Haki, sii vitisho: Maendeleo ya Taifa yayajengwi kwa kutishiana

Haki, sii vitisho: Maendeleo ya Taifa yayajengwi kwa kutishiana

Prof_Adventure_guide

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2023
Posts
533
Reaction score
1,499
Ni dhahiri kuwa taifa letu linapitia kipindi kigumu, ambapo hali ya kisiasa inaendelea kuwa tete na raia wanahitaji kupewa haki zao, si vitisho au hofu. Rais wa Mchogo anaposhindwa kuelewa kwamba wananchi wanadai haki ya msingi ya kuishi kwa amani, maendeleo, na usawa, anaendelea kuathiri zaidi ustawi wa taifa letu. Hakuna kinachozidi kuwaumiza wananchi kuliko kuona viongozi wanapojaribu kuwaongoza kwa kutumia nguvu na vitisho, badala ya kuwaongoza kwa busara, hekima, na maelewano.

Kama taifa, tunahitaji kiongozi anayeweza kusikiliza kilio cha watu wake na kutenda kwa manufaa yao, si mtu anayejikita katika kudumisha hofu kwa wananchi wake. Kila siku, kauli na vitendo vya rais huyu vimekuwa kinyume na maslahi ya taifa letu. Hii sio tu inadhihirisha udhaifu katika uongozi wake, bali pia inadhihirisha kuwa yeye mwenyewe hajui jinsi ya kuongoza taifa lenye utu na heshima.

Tunaendelea kuona makosa makubwa yanayofanywa na rais huyu, makosa ambayo hayawezi kukubalika katika uongozi wa kisasa. Kiongozi ambaye kila anapozungumza, anajidhihirisha zaidi kuwa mwenye mtindo wa uongozi wa kimabavu na kupuuza maoni ya wananchi, si kiongozi wa kipekee bali ni mtu anayekatisha tamaa.

Vijana wa taifa hili, ambao ni injini kuu ya maendeleo yetu, wanajua kuwa taifa letu linahitaji mabadiliko ya kweli. Hii ni kwa sababu vijana hawawezi kumtukuza kiongozi ambaye hana maono ya kimaendeleo, ambaye badala ya kujenga taifa, anajikita katika kutishia raia na kutafuta njia za kuendelea kubaki madarakani kwa njia zisizo halali.

Uongozi wa kweli haujengwi kwa vitisho, bali kwa kuzingatia haki, uwazi, na dhamira ya dhati. Kiongozi anayetaka kujenga taifa imara lazima aonyeshe ujasiri wa kukubali changamoto, kuzingatia maoni ya wananchi, na kuwa mfano wa uongozi wa kiungwana. Huu siyo wakati wa kutishiana; huu ni wakati wa kujenga taifa linalozingatia haki, usawa, na maendeleo endelevu.

Muda wa kuogopa uongozi wa Rais Mchogo umeisha. Wananchi wamejua kuwa haki yao haiko mikononi mwa mtu mmoja. Wananchi hawaogopi tena, na wataendelea kupigania haki zao. Hii ni haki ya kila mmoja wetu. Sisi sote tunahitaji kiongozi ambaye ataonyesha uongozi wa kipekee, na ambaye atakuwa mfano wa ufanisi na ustawi wa taifa letu. Rais Mchogo ameonyesha, kwa maneno na vitendo, kuwa yeye sio kiongozi wa taifa hili. Tumeshuhudia dhihirisho la ujinga wake, na taifa halihitaji kiongozi wa aina hiyo.

Hivyo basi, kama tunataka mabadiliko ya kweli, tuchukue hatua sasa. Hii ni wakati wa kuwa na viongozi watakaosikiliza sauti za wananchi, watakaotoa nafasi kwa maendeleo na si vitisho. Vinginevyo, taifa letu litaendelea kujikuta katika mzunguko wa makosa, kwa kuwa hatukuwa na ujasiri wa kuchagua viongozi wa kweli.
 
anauliza vijana waseme wanadai haki ni haki gani,hivi hajui kuishi ni haki ya msingi ya kikatiba tangu kuanza kutekwa na kupotezwa vijana kwa wazee mpaka watoto amechukuwa hatua gani japo kila akisimama kwenye majukwaa anawakumbusha watu kuwa yeye ni amiri jeshi mkuu tuna kibarua kigumu kama nchi
 
Back
Top Bottom