Hajia Manara aonekana Mwanachi Day japo adhabu yake inaendelea

Hajia Manara aonekana Mwanachi Day japo adhabu yake inaendelea

A
Katika Hali isiyo ya kawaida yule msemaji wa utopolo aliyepigwa marufuku kujihusisha na mambo ya mpira ndani na nje ya nchi Kwa muda wa miaka miwili, Leo ameonekana ndani ya uwanja wa mkapa akiwa na lundo la walinzi.. kwenu TFF
Acha wivu au nawe mtumwa wa TFF🤔
 
Hatakiwi hata kusikiliza Kipindi cha michezo radioni kama huo mchezo utakuwa wa miguu.😁

Adhabu kali ielekezwe hadi kwa Yanga na Manara mwenyewe.
Nyie watumwa wa TFF mnamatatizo sana na wengi wenu ni Wana 🦁
 
... adhabu yake ilikuwa kutojihusisha na na soka for 2 yrs. u-MC wake leo ilikuwa kuwatambulisha WACHEZAJI (wa soka) wa KLABU YA YANGA (ya soka), Uwanja wa Taifa kwenye MECHI (ya soka) kati ya YANGA (ya soka) na Vipers (ya soka).

Matukio yote yaliyofanyika Taifa leo keyword ni SOKA. Haihitaji hata kujua sheria, simple logic tu inatosha kufikia conclusion.
lakini cha ajabu eti anaruhusiwa kupost kwenye accounts zake mambo ya soka. Pia anaruhusiwa kuingia uwanjani kuchek mechi ya SOKA. Unalijua hilo?
 
MC wa harusi inasemekana kakimbia shughuli huko kigogo ..yaan hajamalizia shughuliii ...
 
Katika Hali isiyo ya kawaida yule msemaji wa utopolo aliyepigwa marufuku kujihusisha na mambo ya mpira ndani na nje ya nchi Kwa muda wa miaka miwili, Leo ameonekana ndani ya uwanja wa mkapa akiwa na lundo la walinzi.. kwenu TFF
Alilipwa as mc
 
Hii ni dharau kwa Shirikisho la Soka Nchini na kuharibu mpira wa miguu Tanzania.
Sikutegemea huo uongozi mpya wa Yanga, ungeruhusu hilo kutokea. Kwa hilo, inaonyesha ni kwa jinsi gani hawafai. Ile adhabu, hata kama ni ya uonevu, ilikuwa inatakiwa kufuata taratibu za kuipinga!
 
Ila mnajua kurukaruka, adhabu inaanza baada ya kupewa nakala, je nakala ameshapata ili adhabu ianze mbona mnarukaruka hapa!! Porojo nyingi, adhabu inaanza vipi wakati nakala hajapata! Je nauliza tena nakala yake ameshapewa!!!
 
Huyo hata akipelekwa FIFA atafungiwa Lakini analo kundi linalompa sapoti hasa hao viongozi wa Yanga, maana hao wangekua wanasimamia sheria lakini hawajali.
Hawa jamaa ni wahuni,
Ni dharau kubwa kwa mamlaka na ikiachwa hii,hali itakuwa mbaya zaidi huko baadae.
Ule usemi utanifanya nini? Ndio sasa utakuwa umetimia

Yaani utukane kiongozi kisha unaadhibiwa,halafu unapuuza adhabu,si ni practical ya kile ulichokisema kwa mdomo,sasa unatekeleza kisha uone watakufanya nini!
 
On serious note.
Uongozi wa Yanga wanapaswa kuadhibiwa kwa kudharau maamuzi ya TFF
Yanga ilidhaniwa kuwa imepata viongozi vijana na wenye weledi kumbe ni wahuni watupu. Viongozi wenye weledi hawawezi kuruhusu upuuzi wa aina ile
 
Yanga hawana mbadala wa Manara, wanaamini bila yeye hawawezi kushinda
 
Yanga sio wajinga na hio event haihusiani na ligi na wala TFF haiwahusu.

Ni sawa na kutaka kumfungia mtu kushiriki hata mambo binafsi ya kifamilia kama birthday ya watoto wake, n.k
Mambo ya mpira yanahusu TFF
Hata kwenye viingilio TFF wana mgao wao
 
Kisheria alikuwa anaruhusiwa kuja kama shabiki yani akae jukwaani

Ila hii ya kuja kwenye steji na kushika mic kuanza kusherehesha naona ni ishara ya jeuri kuipuuza mahakama

Nadhani wiki lijalo tutegmee kuona mfululizo wa misamaha tena.

Mashabiki wamejitokeza kwa wingi naona kafikiria akaona hii siku akiiacha ipite hivi hivi bila kuonekana wala kusema chochote ataonekana hana impact kwenye club

Kaamua kujitokeza ili baadaye awe na kauli ya kusema kupitia brand yake aliweza kushawishi umati mkubwa kuja uwanjani.

Mambo ya kiki haya ni kutafutiana lawama baadae uanze kulia TFF inamuonea kwasababu raisi ni shabiki wa Simba.

View attachment 2316274

View attachment 2316276
Umeandika kwa umakini mkubwa Sana[emoji106]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom