Mr George Francis
JF-Expert Member
- Jun 27, 2022
- 234
- 376
HAKI YA MTOTO PINDI WAZAZI WANAPOTENGANA.
Mtoto ana haki ya kupewa matunzo mazuri pindi wazazi wanapotengana, sawa na matunzo aliyoyapata pindi wazazi walipokuwa wakiishi pamoja.
Mtoto atakuwa na haki ya kupata elimu yenye ubora uleule aliokuwa anaupata kabla wazazi wake hawajatengana au kutalikiana.
Mtoto ana haki a kuishi na mzazi ambaye kwa maoni ya Mahakama atakuwa na uwezo wa kumlea mtoto kwa kuzingatia maslahi ya mtoto.
Mtoto ana haki ya kutembelea na kukaa kwa mzazi mwingine wakati wowote atakapotaka isipokuwa kama mpango huo hautaingiliana na programu za masomo au mafunzo.
Kutakuwa na dhana isiyopingika kwamba, kwa maslahi mapana ya mtoto aliye na umri chini ya miaka saba kuishi na mama yake isipokuwa kwa kuepuka kuleta usumbufu kwa mtoto Mahaakama inaweza kuamua mtoto huyo kuishi na baba yake au mtu mwingine kwa masrahi ya mtoto husika.
Endapo kutakuwa na watoto wawili au zaidi, Mahakama hailazimishwi kuamua watoto hao wote walelewe na mzazi mmoja lakini itaangalia masrahi mapana ya kila mtoto.
Hivyo, kutengana kwa wazazi hakutakiwi kuathili masrahi na ukuaji wa mtoto. Mtoto ni lazima aendelee kufurahia maisha yake kama kawaida.
Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 26 cha Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2019 pamoja na kifungu cha 125 cha Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2019.
Kwa ujumla Sheria ya Mtoto na Sheria ya ndoa zote zinaelekeza wazazi kuendelea na malezi ya uhakika kwa mtoto/watoto wao hata kama wametengana au kuachana.
HIVYO, wazazi wenye tabia ya kuacha kutoa huduma ya malezi kwa watoto wenu kwa kigezo kwamba umeachana na mzazi mwenza sheria inakulazimu uendelee kutoa malezi bora kwa mtoto/watoto wako. Kuachana kwenu kusiwe sababu ya watoto kuteseka.
Kwa elimu zaidi kuhusu malezi ya mtoto/watoto, karibu tuendelee kujifunza katika mada zinazofuata.
It's me
Mr George Francis
A Lawyer and LifeCoach
Contacts: 0713736006
Email: mr.georgefrancis21@gmail.com