sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Jacqueline Ntuyabaliwe ambaye ni mjane wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu nchini, marehemu Reginald Mengi, ameshinda pingamizi alilowekewa na wasimamizi wa mirathi katika rufaa ya mirathi ambao ni Abdiel Mengi (mtoto wa marehemu Mengi wa mke wa kwanza) na Benjamin Abrahamu Mengi (ndugu wa marehemu Mengi)
Ameshinda pingamizi hilo baada ya Mahakama kukataa hoja zote saba za pingamizi la wasimamizi wa mirathi.
Hii ni mara ya pili kwa mjane huyo kushinda pingamizi kutoka kwa wasimamizi wa mirathi hiyo wanaopinga kusikilizwa maombi yake ya mapitio.
Mahakama hiyo itasikiliza maombi ya mapitio ya Jacqueline na wanaye kwa tarehe itakayopangwa na Msajili wa Mahakama hiyo, ambayo ndiyo itatoa hatima ya uhalali wa wosia huo na uhalali wa Abdiel na Benjamin kuwa wasimamizi wa mirathi.