Haki na Demokrasia havitakuja Tanzania kwa Rais kuwapa vyeo Serikalini Viongozi wa Upinzani

Ushauri wako ni mzuri sana..lakini pia tusiyapinge sana mawazo ya mama...sababu yeye yupo uwanjani sisi ni watazamaji ...yamkini tungekua uwanjani tungemwelewa zaidi.... Kikubwa ni kuwaombea washauri wake waweze kumshauri vizuri...na yeye kukubali kushaurika....pia tusibanwe sana na historia katika utatuzi wa matatizo....yamkini njia zilizotumika Jana kutatua tatizo zilikuwa sahihi kwa Jana na siyo kwa tatizo la Leo... Tumpe ushauri ili tutapate kuyasemea matokeo .
 
Kwanza kuna upinzani au wapiga keleke tu waliyokosa fursa, wapinzani wanaounga mkono juhudi ndio hao uwape vyeo unategemea nini tena hapo?

Kwa masilahi ya wanasiasa hii ni habari njema kabisa na kwa vile wananchi wanapigania masilahi ya wanasiasa kuliko masilahi yao hivyo hili ni jambo jepesi kabisa, hivi nani atapinga atakapoona Mbowe na Lissu wamekula shavu?
 
Mpinzani atatekeleza sera za CCM au za upinzani?
Hii ndiyo hoja ya msingi mpinzani kuteuliwa kwenye serikali ya ccm maana yake haamini katika itikadi na sera za chama chake.

Kifupi ni wapinzani wasaka vyeo tu ndiyo wanaweza kuungana na ccm kwenye serikali yao.
 
Acha dharau watu aina yako ndio msiolitakia mema taifa.
 
Hii ndiyo hoja ya msingi mpinzani kuteuliwa kwenye serikali ya ccm maana yake haamini katika itikadi na sera za chama chake.

Kifupi ni wapinzani wasaka vyeo tu ndiyo wanaweza kuungana na ccm kwenye serikali yao.
Akitekeleza sera za CCM amekisaliti chama chake.

Akitekeleza sera za upinzani ameisaliti mamlaka yake ya uchaguzi.

Wazo zima limejaa contradiction.

Hiki kitu kinawezekana kwenye public service huko ambako siasa zinachukua backseat to public service. Na huko wala hakuna mjadala kuhusu hili anyway, rais alitakiwa kuchagua watu wa vyama vyote bila kujali vyama. Bila hata kuzungumzia vyama, kwa sababu kuzungumzia vyama kwenye public service ni kuchanganya siasa na public service.

Kwa hivyo rais kwa tamko hili pia anaweza kuwa anachanganya siasa na public service.

Uanachama wa CCM si qualification ya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege.

Kwenye vyeo vya siasa ni kizungumkuti.
 
Na nia ya rais ni kutaka kuzima vuguvugu la upinzani la kutaka mabadiliko makubwa ya mfumo wa utawala na kisera nchini.
 
Naona kama umeshindwa kutofautisha kati ya mahitaji wanasiasa na mahitaji ya wananchi.

Tegemea kuwa dissappointed.
 
Acha dharau watu aina yako ndio msiolitakia mema taifa.
Kama kusema kuwa tuna wapinzani wenye kuunga mkono juhudi ni dharau basi ni wao wenyewe ndio wanajidharirisha hivyo nina haki ya kuwadharau, kuna wapinzani wangapi wameunga juhudi na huwasikii tena kukosoa sasa na hawa wengine ukiwapa vyeo unategemea nini tena hapo?

Tukubali tu hatuna upinzani.
 
Bandiko zuri kabisa si lazima wapinzani wapate nyadhifa ndo tusonge mbele,maana mpinzani akiwa sehemu ya serikali ladha ya upinzani inakosekana.Chaguzi zifanyike kwa haki ili tuwe na upinzani Malini kwa maendeleo ya nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…