Haki yangu kikatiba ya kushawishi/hamasisha wamuongezee muda Rais Magufuli

Haki yangu kikatiba ya kushawishi/hamasisha wamuongezee muda Rais Magufuli

Status
Not open for further replies.

JERUSALEM 2006

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2012
Posts
527
Reaction score
596
5G3TVR.png

1. Katiba ya Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na marekebisho yake ya 30th April 2000 yananipa haki zote kama raia halali wa Taifa la Tanzania kuwa na mawazo huru juu ya jambo lolote ambalo halivunji sheria za nchi yetu.

Mimi kama Mtanzania tarehe 16 Februari 2020 nilianzisha uzi unaosema "KARIBU TUJIUNGE NA KUNDI LA MAGUFULI TENA 2025" na mjadala katika kundi hili ulikuwa unaendelea. Kwa bahata mbaya sana.

2. Katiba ya jamhuri ya Tanzania ( 1977) kuanzia ibara ya18 (UHURU WA MAONI) , ibara ya19 ( UHURU WA MTU KUSHIRIKIANA NA MTU MWINGINE) kwa pamoja zinasema

Ibara 18.1 Bila kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake,na kutafuta,kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru mawasilano yake kutoingiliwa kati.

Naomba nielezee ibara hii ya 18.1; ni kwamba nina uhuru wa kutoa mawazo yangu yoyote, katika chombo chochote ikiwemo Jamii Forums, bila kuingiliwa na yeyote.

Ibara 20.1 Kila mtu anastahili kuwa Huru, bila ya kuathiri Sheria za Nchi, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanyika, na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au mashirika yaliyo anzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.

Nia yangu ni thabiti, ni kuanzisha mchakato wa kubadirisha Katiba kwa kukusanya signatures zaidi ya million tano za wa Tanzania ili kuweza kukidhi matakwa ya kikatiba ya kumuongezea angalau muhala mwengine Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli,

KAULI MBIO YETU NI.

"H.E President Magufuli is too valuable to retire, Tanzanians needs him now more than ever" " Mhe, Rais Magufuli ni wathamani sana kustaafu, Watanzania wanamuhitaji sasa kuliko kipindi kingine chochote"

MWISHO

Kama nilivyo quote vipengele vya katiba, basi naomba mawazo yangu yaheshimiwe. Situkana, sijapanga kuua, wala sija panga kuvunja sheria za Nchi, ninafuata taratibu zote ili kubarisha vipengere vya Katiba ambayo siyo Msaafu wala siyo Bibilia.
 
Upvote 3
Askofu kahamasisha maandamano.
Mimi, nimeunda TELEGRAM group kwa ajili ya kufuata taratibu zote za kisheria katika kufanya amendment za Katiba.

Kosa langu liko wapi?
Kwani kifungu gani Cha katiba amevunja kwa kuhamasisha maandamano?
 
Askofu kahamasisha maandamano.
Mimi, nimeunda TELEGRAM group kwa ajili ya kufuata taratibu zote za kisheria katika kufanya amendment za Katiba.

Kosa langu liko wapi?
Wewe umeunda group kwa kibali cha nani?

Je group lako la telegram mnakibali chochote kutoka TCRA?

Je tukisema umeanzisha group kwaajili ya kuchafua amani ya taifa pamoja na wenzako mnaoshirikiana bila kibali tutakuwa tumekosea?
 
Halafu bila kuathiri maswali tangulizi, Je kibali cha kuunda group la telegram ilikukusanya maoni yako na watu wenye mtazamo kama wako mmekitoa wapi ? Kama unacho toa picha tuone ?

Je kati ya kibali cha kuunda ngroup na kuunda group lenyewe kipi kinatangulia kufanyika? Je ni kibali au unaanza kuunda group ndio upate kibali?
 
Una uthibitisho??
Au unalialia hapa kutafuta huruma baada ya kukosa ubunge?
Mimi kukosa ubunge? Ubunge gani? Huu huu wa kimagimashi uliopatikana 2020?Kifungu gani Cha katiba kinakataza watanzania kuandamano kuelezea hisia zao?
 
Halafu bila kuathiri maswali tangulizi, Je kibali cha kuunda group la telegram ilikukusanya maoni yako na watu wenye mtazamo kama wako mmekitoa wapi ? Kama unacho toa picha tuone ?

Je kati ya kibali cha kuunda ngroup na kuunda group lenyewe kipi kinatangulia kufanyika? Je ni kibali au unaanza kuunda group ndio upate kibali?

Sasa nadhani, umevurugwa.

Nime quote vipengele vya ibala za katiba vinavyonipa uhuru wa kufanya niliyofanya.

Sasa na wewe nipe vifungu vya sheria vinavyonizuia kuunda group kwa mlengo nilio utaja.

Kama kuna sheria ya aina hiyo, niko tayari kufuata sheria hiyo, ila kama hamna nakuomba utulie hivyo hivyo kwa kupoa ili dawa iingie vizuri
 
Mimi kukosa ubunge? Ubunge gani? Huu huu wa kimagimashi uliopatikana 2020?Kifungu gani Cha katiba kinakataza watanzania kuandamano kuelezea hisia zao?

Maandamano hayakatazwi ila fata utaratibu ikiwemo kutochochea ghasia pia bila kuathiri amani ya nchi.

Pia ni lazima upate kibali cha clearance ya police, hii ni kwa mujibu wa sheria zetu za usalama.
 
Sasa nadhani, umevurugwa.

Nime quote vipengele vya ibala za katiba vinavyonipa uhuru wa kufanya niliyofanya.

Sasa na wewe nipe vifungu vya sheria vinavyonizuia kuunda group kwa mlengo nilio utaja.

Kama kuna sheria ya aina hiyo, niko tayari kufuata sheria hiyo, ila kama hamna nakuomba utulie hivyo hivyo kwa kupoa ili dawa iingie vizuri
[emoji3][emoji3][emoji3] imebidi nicheke kwasababu wewe nadhani hufahamu huruhusiwi kuendesha tafiti yoyote wala kutoa takwimu yoyote currently bila wizara husika kukupa kibali hilo unalifahamu kwanza ?

Kama unalifahamu hilo vifungu ulivyo ainisha nisawa sijakataa hata kimoja . Swali Askof . Mwakalukwa amevunja sheria gani naye ambayo umeisema wewe?

Maana kama yeye kusema anataka katiba mpya na kusema atafanya matembezi ya amani unasema kavunja sheria Je wewe hujavunja sheria kwa kutaka kukusanya maoni uchwara ?
 
1. Katiba ya Jamuhuri wa muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na marekebisho yake ya 30th April 2000 yananipa haki zote kama raia halali wa taifa la Tanzania kuwa na mawazo huru juu ya jambo lolote ambalo halivunji sheria za nchi yetu.

Mimi kama Mtanzania tar.16/02/2020 nilianzisha uzi unaosema " KARIBU TUJIUNGE NA KUNDI LA MAGUFURI TENA 2025" na mjadala katika kundi hili ulikuwa unaendelea. Kwa bahata mbaya sana.

2. Katiba ya jamhuri ya Tanzania ( 1977) kuanzia ibara ya18(UHURU WA MAONI) , ibara ya19( UHURU WA MTU KUSHIRIKIANA NA MTU MWINGINE) kwa pamoja zinasema

Ibara 18.1 Bila kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake,na kutafuta,kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru mawasilano yake kutoingiliwa kati.

Naomba nielezee ibara hii ya 18.1; ni kwamba nina uhuru wa kutoa mawazo yangu yoyote, katika chombo chochote ikiwemo jamii forums, bila kuingiliwa na yeyote.

Ibara 20.1 Kila mtu anastahili kuwa Huru, bila ya kuathiri sheria za Nchi, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanyika, na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au mashirika yaliyo anzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.

Nia yangu ni thabiti, ni kuanzisha mchakato wa kubadirisha katiba kwa kukusanya signatures zaidi ya million tano za waTanzania ili kuweza kukidhi matakwa ya kikatiba ya kumuongezea angalau muhala mwengine Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli,

KAULI MBIO YETU NI.
"H.E President Magufuri is too valuable to retire, Tanzanians needs him now more than ever" " Mhe, Rais Magufuri ni wathamani sana kustaafu, Watanzania wanamuhitaji sasa kuliko kipindi kingine chochote"

MWISHO;
Kama nilivyo quote vipengele vya katiba, basi naomba mawazo yangu yaheshimiwe. situkana, sijapanga kuua, wala sija panga kuvunja sheria za nchi, ninafuata taratibu zote ili kubarisha vipengere vya katiba ambayo siyo Msaafu wala siyo Bibilia.
Kama unampenda sana magufuli akimaliza ubabe wake mchukue awe kiongozi wa familia yako.
 
[emoji3][emoji3][emoji3] imebidi nicheke kwasababu wewe nadhani hufahamu huruhusiwi kuendesha tafiti yoyote wala kutoa takwimu yoyote currently bila wizara husika kukupa kibali hilo unalifahamu kwanza ?

Kama unalifahamu hilo vifungu ulivyo ainisha nisawa sijakataa hata kimoja . Swali Askof . Mwakalukwa amevunja sheria gani naye ambayo umeisema wewe?

Maana kama yeye kusema anataka katiba mpya na kusema atafanya matembezi ya amani unasema kavunja sheria Je wewe hujavunja sheria kwa kutaka kukusanya maoni uchwara ?

Sasa mimi kuna utafiti ninao ufanya hapo???
Au kuna jambo lolote linalohusu takwimu ninalolifanya?

Kimsingi, nimeanza processes za kuomba amendment ya katiba, full stop.

Na hii ina hatua zake ikiwemo kukusanya signatures kutoka kwa walengwa.

Sasa huu ni utafiti? Au ni kukusanya facts.

Bado nasubiri vifungu vya sheria.

Kuh. Askofu, hakupewa kibali na Polisi kufanya/hamasisha maandamano kwani sheria inamtaka hivyo.
 
Maandamano hayakatazwi ila fata utaratibu ikiwemo kutochochea ghasia pia bila kuathiri amani ya nchi.

Pia ni lazima upate kibali cha clearance ya police, hii ni kwa mujibu wa sheria zetu za usalama.
Tatizo unaaminisha watu uwongo clearence lazima ipatikane ni kweli hatujakataa bali toka Askf atangaze ulishaona mtunametoka kuandamana hata mmoja?

Je kama askofu alikuwa anafuatilia vibali vya maandamano yake ya hiari ungejuaje ?

Pamoja na sheria za nchi kuwepo bali watawala inabidi watumie hekima na ustaarabu katika ku enforce hizo sheria .

Sheria bila hekima na utii ni bure katika nchi yoyote duniani, jifunzeni kwa hilo.
 
Sasa vibali vinatolewa na nani??? Si polisi??? Sasa kama Polisi wamemkamata maana yake ni nini? Hajaomba kibali.

Simple, fuata sheria za nchi bila shuruti.
 
Sasa vibali vinatolewa na nani??? Si polisi??? Sasa kama Polisi wamemkamata maana yake ni nini? Hajaomba kibali.

Simple, fuata sheria za nchi bila shuruti.
Wewe unauhakika gani kwamba hajaomba vibali? Unaifanya kazi ya polisi kuwa mikononi mwako ?

Kila anaye kamatwa na polisi kwa kuhamasisha maandamano huwa hajaomba kibali?
 
Sasa mimi kuna utafiti ninao ufanya hapo???
Au kuna jambo lolote linalohusu takwimu ninalolifanya?

Kimsingi, nimeanza processes za kuomba amendment ya katiba, full stop.

Na hii ina hatua zake ikiwemo kukusanya signatures kutoka kwa walengwa.

Sasa huu ni utafiti? Au ni kukusanya facts.

Bado nasubiri vifungu vya sheria.

Kuh. Askofu, hakupewa kibali na Polisi kufanya/hamasisha maandamano kwani sheria inamtaka hivyo.
Facts na utafiti tofauti yake nini?
 
Wewe unauhakika gani kwamba hajaomba vibali? Unaifanya kazi ya polisi kuwa mikononi mwako ?

Kila anaye kamatwa na polisi kwa kuhamasisha maandamano huwa hajaomba kibali?

Sasa unataka nikuamini wewe kwamba Askof kaonewa tu ila nisiwaamini polisi wenye hiyo dhamani?

who are you?

Taarifa rasmi ya Polisi imetoka jana, na inasema amevunja sheria, nenda kamsikilize Mambo Sasa.

Ila siwezi kukusikiliza wewe, huna dhamana hiyo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom