Haki ya mtoto pindi wazazi wanapotengana au kuachana

Mr George Francis

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2022
Posts
234
Reaction score
376
HAKI YA MTOTO PINDI WAZAZI WANAPOTENGANA.

Mtoto ana haki ya kupewa matunzo mazuri pindi wazazi wanapotengana, sawa na matunzo aliyoyapata pindi wazazi walipokuwa wakiishi pamoja.

Mtoto atakuwa na haki ya kupata elimu yenye ubora uleule aliokuwa anaupata kabla wazazi wake hawajatengana au kutalikiana.

Mtoto ana haki a kuishi na mzazi ambaye kwa maoni ya Mahakama atakuwa na uwezo wa kumlea mtoto kwa kuzingatia maslahi ya mtoto.

Mtoto ana haki ya kutembelea na kukaa kwa mzazi mwingine wakati wowote atakapotaka isipokuwa kama mpango huo hautaingiliana na programu za masomo au mafunzo.

Kutakuwa na dhana isiyopingika kwamba, kwa maslahi mapana ya mtoto aliye na umri chini ya miaka saba kuishi na mama yake isipokuwa kwa kuepuka kuleta usumbufu kwa mtoto Mahaakama inaweza kuamua mtoto huyo kuishi na baba yake au mtu mwingine kwa masrahi ya mtoto husika.

Endapo kutakuwa na watoto wawili au zaidi, Mahakama hailazimishwi kuamua watoto hao wote walelewe na mzazi mmoja lakini itaangalia masrahi mapana ya kila mtoto.

Hivyo, kutengana kwa wazazi hakutakiwi kuathili masrahi na ukuaji wa mtoto. Mtoto ni lazima aendelee kufurahia maisha yake kama kawaida.

Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 26 cha Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2019 pamoja na kifungu cha 125 cha Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2019.

Kwa ujumla Sheria ya Mtoto na Sheria ya ndoa zote zinaelekeza wazazi kuendelea na malezi ya uhakika kwa mtoto/watoto wao hata kama wametengana au kuachana.

HIVYO, wazazi wenye tabia ya kuacha kutoa huduma ya malezi kwa watoto wenu kwa kigezo kwamba umeachana na mzazi mwenza sheria inakulazimu uendelee kutoa malezi bora kwa mtoto/watoto wako. Kuachana kwenu kusiwe sababu ya watoto kuteseka.

Kwa elimu zaidi kuhusu malezi ya mtoto/watoto, karibu tuendelee kujifunza katika mada zinazofuata.

It's me
Mr George Francis
A Lawyer and LifeCoach
Contacts: 0713736006
Email: mr.georgefrancis21@gmail.com
 

Ni kiasi gani cha pesa kwa mujibu wa sheria kinatakiwa kutolewa na Baba kama child support?
 

Ni kiasi gani cha pesa kwa mujibu wa sheria kinatakiwa kutolewa na Baba kama child support?
Mahakama itaamuru kiasi cha fedha kulingana na hali ya kipato cha mzazi husika. Hii hasa katika maintenance of the child. Mada ijayo kuhusu maintenance of the child nitakuja kuelezea zaidi.
 
Ila kuna wakati tunatofautiana falsafa katika malezi… mmoja yuko ku western zaidi na mwingine ki hard core flani hivi… ni nani kati ya Baba au Mama mwenye haki zaidi ya kuamua mustakabali wa mtoto yaani kwa mfano ni shule gani aende ( jaalia wote wanajiweza kifedha)
 
Inategemea kikubwa ni mtoto kupata elimu bora
 
Mahakama itaamuru kiasi cha fedha kulingana na hali ya kipato cha mzazi husika. Hii hasa katika maintenance of the child. Mada ijayo kuhusu maintenance of the child nitakuja kuelezea zaidi.
mkuu kama mzazi anapokea milion mbili atatoa shingap kwa watoto wawili?
 

 
Mimi nimeachana na mke wangu na aliondoka na watoto wawili, kila nilivyo jaribu kutoa huduma kwa watoto wangu mama yao anakataa nisitoe chochote na wameungana na mama yake mzazi ( mama mkwe). Mara ya mwisho nilienda kuwasalimia watoto wangu mama mkwe alifikia hatua ya kunizuia kwenda kuwaona wanangu, nikamuomba baba mkwe niondoke na wanangu mzee alikubali ila shida ikaja kwa mama mkwe alikataa katakata.

Naumia kuwa mbali na wanangu najaribu kila njia imekuwa ni ngumu sana kuwachukua wanangu sjui la kufanya naomba msaada
 
Doh pole sana mwamba, wakatie life insurance, tia mzigo I think kiwango cha chini ni 64,000/= kwa mwezi hii ni package ya Jubilee Insurance, hii itawasidia maisha yao ya baadae pia kama unauwezo wakatie health insurance na uwafungulie bank account ambayo ni 5,000/= Tshs kwa Nmb. Kamwe usiiingie kwenye mtego wa kugombania watoto, wacha muda utaongea, wanawake walio wengi hasa hawa single mama upeo wao ni mdogo sana.
 
Life insurance mtoto ataweza kuichukua baada ya kufikisha umri gani?
 
Ahsante sana Kwa ushari wako
 
Life insurance mtoto ataweza kuichukua baada ya kufikisha umri gani?
18 YEARS, hii ndio gap wahindi na baadhi ya familia zinazojielewa wanatupiga, 64,000/= ni kama 768,000/= kwa mwaka , kwa ten years ni kama 7,680,000/= , ambapo kwa calculations zao atapata kama 25,000,000/= kama sikosei,
 
Wakili Msomi usituangushe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…