Haki ya Faragha: Waliodukua Mawasiliano ya Kinana na Makamba washitakiwe

Tatizo si kujifunza, bali ni enforcement ya haki hizo ili kama mtoa mada anavyoeleza, watu washitakiwe.
 
Tatizo si kujifunza, bali ni enforcement ya haki hizo ili kama mtoa mada anavyoeleza, watu washitakiwe.
utashitaki vipi wakati hakuna utendewaji kazi wa sheria hiyo haunoni kama unapoteza mda na pesa .

yani inakuwa sawa na kuandaa nyanya, ndimu, mchele na vikolokolo kibao wakati mpishi hayupo.
 
Hao wahaini waliokua wanapanga kumfanyizia Rais wetu dawa yako iko inachemkia jikoni, Tanzania nzima iliwasikia. Watalipia tu, sio akhera hapahapa duniani.
 
Hata kama qalikuwa qanaongea upuuzi, haki yao ya faragha ipo pale pale. Waliokiuka haki ya faragha ya Kinana na Makamba wachukuliwe hatua za kisheria.
 
Tujue siku hizi mzalendo namba moja bwana Msiba yuko wapi
 
vyama vya kutetea haki za binaadamu vitashindwa japo nia ni nzuri kama ile ya saed kubenea vs bashite .
 
Mwendazake ,kafa na siri nyingi kutoka KWa viongozi aliowadukua, ukikubali kuwa KWENYE teuzi, au mtu muhim katika Taifa LAZIMA udukuliwe hakuna namna, Kinana ni MOJA viongozi Muhim katika Taifa hili Bila kujali ni Mwanaccm, napendekeza SSH katika kipindi Chake amebakiza kuendea na kamchezo ka mtangulizi wake , awe anawadukua 😂🤣 hakuna MCHEZO apa
 
Wale walikuwa wanamuomgelea jiwe ili kulikomboa taifa dhidi ya unyama wake. Maana yake ni wazalendo haswa na wallishangaa ni namn gani walimpitisha jiwe kuwa rais wakati hata ukuu wa wilaya alikuwa hafai
 
hahaha, na vile vigazeti vyake sivioni kabisa kwenye meza za magazeti
Alijitoa ufahamu yule wakati alikuja mzizzima kufanya kazi
Ufadhili mrija umekauka au umekatika au umeziba
 
Katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, 1977, imeelezwa wazi.

SEHEMU YA TATU
HAKI NA WAJIBU MUHIMU

Haki ya Usawa
(
Haki ya faragha
na usalama wa
mtu
Sheria ya 1984
Na.15 ib.6)
16.-(1) Kila mtu anastahili kuheshimiwa na kupata hifadhi
kwa nafsi yake, maisha yake binafsi na familia yake na
unyumba wake, na pia heshima na hifadhi ya maskani yake na

mawasiliano yake ya binafsi.

Hivyo basi tunaona wazi kuwa kuna watu wenye nia ovu, wanatumia mianya ya wao kuwa serikalini na kutekeleza mambo ya ovyo.
Ili kukabiliana na hili, sharti washitakiwe.
 
hahaha kuna sehemu nilikuwa namwona mara kwa mara alikuwa kama mwana TISS flan hivi.. sijui nani kawambia ukinyoa kipara na ndevu na visuti tu uankuwa na mamlaka.
Walimdanganya mengi
 
Kwa hiyo katika hii case ashitakiwe mshitakiwa no mbili na tatu, maana mshitakiwa no moja alisha tangulia mbele za haki!!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…