Uchaguzi 2020 Hakika Dkt. Magufuli haamini macho yake. Alifikiri A, imekuwa B!

Uchaguzi 2020 Hakika Dkt. Magufuli haamini macho yake. Alifikiri A, imekuwa B!

Kwaiyo Lissu ndio atakununulia Nguo?
Jitume tafuta pesa kwa Akili na jasho lako, Watu wananunua ndinga mpya kila siku wewe unafikiria Lissu atakupa nafuu ya Maisha.
Miradi yote mikubwa anayofanya magu hela anapeleka kwa mabeberu na mzunguko wa pesa ndani ya inchi unakuwa mdogo. Ndege tatu tu ni sawa na angejenga hospitali kumi ktk mikoa tofauti ambayo ingeajiri watu wengi na hela ingezunguka na kodi ingekusanywa zaidi
 
Kwaiyo Lissu ndio atakununulia Nguo?
Jitume tafuta pesa kwa Akili na jasho lako, Watu wananunua ndinga mpya kila siku wewe unafikiria Lissu atakupa nafuu ya Maisha.
Atanipa nafuu ya maisha kwa kuimarisha uchumi(kwa kuimariaha sekta binafsi, kuongeza mshahara) ili na sisi wauza karanga na ubuyu na mitumba tuuze sana
 
Me mwenyewe kura yangu kwa Lissu....haiwezekani miaka mitano yote hii sijawahi kununua nguo dukani hata jeans moja tu.maisha magumu watoto wa wenye wanasoma tu na hakuna ajira
Matikiti maji yanauzwa 2000 kwa moja nenda kalime kama hutopata hela,wewe unabeti alafu utegemee kupata hela.
 
Jipange ukapige Kura kukamilisha idadi ya Kura Laki sita za Lisu dhidi ya zaidi ya m.20 za JPm,

Mwaka huu sijui mtaweka wapi Sura zenu
 
Ushamba na ulimbukeni akili amna ni kutumia mababu tuu
 
Pamoja na kuubana vilivyo upinzani kwa miaka yake mitano madarakani, haamini kuuona ukiwa na nguvu kwa namna hii hadi kuomba msaada wa wastaafu. Pamoja na kuuaminisha umma, tangu kuingia kwake madarani, kuwa anapendwa, anakubalika, anaheshimika na anaaminika kuliko yeyote yule kwenye uongozi, Dr. Magufuli haamini kuona wananchi 'wakitamani' kumuondoa madarakani kwa kura zao Oktoba 28.

Pamoja na 'mikwara' yake kwa makada wa CCM walioachwa pembeni wakati wa kura za maoni kuwa ni LAZIMA wawaunge mkono wagombea waliopitishwa na CCM yetu, Dr. Magufuli haamini macho yake anaposhuhudia sura za kukasirika na ghadhabu za makada hao. Makada wa maelfu nchi nzima wamejipanga kuwapigia kura wapinzani kwakuwa walioletewa hawakuwachagua.

Pamoja na kutumia jukwaa la Urais kwa miaka mitano kujinadi, kujiaminisha na kujitamba mbele ya watanzania, Dr. Magufuli hayaamini macho yake anapoona watanzania hawamulewi kwenye kampeni zake na hata hawasisimuliwi na ahadi zake tena. Wamejaa uchungu mioyoni mwao; wamepoteza matumaini kuliko kuyapata. Watanzania wanataka kuanza upya. Wanataka mabadiliko. Wanashindwa kumuelewa Dr. Magufuli.

Hakika, Dr. Magufuli haamini anachokiona. Ametarajia A, anaona B. Wako wapi wale waliokuwa wakimshabikia miaka yote mitano? Wako wapi waunga mkono juhudi? Ni wazi, tafakari atakayoifanya Chato kuanzia jana hadi tarehe 14/9/2020 itajikita katika kujiuliza: amewakosea nini watanzania hadi wampe 'surprise'hii ya kiuchaguzi? Atakapoanza na Kagera, ajirekebishe na ikibidi aombe radhi kwa kuteleza kwake kwa hili na lile.

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kahama, Shinyanga)
Mzee Tupatupa . Huyu kama si kubebwa na kitengo. Mbona chali muda mrefu tu
 
Me mwenyewe kura yangu kwa Lissu....haiwezekani miaka mitano yote hii sijawahi kununua nguo dukani hata jeans moja tu.maisha magumu watoto wa wenye wanasoma tu na hakuna ajira
Nimeona mgombea wenu bagamoyo anaongea alafu watu wanamcheki tu kisha wanasema hiiii, akiondoka wanafuta miguu vumbi🤣🤣🤣🤣
 
No one is perfect ila JPM for presidency. Subirini 2025.
 
Hali ilivyo kwa sasa
8b8772af65a848b2211cc750a1e7211b.jpg


Sent from my Infinix X624 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom