Uchaguzi Zambia 2026: Hakainde Hichilema ashinda Urais kwa muhula wa pili

Uchaguzi Zambia 2026: Hakainde Hichilema ashinda Urais kwa muhula wa pili

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Hakainde Hichilema ashinda Urais kwa muhula wa pili

Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema, ameshinda uchaguzi na kupata muhula wa pili wa miaka mitano, baada ya kupata asilimia 61.4 ya kura dhidi ya asilimia 38 alizopata mpinzani wake mkuu, Brian Mundubile. Tume ya Uchaguzi ya Zambia imemtangaza Hichilema kuwa Rais mteule.

Matokeo yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Zambia (ECZ)

Hakainde Hichilema (UPND) — 61.4% (Kura 2,965,326)
Brian Mundubile (PF) — 36.9% (Kura 1,856,217)


Baada ya kutangazwa kwa ushindi huo, wafuasi wake walijitokeza Lusaka kusherehekea, huku Hichilema akiwashukuru wananchi kwa kumuamini na kuwaahidi kuendelea kuwafanyia kazi.

1787030721589.png
Zambian President Hakainde Hichilema has been reelected for a second five-year term, the Electoral Commission of Zambia announced early Tuesday.

He was declared the outright winner of last Thursday’s presidential election without the need for a run-off, having secured 61.4% of the 5 million votes cast.

According to the commission, Hichilema won with 2,965,326 votes and his closest competitor was opposition leader Brian Mundubile, who won 1,856,217 votes.

“I therefore declare, Hichilema Hakainde S, to be president-elect of the Republic of Zambia this 18th day of August, 2026,” commission chairperson Mwangala Zaloumis said.

Hichilema’s victory follows a closely watched election which saw the vote counting suspended last Friday and then restarted hours later under heightened security after the commission said there had been attacks against some polling station officials and some ballot papers had been stolen.

Chanzo: apnews.com

=================

Tume ya Uchaguzi ya Zambia (ECZ) imetangaza matokeo ya awali ya uchaguzi wa Rais kutoka majimbo, huku mgombea wa chama cha United Party for National Development (UPND), Hakainde Hichilema, akiendelea kuongoza.

Matokeo kutoka majimbo 135 kati ya 226, kama yalivyotangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Zambia (ECZ).

Ulipolala, kura hazikulala Hakainde Hichilema (HH) sasa ana kura 1,544,140 (58.9%), huku Brian Mundubile akiwa na kura 1,030,662 (39.3%). Tofauti ya kura imeongezeka zaidi ya mara mbili usiku kucha — kutoka 225,971 hadi 513,478.

Soma>> Maaskofu Wakatoliki Zambia: Hali iliyojitokeza baada ya uchaguzi imeweka mashaka kuhusu uadilifu wa mchakato huo

Majimbo 91 bado yamebaki
, hivyo endeleeni kufuatilia; nasi tutaendelea kuwa hapa.

Morning Zambia ☕ Results from 135 of 226 constituencies as announced by ECZ.You slept, the num...jpg
Morning Zambia ☕ Results from 135 of 226 constituencies as announced by ECZ.You slept, the num...jpg

Matokeo kutoka majimbo 161 kati ya 226, kama yalivyotangazwa na ECZ:

Hakainde Hichilema (HH): 2,057,986
Brian Mundubile: 1,190,920
Tofauti ni kura 867,066.

Awamu ya hivi karibuni ilikuwa ngumu sana kwa Mundubile—kati ya kura 680,669 zilizotangazwa, takribani robo tatu zilikwenda kwa HH.

Namba muhimu ya kuangalia ni 50%, kwasababu ndiyo inayoweza kuamua iwapo kutakuwa na marudio ya uchaguzi. Kwa sasa, HH yuko kura 405,831 juu ya nusu ya kura zote zilizohesabiwa. Haya bado si matokeo ya mwisho.

Mundubile ameendelea kushuka kutoka 43.1% hadi 39.3%, na sasa 36.0% katika awamu tatu zilizopita za matokeo.

Uhesabuji wa kura unaendelea.

1786972695535.png

Rais Hakainde Hichilema anapata uungwaji mkono mkubwa sana katika Mkoa wa Kusini (97%), Mkoa wa Magharibi (97%) na Mkoa wa Kaskazini-Magharibi (96%).

Hizi si ushindi wa kawaida tu, bali ni ushindi wa kishindo unaokaribia kukamilika kabisa. Matokeo bora zaidi ya Brian Mundubile kufikia sasa ni katika Mkoa wa Luapula (71%), huku Mkoa wa Mashariki ukimpatia idadi kubwa zaidi ya kura—jumla ya kura 307,103—zikimpa asilimia 65 ya kura za mkoa huo.

Eneo linaloshuhudia ushindani mkali zaidi bado ni Mkoa wa Lusaka, ambapo HH anaongoza kwa kura 174,699 dhidi ya kura 160,548 za Mundubile. Wakati huo huo, Mkoa wa Muchinga na Mkoa wa Mashariki bado hayajaongeza matokeo mapya tangu taarifa ya awali, ikimaanisha kuwa bado kuna kura zinazosubiri kuhesabiwa na kutangazwa.


1786973832774.png

1786973840618.png
Vyanzo: Zambian Corner na Phoenix FM Zambia
 
Kwa tofauti kubwa ya hizo kura HH kashinda tena uchaguzi sema wazambia wao yeyote anashinda uchaguzi iwe upinzani au chama kilichoshika dola huyu HH alimuangusha mtu mwenye dola alikua upinzani leo yeye ananyatiwa na mpinzani tena..
 
Katika aspect ya kiuchumi , nini kimebadilika kwa wananchi?
All in all Wazambia sio wa kujifananisha na Watanzania wao wapo wachache na vitu vingi wanafanya kwa ajili ya Wananchi..
Wametengeneza bara bara kubwa nyingi kwa kiwango bora..
Wameongeza kilimo cha mahindi na wateja wao wakubwa ni Kenya.
Bei ya Shaba kuwa imara kupelekea pesa yao kuwa na nguvu kuliko Nchi nyingi za Afrika.
Wamepunguza kodi kwenye magari kwa kutumia mfumo wa GVM wao kuingiza Fortuner ya 2023 wanalipia sawa na Tsh 12m wakati Tanzania gari hiyo hiyo inazidi Tsh 40m.
Standard of living imeongezeka kwa asilimia chache maana wanaweza kutumia vitu bora kwa gharama ndogo..
Vipo vingi nikifananisha na Nchi zingine naona wao wanaenda vizuri..
 
Tume ya Uchaguzi ya Zambia (ECZ) imetangaza matokeo ya awali ya uchaguzi wa Rais kutoka majimbo, huku mgombea wa chama cha United Party for National Development (UPND), Hakainde Hichilema, akiendelea kuongoza.

Matokeo kutoka majimbo 135 kati ya 226, kama yalivyotangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Zambia (ECZ).

Ulipolala, kura hazikulala. HH sasa ana kura 1,544,140 (58.9%), huku Brian Mundubile akiwa na kura 1,030,662 (39.3%). Tofauti ya kura imeongezeka zaidi ya mara mbili usiku kucha — kutoka 225,971 hadi 513,478.

Ramani bado inaonyesha majimbo matano kwa kila upande, lakini fuatilia kwa karibu Lusaka — Mundubile amepunguza tofauti hiyo hadi kura 9,867.

Majimbo 91 bado yamebaki, hivyo endeleeni kufuatilia; nasi tutaendelea kuwa hapa.

View attachment 3651658View attachment 3651659

Vyanzo: Zambian Corner na Phoenix FM Zambia
Hawa watu walikuja October kujifunza mambinu
 
Kwa tofauti kubwa ya hizo kura HH kashinda tena uchaguzi sema wazambia wao yeyote anashinda uchaguzi iwe upinzani au chama kilichoshika dola huyu HH alimuangusha mtu mwenye dola alikua upinzani leo yeye ananyatiwa na mpinzani tena..
Alianza chiluba 1990s kukiondoa chama tawala madarakani hadi leo hichilema,na hakuna chochote cha maana Zambia,hata huduma za afya za kibingwa wanakuja kutibiwa Tanzania na ugali wa uhakika ni mpaka huku tuvune vizuri
 
All in all Wazambia sio wa kujifananisha na Watanzania wao wapo wachache na vitu vingi wanafanya kwa ajili ya Wananchi..
Wametengeneza bara bara kubwa nyingi kwa kiwango bora..
Wameongeza kilimo cha mahindi na wateja wao wakubwa ni Kenya.
Bei ya Shaba kuwa imara kupelekea pesa yao kuwa na nguvu kuliko Nchi nyingi za Afrika.
Wamepunguza kodi kwenye magari kwa kutumia mfumo wa GVM wao kuingiza Fortuner ya 2023 wanalipia sawa na Tsh 12m wakati Tanzania gari hiyo hiyo inazidi Tsh 40m.
Standard of living imeongezeka kwa asilimia chache maana wanaweza kutumia vitu bora kwa gharama ndogo..
Vipo vingi nikifananisha na Nchi zingine naona wao wanaenda vizuri..
Hii ni fantasy bro, Zambia mahindi wanategemea Tanzania na barabara za tz ukizipeleka Zambia basi itakua lami hadi vichochoroni
 
Alianza chiluba 1990s kukiondoa chama tawala madarakani hadi leo hichilema,na hakuna chochote cha maana Zambia,hata huduma za afya za kibingwa wanakuja kutibiwa Tanzania na ugali wa uhakika ni mpaka huku tuvune vizuri
Watanzania huwa mnajidanganya sana sijui shida nini aisee Wazambia wanalima mahindi ya kutosha na pia katika mboga mboga wao Samaki wanao wa kutosha mpaka ilifikia kipindi watu wa mbeya wauza samaki walianza kuchukua samaki Zambia baada ya kupigwa marufuku wakakimbilia Mozambique..
Samaki ambae utakula livingstone kwa kwatcha 50 sijui Tanzania utalipia ngapi hao kuku wa kienyeji hawathamini wanawaita chicken village...
Wazambia wanaamini katika supermarket ndio maana Lusaka tu wana malls nyingi sana..
 
Samia alijitangazia matokeo ndani ya siku tatu alooo 🙌🙌🙌
 
Hii ni fantasy bro, Zambia mahindi wanategemea Tanzania na barabara za tz ukizipeleka Zambia basi itakua lami hadi vichochoroni
Chakula wao sasa hivi wanalima sana kuna kipindi walikua na tatizo la mvua ndio tuliwauzia mahindi ila kwa sasa wana mahindi ya kutosha mimi napita hapo kila mwezi kuhusu Nchi za kusini nazunguka kama kariakoo na Mwenge...Nchi ambayo chakula ni tatizo ni DRC pekee na soko kubwa wameshika wao Tanzania na SA wanapeleka unga kutokea SA..
 
Hii ni fantasy bro, Zambia mahindi wanategemea Tanzania na barabara za tz ukizipeleka Zambia basi itakua lami hadi vichochoroni
Zambia wamewapa wachina wanajenga bara bara zao kwa kutoza kodi ya tolls kila mji kuna toll gate 11 kutokea Livingstone mpaka Nakonde na sehemu ambayo bara bara yao mbovu ni mpika mpaka unaitafuta Chinsali kuanzia hapo bara bara pana mpaka Tunduma..
 
Back
Top Bottom