mo kwa sababu bado haamini kama kweli Mo naye kamtosa na hisia zake ni kuwa Mo kasikiliza majungu toka kwa Babra.
2. Manara hana kifua cha kutunza siri kama hulka ya wanaume wengi walivyo. Kwa hiyo walio karibu na Bakhresa na GSM wawaambie kabisa nao wajiandae ni suala la muda tu nao "press" za kuwachamba zitawahusu. Yaliyomkuta MO ambaye ni mtu wake wa karibu sana na wao yatawakuta huko mbele ya safari. Ikiwezekana Bakhresa na GSM wachukue tahadhari mapema akifika nyumbani kwao aishie nje hata sebuleni asiingie na kama ni ofisini aishie mapokezi tu asiingie ofisini kwao. Wakifuata ushauri wangu hawatajuta huko mbele ya safari. Na CCM nao wajitahidi asiwepo wakati wanafanya vikao vyao vya kimkakati. Ogopa sana ntu ambaye anongea kwanza halafu ndio anaanza kufikiri kile alichokiongea.
3. Manara ni mswahili kweli kweli na leo naona ilibaki kidogo tu afuatane na kigoma cha urugway na tarumbeta kwenda kuwazodoa Simba mbele ya waandishi wa habari.
4. Suala la kujitolea Simba bila kulipwa hilo ni uzembe wake mwenyewe kwani kuna mtu alimlazimsha kuendele kuwepo Simba.
5. Kitendo cha kufukuzwa kimemchanganya sana kisaikolojia na walio karibu naye wamtafutie mtaalamu amuweke sawa. Mbaya zaidi alikuwa anawatukana watu kwa kutumia mgongo wa Simba na alijua atakuwa Simba milele na timu aliichukulia kama mali yake binafsi sasa kitendo cha kufukuzwa wale watu aliokuwa akiwazodoa hasa waandishi wa habari nao wanajibu mapigo basi ndio anazidi kuchanganyikiwa kabisa.
6. Simba walikuwa sahihi kumtuhumu kuwa anaihujumu timu kwa sababu iwapo leo tu katoa siri zote Simba anazozijua mbele ya waandishi wa habari je vipi akiwa chemba anakula biriani ya ngamia na wakina Hersi na Ghalib halafu akapewa mshiko kidogo si atabwabwaja kila kitu.

Manara ana hoja kwenye mambo yafuatayo japo nayo ni kama kashayaribu kutokana na kuongea kwake mpaka kupitiliza:-
1. Suala la kudhulumiwa mshahara hilo angelipeleka mahakama ya kazi lingepatiwa ufumbuzi kisheria na kama ana haki zake angelipwa huko.
2. Manara ni mshamba na hana uelewa wa mambo japo kila siku anajisifu kuwa kazaliwa Kariakoo kwani suala la kudukuliwa ni suala la jinai na alitakiwa kushtaki polisi na TCRA kimya kimya. Sasa alivyo fala anaenda kushtaki kwa waandishi wa habari bila kujua kuwa anawapa nafasi watuhumiwa wake wafute ushahidi kama kweli upo na mwisho wa siku anaweza kujikuta yeye ndio mtuhumiwa kwa kutoa tuhuma za uongo.
3. Suala la wafanyakazi kumi kutimuliwa na wengine kuondoka kwa kipindi kifupi toka aingie Babra inabidi lifanyiwe uchunguzi na bodi ya Simba. Inawezakana aidha ni kweli Babra ana matatizo au Babra yupo "strict" sana kwenye usimamizi kiasi tunajua wabongo wengi wanafanya sehemu ya kzai ni kijwe badala ya kuwa sehemu ya kuwajibika.

Ushauri wangu wa bure kwa Bodi ya Simba, Mo na Babra msipoteze muda kabisa kujibishana na Manara endeleeni na kazi zenu.

Kwangu Manara awe amesema kweli au amesema uongo sio tatizo kabisa lakini tatizo kubwa ni pale alipoenda mbele ya waandishi wa habari na kuanza kutoa siri za mwajiri wake wa zamani. Hiyo ni kukosa weledi na kitendo cha kushindwa kutunza siri kitamuharibia sana huko mbele ya safari kwani hata marafiki zake, waajiri wake wengine na washirika wenzake kibiashara watakuwa wanakaa naye kwa taahadhari sana na baadhi ya michongo ataikosa.
 
Unazingua ww simba inatakiwa imuheshimu manara kwasababu alikuwepo toka simba wana shindia mihogo manji anatesa mjini hata mkude hakustahili anayopitia sasa ni baadhi ya watu waliovumilia simba kwa mda mrefu japo walikuwa na option ya kuondoka halafu babra anakuja, anakuta watu wameipambania timu analeta siasa zake hata mimi nisingekubali babra kaifanyia nn simba zaidi ya kulinda maslahi ya mo tu kuna watu wameipambania simba akiwemo manara na mkude.
 
Kupitia kuropoka kwa haji manara ndo nimegundua umuhimu wa kile kiapo wanachosemaga viongozi wa serikali kwamba sitotoa siri za serikali kumbe kina mantiki kubwa sana na hapa haji inabidi ajiandae kuanguka kibiashara kwa promo zake kwani hakuna bosi atakaekuwa tayari kufanya nae kazi kwani anawaza kama ameweza kumzungumza mo kwa mabaya jee atashindwaje kunianika na mimi pindi tukishindwana
Hakika
 
Alichokifanya manara leo hakina tofauti na mtu ukatongoze mke wa mtu, akukubalie tena bila usumbufu, umpige rungu halafu siku moja ukiwa unapiga rungu afumaniwe na mumewe, aje aachike halafu aje kwako kutaka muishi wote kwa kuwa ameshaachika kwa mumewe kisa ni wewe wakati wewe unawaza kama aliweza kumdangaya mumewe akaja kwangu, jee itashindikana vipi atoke kwangu aende kwa mwingine? Hapo naona mwanaume utasema aaah wapi hapa hakuna mwanamke wa kukaa nae ndo haji manara huo mfano unamuhusu.
Duuh huo mfano kiboko
 
Ila kawavua nguo simba na kama ni kweli aliyosema soon simba inaenda shimoni yanga itakua inajipigia tu kama zamani
Ndoto ya mwendawazimu hiyo. Maneno ya mropokaji, msaliti na mpuuzi hayawezi kuiangusha Simba. Najua uwekezaji wa Mo Simba umekuwa mwiba mchungu kwenu Utopolo, mtasubiri sana anguko la Simba.
 
Shida ya Manara ni kuinua mabega juu.
Yaani kujikweza tu basi.

Angekuwa mnyenyekevu Angekula sana pesa za Matajiri.

Kuna mambo yanahitaji subira ili kukaa sawa.
Manara anataka kila dukuduku yake itatuliwe leo leo.
 
Ivi mmewahi kufanya kazi na wahindi?; ni unprofessional sana.......Manara inawezekana yuko sahihi sema amechelewa kusema hayo
 
Back
Top Bottom