Hakika Mungu yupo na Watanzania. Ogopa Sana nchi ambayo watu wake si wepesi wa kuingia mtaani

Hakika Mungu yupo na Watanzania. Ogopa Sana nchi ambayo watu wake si wepesi wa kuingia mtaani

Woga tupa kulee

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2012
Posts
1,752
Reaction score
1,311
Tanzania ni nchi ambayo tumependelewa na Mungu. Nchi ambayo wananchi wake ni wapole na taasisi zake ikiwemo idara ya ujasusi na vyombo vya usalama ni imara mno na ambavyo haviwezi kuruhusu mtu yeyote wa mamlaka na cheo chochote achezee hatma njema ya nchi yetu.

Ukifanya hivyo, wananchi wa Tanzania huingia magotini na kushtaki kwa Mungu, na hii huweza kupelekea Mungu kukuita ili akipangie kazi nyingine!

Kongole vyombo vyetu vya ulinzi na usalama.
Kongole nchi na watanzania kwa ujumla.

Mungu ibariki Tanzania.
Mungu ibariki Africa.
 
Ulivyoingiza idara ya ujasusi na vyombo vya ulinzi ndipo ulipoleta mkanganyiko wa mada yako.

Maana hao jamaa wamekuwa wakisikia jamaa wakijinadi waziwazi kwenye chaguzi kuwa watashinda kwa kutumia dola na wao hawajawahi kukemea!

Ndo kusema chaguzi zilikuwa zikishinda kwa kutumia dola?

Chama chochote cha kisiasa kinatakiwa kushinda kupitia wananchi kikatiba na siyo dola hususa kwenye mfumo wa vyama vingi.
 
Ulivyoingiza idara ya ujasusi na vyombo vya ulinzi ndipo ulipoleta mkanganyiko wa mada yako.

Maana hao jamaa wamekuwa wakisikia jamaa wakijinadi waziwazi kwenye chaguzi kuwa watashinda kwa kutumia dola na wao hawajawahi kukemea!

Ndo kusema chaguzi zilikuwa zikishinda kwa kutumia dola?

Chama chochote cha kisiasa kinatakiwa kushinda kupitia wananchi kikatiba na siyo dola hususa kwenye mfumo wa vyama vingi.
Wana mkono katika kumwondosha mwendazake. Safari yake haikua natural kiivyo, Bali "elimination" of state's risk
 
Yes. Umesema kweli. Vizazi na vizazi vitasoma tulikuwa na rais aliyepuuza virus vya corona, watu wakafa kwa wingi na yeye mwishoni akafa kwa hiyo hiyo corona.
Tunajua alifariki kwa matatizo ya moyo..........uamuzi ni wako
 
Unajua wangapi wanaingia, waliingia, na bado wataingia Mtaani kwa Jina la Mungu ?

Pitia Historia tu itakwambia...., Imani ni Moja ya Jambo kubwa lililoangamiza Maelfu kwa Mamilioni ya Watu..., Watu hawachelewi kukwambia huko tulipopiga magoti tumeambiwa tuchukue mishale na mapanga....
 
Nimekuelewa, unamuongelea yule FEDHULI aliye garagaza Katiba, akaweka Bunge mfukoni, akaitisha Mahakama na akadhibiti vyombo vya habari.

Yule aliyeiba kura za uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2019 na uchaguzi Mkuu wa 2020 ili atawale milele. Watanzania walipiga magoti hatimaye Mungu akasikia hatimaye AKAFA kwa CORONA mwezi Machi 2021.
Hana legacy yoyote ile ya maana aliyo iacha! Zaidi tu aliwageuza nyinyi MATAGA kuwa misukule na waimba mapambio wake.
Tulishaambiwa tuibadili Historia ya Nchi hii kwa kuingiza haya mambo ya Jiwe, sijui imekaaje hii? tuachane na kina Rebman, Livingstone nk
amini nawaambia kwa utawala wa huyu Mama ni mwezi tutasahau yote ya Buldozer km alivunja Kimara kwa kuwa hakupigiwa kura, na Mwanza akwaacha na kuongeza daraja la Busisi
 
Ishu ni kuamini...........mbona povu? Fata upendacho

Last moments of the ‘Bulldozer’ John Pombe Magufuli​

Tanzanian President John Magufuli was discharged from Nairobi Hospital while on life support and flown to Dar es Salaam late last week after doctors concluded that he could not be resuscitated, the Nation has established.

The President, who was flown to Kenya secretly on March 8 after suffering acute cardiac and respiratory illnesses, was under intubation when a decision was made to fly him back home.

Magufuli’s entry and exit from Kenya was a guarded affair, that only select National Intelligence Service (NIS) officials and members of the National Security Advisory Committee were aware of.

Sources say he died at Mzena Hospital shortly after arrival on Thursday last week, contradicting the Tanzanian government’s official account of the death occurring on Wednesday this week.

“Dear Tanzanians, it is sad to announce that today, March 17, 2021, around 6pm, we lost our brave leader, President John Magufuli, who died from a heart disease at Mzena hospital in Dar es Salaam,” Vice President Samia Suluhu Hassan announced on state broadcaster on Wednesday, shortly before midnight

While the Tanzanian government had long denied that President Magufuli was sick, the Nation was the first media house to report the admission to Nairobi Hospital of “an African leader” on March 9.
 
Wana mkono katika kumwondosha mwendazake. Safari yake haikua natural kiivyo, Bali "elimination" of state's risk


What if he was advanced accordingly and disagreed?

Should we still blame them?

Na misimamo ya jamaa ilikuwa inajulikana?!
 
Back
Top Bottom