Mimi nafikiri tatizo si Lugha ipi itumike,bali ni QUALITY ya wale wanaoingia katika taaluma hii ya ualimu.
Hapo awali miaka ya 60's,70's,80's mpaka 90's mwanzoni, kulikuwa na walimu wale waliofundishwa kipindi cha mkoloni na soon after that.
Backthen Ualimu ilikuwa taaluma yenye heshima,being a Teacher , lilikuwa ni suala la heshima mtaani.Kupata nafasi ya kusomea ualimu ,requirements zake zilikuwa za uhakika,ndiyo maana tukawa na walimu hao ninaowazungumzia hapo.
Mimi nadhani kuwa LUGHA si tazizo.
By the way fikiria haya yafuatayo:
Fikiria vitabu vyote tulivyonavyo katika sekondari na vyuo vibadilishwe kutoka English to Swahili kwa maana ya kuvitafsiri.Je, gharama za posho ya wale wataotafsiri itakuwa kiasi gani? ukizingatia siku zote za mradi huo.
Gharama za makaratasi,gharama za uchapishaji,ghrama za binding n.k
Mradi huu wa kubadilisha Lugha ya kufundishia mashuleni na vyuoni ni mkubwa mno,unahitaji fedha nyingi ambazo hatuna.NDIO MAANA HAO VIONGOZI WETU WANALIZUNGUMZA KISIASA ZAIDI.
Mjapani,Mjerumani,Mfaransa,Mkorea, wameweza kutumia lugha zao kutokana na uwezo wa kumudu gharama hizo na nyingine ambazo zipo associated na mradi kama huo.
Waswahili tunasema kupanga ni kuchagua,je,tupeleke pesa kwenye mradi kama huo au tujenge barabara?
Naomba kuwasilisha.