Haki yangu kikatiba ya kushawishi/hamasisha wamuongezee muda Rais Magufuli

Status
Not open for further replies.

JERUSALEM 2006

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2012
Posts
527
Reaction score
596

1. Katiba ya Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na marekebisho yake ya 30th April 2000 yananipa haki zote kama raia halali wa Taifa la Tanzania kuwa na mawazo huru juu ya jambo lolote ambalo halivunji sheria za nchi yetu.

Mimi kama Mtanzania tarehe 16 Februari 2020 nilianzisha uzi unaosema "KARIBU TUJIUNGE NA KUNDI LA MAGUFULI TENA 2025" na mjadala katika kundi hili ulikuwa unaendelea. Kwa bahata mbaya sana.

2. Katiba ya jamhuri ya Tanzania ( 1977) kuanzia ibara ya18 (UHURU WA MAONI) , ibara ya19 ( UHURU WA MTU KUSHIRIKIANA NA MTU MWINGINE) kwa pamoja zinasema

Ibara 18.1 Bila kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake,na kutafuta,kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru mawasilano yake kutoingiliwa kati.

Naomba nielezee ibara hii ya 18.1; ni kwamba nina uhuru wa kutoa mawazo yangu yoyote, katika chombo chochote ikiwemo Jamii Forums, bila kuingiliwa na yeyote.

Ibara 20.1 Kila mtu anastahili kuwa Huru, bila ya kuathiri Sheria za Nchi, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanyika, na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au mashirika yaliyo anzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.

Nia yangu ni thabiti, ni kuanzisha mchakato wa kubadirisha Katiba kwa kukusanya signatures zaidi ya million tano za wa Tanzania ili kuweza kukidhi matakwa ya kikatiba ya kumuongezea angalau muhala mwengine Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli,

KAULI MBIO YETU NI.

"H.E President Magufuli is too valuable to retire, Tanzanians needs him now more than ever" " Mhe, Rais Magufuli ni wathamani sana kustaafu, Watanzania wanamuhitaji sasa kuliko kipindi kingine chochote"

MWISHO

Kama nilivyo quote vipengele vya katiba, basi naomba mawazo yangu yaheshimiwe. Situkana, sijapanga kuua, wala sija panga kuvunja sheria za Nchi, ninafuata taratibu zote ili kubarisha vipengere vya Katiba ambayo siyo Msaafu wala siyo Bibilia.
 
Upvote 3
Nashawishi ili tubadirishe katiba ya sasa inayomnyima haki ya kuendelea na nngwe ya tatu Mhe. Rais.

So sivunji katiba, ila nashawishi ili tubadili katiba
Unadhani wana demokrasia kwanini waliweka ukomo wa uongozi na kuweka kipindi cha hio miaka ?, ni kwamba kulikuwa hakuna watu wanaofaa kama huyu wako wa sasa ? umepitia pro and cons au ?

Haya tuseme huyu ni malaika na anafaa akija asiyefaa na yeye tutabadilisha Katiba ili apunguziwe muda au itabidi twende naye tu, to infinity?
 
Kweli kabisa mkuu! Hawa jamaa sijui wana lengo gani.
 

Hizo tafiti umefanya lini?

Mimi nataka kuwahamasisha watanzania zaidi ya 5M ili waunge harakati hizi.

Katiba sio Msaafu
 

Hiyo misingi ya sheria pigania wewe.

Miki napigania kubadilishwa kwa katiba ili rais aliyeko madaraki aendelee kuongoza angalau kwa muhula mmoja zaidi.

Kwani shida iko wapi? Mengine fanya wewe
 

Baba wa Taifa Mwl. Nyerere alikuwa analazishwa kila wakati aongeze muda mpaka alipoamua kuondoka kwa lazima.

Na sisi tuna haki zote za kumlazimisha kiongozi tunayona anafaa.

Kiongozi mzuri ni yule anayetafutwa na watu sio anayetafuta mwenyewe uongozi.

H.E Mr President amekidhi vigezo hapo juu
 
Haki hizo ulizonazo ni kinyume na wale wanaompinga, wao wanapotezwa na kufitiniwa. Mwamakula kaomba tu katiba mpya na tume huru. Tayari Yuko mikononi mwa police.

Haki za upande moja za nini ?! .

Ukitaka kujua ukweli weka kura za maoni humu. Utajua mh anakubalika kiasi gani [emoji120]
 

Mimi sijaongelea vyama hapa.

Wewe kama ni CCM baki na chama chako. Mimi ni Mtanzania mwenye haki zote za kumshawishi mwananchi yeyote tubadilishe katiba ili Mhe. Rais azidi kutuhudumia
 
Haijawahi kutokea , wala haitakuja kutokea , kwa watawala walio mfuatisha Mwl. Kupendwa na kulazimishwa kubaki madarakani hata siku moja. Ukweli unajulikana na wewe unajua pia .

Haki kila mtu anayo hakuna asiye na haki, sote tuna haki ya kukubali au kupinga jambo fulani .

Unayo yaendeleza ni mawazo yako binafsi, hata mwenyekiti wako hayataki. Kwa ushahidi polepole alioleta bungeni siku sio nyingi.

[emoji117]Unataka kutuambia wewe na polepole nani anajua zaidi maswala ya ndani ya chama?


[emoji117]Unataka kusema wewe na mwenyekiti wa chama nani anamaamuzi juu ya kuongoza taifa na undani wake?


[emoji117]Unataka kutuambia kuwa alichokisema mwenyekiti kuwa hata ongeza muda wa madaraka sio sahihi?

[emoji117]Mwl. Alipoulizwa aendelee kuongoza alijibu nini?

Ukishajibu hayo maswali njoo tuendelee na mada .................
 
Unakaribishwa pia,
Jambo la msingi sheria za nchi ziheshimiwe bila kuathiri uhuru wa wengine

anaevunja sheria za nchi na kuwa na double standard ndio huyo huyo aliepo madarakani, kwanini tusianze kukemea hayo kabla ya kumwongezea muda ? kweli wewe huvunjinsheria ila yeye magufuli anavyokanyaga sheria anavyotaka yeye je ni sawa ??
 
Seriously hayo ni mawazo yako huru na ninayaheshimu.

Please respect my opinion too.

Haya ya jamaa sio mawazo ni facts. ya kwako wewe ndio mawazo, sisi tunaweza kabisa tukafact chek alichosema jamaa au nasema uongo ndugu zangu
 
Sema nyinyi wachache hamtaki, kwa taarifa yako ndio kwanza hii kampeni inaanza.

Sasa kaa kwa kutulia uone moves
 
Yani haki ya kubadilisha katiba kumuongezea muda unayo ila ya kuomba katiba mpya ya Rasimu ya warioba huna. Hapo ndyo uyajua hii nchi ina wenye nao wengine ni kama wafungwa kama sio watumwa.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…