Bams, sijui niseme umetoa 'mahubiri' (sermon), au hotuba ya kuamsha mori wa askari wanaoelekea vitani. Sina shaka jambo hili umeliwaza kiumakini mkubwa hadi kufikia hatua hii ya kutoa mifano uliyoitumia.
Tupo wengi tunaojiuliza nchi yetu hii imekuwaje hadi ifikie hapa, lakini tunayaona yanayotokea na kuzidi kutikisa kichwa kwa kutoamini yanatokea kweli.
Sitaandika mengi, ngoja niweke machache haya.
1. Ule mfano wa kitu cha thamani kubwa (HAKI) wanachonyang'anywa waTanzania na wasijue cha kufanya..., anayenyang'anya haki hiyo "Hakimbii" badala yake ananyang'anya kwa nguvu huku akielekeza mitutu ya bunduki kwa yeyote atakayejaribu kuitafuta haki hiyo. Hii ndio mbinu inayotumika sasa na kwa mafanikio makubwa katika kuwatia woga waTanzania.
Itakapotokea, siku moja akatokea mwananchi aliyetiwa kichaa kwa kuporwa haki yake na kusema liwalo na liwe, pengine huo ndio utakaokuwa mwanzo wa wengi kuiichukua haki yao bila kujali mitutu inayoonyeshwa mbele zao.
Tuchukulie mfano huu: tuseme kijiji au vijiji kadhaa katika wilaya moja walianzishe kwa kusema hawatakubali kunyang'anywa haki zao, hawa wanyang'anyi watadharau na kuendelea na dhuruma yao? Mfano mmoja kama huu ukitokea sehemu moja, kitakuwa kichocheo kikubwa sehemu mbalimbali nchi nzima.
Hapajatokea mfano, ndio maana hawa 'walevi' wa madaraka watazidisha ulevi wao.
2. Nadhani katika kuandika kwako kwamba "mtu mmoja, mtendaji" kuwanyang'anya haki kundi zima la wananchi na wasimfanye lolote..., utakuwa umesahau kauli iliyotoka juu wiki chache zilizopita kwamba "yeyote atakayemnyanyasa mwanachama wa CCM," akakiona..." Habari hii iliwekwa humu JF na 'clip' ya video ilionyeshwa.
Huu ulikuwa ni ujumbe mahsusi uliolenga nyakati hizi. Usifikiri ujumbe kama huo hao watendaji huko vijijini hawakuupokea. Kwa hiyo wanapofanya wanayoyafanya sasa wanajua wanayo kinga isiyohojiwa.
Nimependa mfano huo wa aliyowaambia wale wanafunzi walipokutana na Mwalimu Nyerere.
Tupo njiani, na nadhani hatuko mbali sana...somebody will call the bluff and see what happens. That will be the beginning of the end...