Haki ya Faragha: Waliodukua Mawasiliano ya Kinana na Makamba washitakiwe

Haki ya Faragha: Waliodukua Mawasiliano ya Kinana na Makamba washitakiwe

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
16,419
Reaction score
26,594
Miaka kadhaa iliyopita mawasiliani binafsi kati ya Comrade Kinana na Makamba yalidukuliwa.

Hiki kilikuwa si kitendo cha kistaarabu na heshima.
Sina uhakika lakini kumfuatilia mtu nyendo zake inahitaji kibali cha mahakama.

Hawa wazee wetu Kinana na Makamba walikuwa watumishi wa ngazi za juu sana katika chama, na waliwahi kuwa Makatibu Wakuu wa CCM.

Hivyo hata kibinadamu wanaweza kutia neno kibinafsi wakiona jambo haliendi sawa, ili wakashauri mbele ya safari.

Vijana, inawezekana ikawa wa TCRA, wakawadukua mawasiliani yao na kumpelekea Rais Magufuli.

Hao vijana na uongozi wao watafutwe na kushitakiwa.
 
Kwani walikuwa wanaongea nn cha maana zaidi ya kejeri na kukashifu tu? Kuna wakati najiuliza hivi zile sauti zilizorekodiwa wale watu walikuwa wanalalamika kwa maslahi ya Taifa au wakulalamikia maslahi yao binafsi kubinywa? Na ndiyo maana mpq leo nashangaa NAPE na January wana nini haswa cha kuwekwa kwenye Uwaziri!
 
Hiki kilikuwa si kitendi cha kistaarabu na heshima. Sina uhakika lakini kumfuatilia mtu nyendo zake inahitaji kibali cha mahakama.
Kinadharia, ndiyo. Lakini kiuhalisia siyo. Duniani kote kuna watu ajira zao ni kufuatilia nyendo zenu.

Hali ni mbaya zaidi kwa hawa wanaojifanya vinara wa haki za binadamu duniani.
 
Watashitakiwa vipi wakati walalamikaji au watendwaji wenyewe wapo kimya.
Hili ni swala kubwa kuliko unavyofikiri.
Kwanza ni ukiukwaji wa katiba, kulinda usiri wa mtu katika jamii.
Ni swala la haki za kibinafsi na ukiukwaji wake.
Kisiasa Makamba na Kinana inawawia vigumu kushitaki kwani wanaweza tibua mengi ndani ya chama.
Lakini vyama vya haki za binadamu vinaweza kuendesha hii kesi ili kuliwekea msimamo katika misingi ya ukiukwaji wa haki.
 
Mkuu hiyo haki ya usiri ( utunzwaji wa faragha ya mtu mtandaoni) ipo tokea zaman na haijaanza leo wala jana.

lakini utendaji wake wa kazi haipo ndo maana juzi tigo walitoa taarifa za mteja wao kwenda mahakamani wakati hilo ni kosa.

ukipata mda ebu nenda you tube kasearch interview ya Maxence Melo na EATV utajifunza kitu.
 
Back
Top Bottom