nyboma
JF-Expert Member
- Aug 29, 2021
- 2,308
- 7,366
Moja kwa moja kwenye historia yangu binafsi ya maisha yangu enzi za utafutaji, ni miaka takribani 27 imepita tangu mshiriki wangu katika biashara akimbie na fedha zote na mtaji na kutokomea kusikojulikana, kwa ufupi ni kwamba huyu bwana miaka hiyo enzi za utafutaji niliungana nae tukawa tunafanya biashara ya kuleta bidhaa moja adimu sana katika jiji la Dar es salaam.
Kusema kweli ile biashara ilitulipa sana, na utaratibu wa biashara ulikuwa na mlongomlongo mrefu kidogo (kuanzia kuifuata, kuinunua na kuisafirisha) ilituchukua takribani wiki mbili kuifuata bidhaa hiyo kutoka mkoa fulani ili kuifikisha katika sehemu yetu ya biashara ambayo ilikuwa Dar es salaam.
Baada ya kuona biashara yetu imechanganyia sana ili kuweza kuendana na kasi ya biashara tukawa tumejiwekea utaratibu mpya ya kwamba ikitokea mimi nimeenda kufuata mzigo, mwenzangu anabaki kituo cha kazi kumalizia mzigo uliobaki (reminants) na yeye ikitokea amesafiri kwenda kufuata mzigo basi na mimi ningebaki kumaliza mzigo uliobaki katika eneo letu la biashara.
Huu utaratibu uliendelea kwa kipindi fulani, hadi siku mmoja huyu mwenzangu alipoamua kutokomea jumla jumla siku alipoenda kufuata mzigo mpya, asikuambie mtu nilipitia kipindi kigumu sana maana fedha zote za biashara alitokomea nazo kusikojulikana kwa kuwa nilikuwa napafahamu kwao ilinibidi nifunge safari kwenda nyumbani kwao kuulizia kama alifika huko jibu nililolipata kutoka kwa wazazi na ndugu zake ni kwamba huyu rafiki yangu hakufika kwao kwa siku za karibuni, moja kwa moja nikajua mwenzangu eidha kaliwa na simba (maana enzi hizo sehemu kubwa ya tanzania ilikuwa imetawaliwa na mapori) wazo la pili ni kwamba kaaamua kukimbia na fedha zetu zote ili akaanze maisha sehemu nyingine tanzania, baada ya muda kupita ndipo nikagundua jamaa katokomea na fedha zote.
Narudia tena nilipitia kipindi kigumu sana kwa wakati huo nilikaa takribani mwaka mzima bila kujishughulisha na chochote na katika kipindi hicho nilikuwa nikifikiria naanzaje upya? kwa ule msongo wa mawazo niliokuwa nao katika kipindi kile ni kwamba nilimuachia Mungu aseme nae na ndipo akili ya kuanza upya ilinijia maana kwa wakati ule nilijua huwenda mwenzangu angeweza rudi na mzigo wa kutosha kumbe maskini nilikuwa napoteza muda bure ndio nikakata shauri nikajikusanya nikaanza upya na biashara ya ulanguzi nilipambana usiku na mchana na kwa kweli namshukuru Mungu mno kwa miaka ishirini (20) ya utafutaji na upambanaji nimepiga hatua kubwa mno, na kitu nilichojifunza katika miaka yangu 20 katika biashara ni;
Moja, hapa naomba niseme jambo moja kubwa kama Mungu alikuandikia kwamba “UTAPATA” ukweli ni kwamba utapata tu hata kama utakuatana na vizingiti vya namna gani” cha muhimu ni kuendelea kupambana maana changamoto tumeumbiwa sisi binadamu.
Pili, katika kufanya kwangu biashara na uhakika kabisa ukifanya biashara moja tu kwa zaidi ya miaka kumi na tano (15) na hakika Mungu lazma akupe “REWARD” na hakika ndani ya miaka hiyo hata kama ulianza ulanguzi na hakika kwa muda huo utakuwa umepiga hatua kubwa ya kuwa na duka lako kubwa la jumla, ukiona hujapiga hatua yoyote kwa biashara hiyohiyo jua kabisa unashida mahari.
Turudi kwenye kisa changu, labda niwaambie ni kwa sababu gani nimeamua kuwaletea hiki kisa, ni kwamba wiki iliyopita nikiwa Dodoma kwa majukumu yangu binafsi nilionana na mdaiwa wangu katika maeneo fulani akiwa amedhoofu mno ni mimi ndiye niliyemkumbuka na kumuita kwa jina lake mwanzo hakuweza kunitambua ila baada ya kumtajia jina langu “Nyboma” akanikumbuka kwa kweli nilisikitika mno kwa maisha niliyomkuta nayo kwa ufupi nilimuachia kiasi fulani cha fedha nikaamua kuondoka zangu moyo ukiwa mweupe kabisa.
Hitimisho, kwa wale rafiki zangu ambao wanatamani kuingia katika biashara ya partnership ni kwamba wawe makini na watu ambao wataingia nao katika kuanzisha biashara hiyo ya pamoja, kwa umri wangu nimeona mengi na zama za sasa binadamu hawaaminiki tena linapokuja suala la pesa.
Na mwisho kabisa siri ya mafanikio yangu ni “SAVING” nakumbuka miaka ya 80’s na 90’ dar ulikuwa mji wa starehe sana na watu ambao niliishi nao pamoja walikuwa watu wa starehe ila hadi naandika uzi huu leo asilimia kubwa bado wanaishi kwa nyumba walizojenga wazazi wao na wengine bado wapo kwenye nyumba za kupanga maisha yakiwa yamewaelemea enzi hizo hawa fedha zote walizopata walizitumia katika starehe wakijua kwamba watapata fedha tena kumbe maisha huwa yana hesabu yake pia nakumbuka kwa wakati huo mimi fedha zangu nilikuwa nafanya SAVING na kupitia saving ndio nimeweza miliki vyote nilivyo navyo leo hii.
Hivyo ushauri kwa wadogo zangu na vijana wangu mliopo huko makazini msiridhike na mishahara yenu mkawa mnaitawanya hovyo pasipo kufanya saving, mjitahidi hata kwa hicho hicho mnacholia kuwa ni kidogo wewe jinyime vitu fulani hata ukionekana wewe ni mshamba katika jamii inayokuzunguka yote sawa tu, ila katika akili yako unajua kabisa katika akaunti yangu ya benki niko na saving fulani ambayo nitaifanyia jambo fulani na zaidi nikukumbushe tu siku zote zoezi suala zima la saving liendane na wewe kuwa na wazo murua la biashara na hakika Mungu atakufungulia njia na utafanikiwa pakubwa mno.
Asubuhi njema.