Haki inahitaji kuonekana Imetendeka hata kama ni kwa Kutoana Kafara - Kwa manufaa ya Kesho Yetu

Haki inahitaji kuonekana Imetendeka hata kama ni kwa Kutoana Kafara - Kwa manufaa ya Kesho Yetu

Logikos

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
17,572
Reaction score
27,416
Justice needs to be Seen to be Done.....

Ni mengi yametendeka hivi karibuni wala hayahitaji maelezo, kuna wengi waliopoteza ndugu zao na jamaa zao (hata tukisema hao jamaa walikuwa waharifu basi ni vema tungewashika na kuwashitaki)...

Sasa sababu tumeshafika hapa na tunahitaji kuponyana na kuanza upya kama Jamii inabidi wale waliopoteza watu wao, tuweze kuwaonyesha kwamba tupo nao na kuna haki inatendeka...

Tufanye Nini ?
Mvua (Vifungo) vitembee kwa watu wa kutosha waliopo / waliokuwepo katika sehemu za wadhifa mbalimbali hata kama hawakuhusika moja kwa moja lakini wawajibike kwa manufaa ya nchi. Kwahio ni vema hawa watawala wakakaa pamoja na kuona ni nani wa kuwatoa kafara (au wahusika wa makosa yaliyofanyika ni kina nani ili kuwawajibisha); Bila hivyo vidonda vya watu havitapona...

Nilishasema haya hapo kabla, lakini nadhani tumeshavuka hapo, Kama ni Mguu unahitaji kukatwa sababu kuufunga bandage pekee sio suluhisho...

 
Back
Top Bottom