Haki yangu kikatiba ya kushawishi/hamasisha wamuongezee muda Rais Magufuli

Status
Not open for further replies.

JERUSALEM 2006

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2012
Posts
527
Reaction score
596
5G3TVR.png

1. Katiba ya Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na marekebisho yake ya 30th April 2000 yananipa haki zote kama raia halali wa Taifa la Tanzania kuwa na mawazo huru juu ya jambo lolote ambalo halivunji sheria za nchi yetu.

Mimi kama Mtanzania tarehe 16 Februari 2020 nilianzisha uzi unaosema "KARIBU TUJIUNGE NA KUNDI LA MAGUFULI TENA 2025" na mjadala katika kundi hili ulikuwa unaendelea. Kwa bahata mbaya sana.

2. Katiba ya jamhuri ya Tanzania ( 1977) kuanzia ibara ya18 (UHURU WA MAONI) , ibara ya19 ( UHURU WA MTU KUSHIRIKIANA NA MTU MWINGINE) kwa pamoja zinasema

Ibara 18.1 Bila kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake,na kutafuta,kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru mawasilano yake kutoingiliwa kati.

Naomba nielezee ibara hii ya 18.1; ni kwamba nina uhuru wa kutoa mawazo yangu yoyote, katika chombo chochote ikiwemo Jamii Forums, bila kuingiliwa na yeyote.

Ibara 20.1 Kila mtu anastahili kuwa Huru, bila ya kuathiri Sheria za Nchi, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanyika, na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au mashirika yaliyo anzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.

Nia yangu ni thabiti, ni kuanzisha mchakato wa kubadirisha Katiba kwa kukusanya signatures zaidi ya million tano za wa Tanzania ili kuweza kukidhi matakwa ya kikatiba ya kumuongezea angalau muhala mwengine Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli,

KAULI MBIO YETU NI.

"H.E President Magufuli is too valuable to retire, Tanzanians needs him now more than ever" " Mhe, Rais Magufuli ni wathamani sana kustaafu, Watanzania wanamuhitaji sasa kuliko kipindi kingine chochote"

MWISHO

Kama nilivyo quote vipengele vya katiba, basi naomba mawazo yangu yaheshimiwe. Situkana, sijapanga kuua, wala sija panga kuvunja sheria za Nchi, ninafuata taratibu zote ili kubarisha vipengere vya Katiba ambayo siyo Msaafu wala siyo Bibilia.
 
Upvote 3
Sasa unataka nikuamini wewe kwamba Askof kaonewa tu ila nisiwaamini polisi wenye hiyo dhamani?

who are you?

Taarifa rasmi ya Polisi imetoka jana, na inasema amevunja sheria, nenda kamsikilize Mambo Sasa.

Ila siwezi kukusikiliza wewe, huna dhamana hiyo.
Sitaki kuvunja sheria hapa , ila nadhani vyombo vyetu vya usalama vinatakiwa kujitathimini sana . Kwasababu lukuki ambazo hata wewe unazijua sana.

Mimi nawezakuwa sio kitu bali natoa maoni kulingana na mwenendo wa taifa unavyoelekea .
 
Halafu vifungu vya sheria unavyozungumzia ni vipi? Maana hapa hatujabishana sheria ambayo kimsingi nadhani itakutatiza pia .

Wewe si umesema nimevunja sheria kwa kuanzisha group la TELEGRAM, as if sheria zetu zinatuhitaji tujisajili kila tunapoanzisha groups za social medias,

Nipe hizo sheria nilizovunja
 
Jifunze kuwa mvumilivu pale unapotofautiana mawazo na wenzako.

Usitumie matusi, sio jambo zuri hata kidogo.

You can still convey your message without provacation languages.

So grow up.
Nachofurahia watu hawaogopi tena kuongea na kuambiana kuhusu Corona... wameanza kuacha kumungunya maneno na sasa wanasema... “ni Corona”....
Wamebaki wapuuzi wachache wanaojipendekeza kwa jiwe.
 
Facts are tangible solution in regarded situations, research is an ideal solution of a certain query.

So at-least naweza kukujibu hivi.
Ili upate tangible solutions in regarding of certain situation what will you do?

Maana naona unachanganya mambo hapo.
 
Sitaki kuvunja sheria hapa , ila nadhani vyombo vyetu vya usalama vinatakiwa kujitathimini sana . Kwasababu lukuki ambazo hata wewe unazijua sana.

Mimi nawezakuwa sio kitu bali natoa maoni kulingana na mwenendo wa taifa unavyoelekea .

Kujitathimini ni muhimu, wao ni binadamu so hiyo kawaida. Ila kwa sehemu kubwa wanafanya kazi zao kwa weredi mkubwa.
 
Wewe si umesema nimevunja sheria kwa kuanzisha group la TELEGRAM, as if sheria zetu zinatuhitaji tujisajili kila tunapoanzisha groups za social medias,

Nipe hizo sheria nilizovunja
Kwa Scenario yako group la telegram umeunda ili ufanye nini? Hapo ndio kwenye mzizi wa tatizo lako?

Ukishapata hizo facts unazo zitetea unazipeleka wapi ? Unakaanazo wewe binafsi au twatakiwa tuzijue nasi? Je tukizijua utatwambia zinaitwaje ?
 
Maandamano hayakatazwi ila fata utaratibu ikiwemo kutochochea ghasia pia bila kuathiri amani ya nchi.

Pia ni lazima upate kibali cha clearance ya police, hii ni kwa mujibu wa sheria zetu za usalama.
Kuna Sheria ipo juu ya katiba nchi hii? Je na wewe kuchochea watu ili wakubali kuongeza muda wa rais aliyepo madarakani si uchochezi? Je si uchochezi wewe kuamusha hasira za wale ambao hawataki Magu aongezewe muda? Au umepata kibari?
 
Nachofurahia watu hawaogopi tena kuongea na kuambiana kuhusu Corona... wameanza kuacha kumungunya maneno na sasa wanasema... “ni Corona”....
Wamebaki wapuuzi wachache wanaojipendekeza kwa jiwe.

Sasa CORONA imeingiaje hapa? Seriously?

Ok, tuhamie huko kwenye CORONA. Unataka Rais akufanyeje ili uridhike?

Je, unataka atangaze state of emergence ili tusiwe tunatoka ndani au tupigwe curfew ndo uone amefanya kitu? Waliofanya hivyo wamesaidikaje? Corona imeisha?? Hapana.

Je, unataka atangaze kwamba sasa tuna janga la Corona kwa hiyo kila mtu avae barakoa na kunawa mikono? Je, waliofanya hivyo wamesaidikaje? Corona imeisha ? Hapana.

Anachofanya Mhe. Rais ni kuondoa hofu miongoni mwetu watanzania.

Sio kila mtu anaweza kuhimili hofu hizi, acheni watu waishi na waendelee na maisha kama kawaida.
Mungu yupo atatulinda.

Mbona sijakusikia ukilalamika kuhusu Ukimwi, Malaralia, Kifua kikuu, Saratani etc. na hivi vyote vinaua kuliko Corona?

Tafiti zinaonesha Corona inaua less than 3% ya wanao ambukizwa, lakini magonjwa niliyokutajia hapo, yanaua kuanzia 30% ya maambukizi.

Relax uko kwenye mikono salama ya jemedari
 
Kuna Sheria ipo juu ya katiba nchi hii? Je na wewe kuchochea watu ili wakubali kuongeza muda wa rais aliyepo madarakani si uchochezi? Je si uchochezi wewe kuamusha hasira za wale ambao hawataki Magu aongezewe muda? Au umepata kibari?

Ukiona unapata hasira kwa mawazo mbadala ya mwenzako, sasa huo ndio ujinga wa kifikra.

Tunaita lack of political tolerance. Au political vandalism.
 
Kujitathimini ni muhimu, wao ni binadamu so hiyo kawaida. Ila kwa sehemu kubwa wanafanya kazi zao kwa weredi mkubwa.
Hilo ndio jibu maana kazi yetu ni moja kujenga tanzania nasi kuharibu tanzania .

Ushahidi wa wazi sakata la kutekwa kwa Tajiri mmoja hapa nchini Mh raisi alisema nanukuuu"""" POLISI MSIWAFANYE WATANZANIA NI WAJINGA "" unajua maana ya hii kauli ?

Explanatory ya mtu unae mtetea juu ya huo mkasa uliiona ni sahihi?

Sakata la akwilina ? Unalifahamu kwamba risasi inaweza kupigwa juu ikarudi na kumpiga mtu kichwani upande wa pembeni mwa kichwa , bado unasema weledi .

Rejea kauli ya Raisi watanzania sio wajinga .
 
Naelewa unatimiza haki yako kikatiba ila Rais alishasema hataongeza muda.

Naamini hatafanya hivyo.
 
Sasa CORONA imeingiaje hapa? Seriously?

Ok, tuhamie huko kwenye CORONA. Unataka Rais akufanyeje ili uridhike?

Je, unataka atangaze state of emergence ili tusiwe tunatoka ndani au tupigwe curfew ndo uone amefanya kitu? Waliofanya hivyo wamesaidikaje? Corona imeisha?? Hapana.

Je, unataka atangaze kwamba sasa tuna janga la Corona kwa hiyo kila mtu avae barakoa na kunawa mikono? Je, waliofanya hivyo wamesaidikaje? Corona imeisha ? Hapana.

Anachofanya Mhe. Rais ni kuondoa hofu miongoni mwetu watanzania.

Sio kila mtu anaweza kuhimili hofu hizi, acheni watu waishi na waendelee na maisha kama kawaida.
Mungu yupo atatulinda.

Mbona sijakusikia ukilalamika kuhusu Ukimwi, Malaralia, Kifua kikuu, Saratani etc. na hivi vyote vinaua kuliko Corona?

Tafiti zinaonesha Corona inaua less than 3% ya wanao ambukizwa, lakini magonjwa niliyokutajia hapo, yanaua kuanzia 30% ya maambukizi.

Relax uko kwenye mikono salama ya jemedari
Kuhusu swala hili, mimi pamoja na wenzangu wote wenye akili timamu na utashi najua Tanzania ugonjwa wa corona upo na unachukua uhai wa watu kila siku.

Tatizo labda wewe na familia yako mko salama but kwa upande wangu ndugu zangu wameshafariki kwa janga hili, ambalo mnalificha ficha.

Juzi timu ya Namungo Fc wameenda Angola unajua kilichotokea kule?

Wale wachezaji watatu waliokutwa na corona positive walikuwa wapi kama sio hapa nchini?

Janga hili sio aibu ni janga la dunia nzima .
 
Jemedari mfalme juha
 
Mleta mada nadhani walioweka kikomo cha miaka 10 walitafakari na kuona kabisa inamtosha kiongozi kufanya mambo yake kwa mujibu wa taratibu za kisheria na kukabidhi yale ambayo hatomaliza kwa mrithi wake.

Utaratibu wa kupokezana baada ya miaka kumi ni mzuri na umeshazoeleka kwakuwa ni sehemu ya checks and balance , hata ikitokea mbeleni huko tukapata rais ambaye pengine hatofanya vizuri tutakua tunajua kwa dhahiri kwamba tutakaa nae miaka kumi na kisha ataondoka madarakani... tukianza kubadilisha katiba tutakuwa tuna set kitu kinaitwa precedence.....huko mbeleni tutapata viongozi wengine ambao watatuambia nimefanya vizuri sana na hivyo hakuna haja hata ya kupiga kura kwa mfano na hatutakuwa na cha kumfanya maana anaweza kuwa ndani ya takwa la kisheria .......sidhani kama kuongeza muda wa rais itakuwa ni muarobaini wa matatizo yetu kwakuwa hata rais ni mtu wa kawaida tu loolote laweza kumfika....sasa kama utabadilisha katiba kwa ajili yake na ukute kesho yake hayupo unafanyaje ? unabadilisha tena au? Rais Magufuli ameonyesha njia na nadhani kupitia uongozi wake madhubuti nchini na ndani ya chama ataweza kutuletea kiongozi mzuri toka kwenye chama au kwingineko maana bado kuna hazina ya viongozi wengi wazee kwa vijana
 
Ongeza hii Mkuu.
tapatalk_1613487741521.jpeg
 
1. Katiba ya Jamuhuri wa muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na marekebisho yake ya 30th April 2000 yananipa haki zote kama raia halali wa taifa la Tanzania kuwa na mawazo huru juu ya jambo lolote ambalo halivunji sheria za nchi yetu.

Mimi kama Mtanzania tar.16/02/2020 nilianzisha uzi unaosema " KARIBU TUJIUNGE NA KUNDI LA MAGUFURI TENA 2025" na mjadala katika kundi hili ulikuwa unaendelea. Kwa bahata mbaya sana.

2. Katiba ya jamhuri ya Tanzania ( 1977) kuanzia ibara ya18(UHURU WA MAONI) , ibara ya19( UHURU WA MTU KUSHIRIKIANA NA MTU MWINGINE) kwa pamoja zinasema

Ibara 18.1 Bila kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake,na kutafuta,kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru mawasilano yake kutoingiliwa kati.

Naomba nielezee ibara hii ya 18.1; ni kwamba nina uhuru wa kutoa mawazo yangu yoyote, katika chombo chochote ikiwemo jamii forums, bila kuingiliwa na yeyote.

Ibara 20.1 Kila mtu anastahili kuwa Huru, bila ya kuathiri sheria za Nchi, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanyika, na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au mashirika yaliyo anzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.

Nia yangu ni thabiti, ni kuanzisha mchakato wa kubadirisha katiba kwa kukusanya signatures zaidi ya million tano za waTanzania ili kuweza kukidhi matakwa ya kikatiba ya kumuongezea angalau muhala mwengine Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli,

KAULI MBIO YETU NI.
"H.E President Magufuri is too valuable to retire, Tanzanians needs him now more than ever" " Mhe, Rais Magufuri ni wathamani sana kustaafu, Watanzania wanamuhitaji sasa kuliko kipindi kingine chochote"

MWISHO;
Kama nilivyo quote vipengele vya katiba, basi naomba mawazo yangu yaheshimiwe. situkana, sijapanga kuua, wala sija panga kuvunja sheria za nchi, ninafuata taratibu zote ili kubarisha vipengere vya katiba ambayo siyo Msaafu wala siyo Bibilia.
Mods futeni huu uzi...unaweza kusababisha maambukiz ya covid 19
 
Mleta mada nadhani walioweka kikomo cha miaka 10 walitafakari na kuona kabisa inamtosha kiongozi kufanya mambo yake kwa mujibu wa taratibu za kisheria na kukabidhi yale ambayo hatomaliza kwa mrithi wake.

Utaratibu wa kupokezana baada ya miaka kumi ni mzuri na umeshazoeleka kwakuwa ni sehemu ya checks and balance , hata ikitokea mbeleni huko tukapata rais ambaye pengine hatofanya vizuri tutakua tunajua kwa dhahiri kwamba tutakaa nae miaka kumi na kisha ataondoka madarakani... tukianza kubadilisha katiba tutakuwa tuna set kitu kinaitwa precedence.....huko mbeleni tutapata viongozi wengine ambao watatuambia nimefanya vizuri sana na hivyo hakuna haja hata ya kupiga kura kwa mfano na hatutakuwa na cha kumfanya maana anaweza kuwa ndani ya takwa la kisheria .......sidhani kama kuongeza muda wa rais itakuwa ni muarobaini wa matatizo yetu kwakuwa hata rais ni mtu wa kawaida tu loolote laweza kumfika....sasa kama utabadilisha katiba kwa ajili yake na ukute kesho yake hayupo unafanyaje ? unabadilisha tena au? Rais Magufuli ameonyesha njia na nadhani kupitia uongozi wake madhubuti nchini na ndani ya chama ataweza kutuletea kiongozi mzuri toka kwenye chama au kwingineko maana bado kuna hazina ya viongozi wengi wazee kwa vijana

Umeongea vizuri sana. Hoja zako zinakinzana na zangu, lakini umeongea kwa ustadi mkubwa na umeeleweka bila kutumia lugha mbaya.

Asante sana kwa ushauri wako, lakini kwa maoni yangu, huko nyuma tumeshajaribu sana maraisi mbali mbali, lakini hamna kitu wamefanya zaidi ya ufisadi kuongezeka nchini.

Pia, sio lazima tuwe na msululu wa marais wengi wastaafu, huu sio muarobaini wa matatizo yetu.
 
Teuzi zimeshaisha acheni shobo Mzee mwenyewe hataki kashakataa viherehere tu....halafu akiendelea muanze vurugu....
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom