Haki mojawapo ya Mbunge ni kutetea Wananchi wake na sio Serikali

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
7,899
Reaction score
10,415
Mbunge ni kiongozi anayechaguliwa na wananchi ili akawawakilishe Serikalini badala yao.

Moja ya haki yake kuu ni kuwatetea wananchi na sio Serikali.

Hivyo basi mbunge anapogeuka na kuanza kuitetea Serikali huku wananchi wake anawasaliti hapo anakuwa amevunja haki zake na kuusahau wajibu wake.
 
Unataka kusema 'wajibu wa mbunge' nadhani.

Hawa wabunge wa kuteuliwa na serikali wanawajibika kwa serikali. Tunayataka wenyewe! Na bado.
 
Kwa huku kwetu ni ngumu, huku chama/serikali ina nguvu ya kuamua nani sasa awe Mbunge wa sehemu fulani, na Wananchi kwenye boksi ni kama kusherehesha tu...hivyo akizifikiria milioni kumi na kitu, jumlisha na posho atabaki na chama/serikali...cha kujifia.
 
Hatuna wabunge ila tuna kikundi cha wahuni na matapeli wanaolipwa mishahara na posho kwa Kodi za wananchi. Mfumo wa uchaguzi wa Tanzania hautoi nafasi kwa sanduku la kura kuamua maana yake asilimia kubwa la wabunge waliopo sio chaguo la wananchi,kwasababu ya udhaifu wa tume ya uchaguzi, uelewa mdogo wa elimu ya uraia miongoni kwa wananchi,rushwa,udhaifu wa baadhi ya vyama vya siasa pamoja na serikali kuingilia
 
Kwa kifupi tu: tunahitaji Katiba Mpya!
 
Back
Top Bottom