JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Andiko la Wakili Bashir Yakub kuhusu haki ya mzazi kumuona mtoto baada ya kutengana na mwenza au kuachana kabisa.
Sheria Namba 21 ya Mwaka 2009 Kifungu cha 38 cha Sheria ya Mtoto kinatoa haki hiyo na mzazi au mlezi anayekaa na mtoto hapaswi kuipinga, muhimu kusiwe na lengo la kumdhuru au kitu chochote kibaya wakati wa kumuona.
Anayenyimwa haki hiyo anaweza kufungua malalamiko Mahakama ya Mwanzo au ya Wilaya iliyopo ndani ya eneo analoishi mtoto (Awe na chini ya miaka 18).
Sababu za kumtima mzazi haki hiyo kwa madai hatoi matunzo au alimtelekeza Mtoto hazina mashiko kisheria, kwani mzazi au mlezi naye ana haki ya kufikisha malalamiko yake Mahakamani kuhusu madai yake hayo lakini si kumnyima mzazi mwenzake haki ya kumuona mtoto.