Kwa wale wapenzi wa historia ambao tulizoe kusoma kuhusu miujiza katika misahafu mtaelewa ninachosema.Inawezekana kabisa mkachanganywa na mazingaombe mfanyiwayo mmkifikiri ni miujiza.
Tundu Lissu Amekuwa kama Sauti ya mtu aliaye Nyikani,Ni muujiza unaotembea.Anatupa habari njema kuhusu kuja kwa neema katika Tanzania.John Pombe Magufuli ambaye kama JINA lake lilivyo alikuwa ni Yohana tu ambaye ni mtangulizi wa Mteule.JPM alilijua hilo ndio maana shetani alitaka kumwondosha ili mpango wa Mungu usitimie kwa Tanzania kuwa nchi ya neema.Nchi ya furaha,nchi ya matumaini.
Jaribu kufikri taifa ambalo watu wote wana afya tele na furahamTaifa ambalo limejaa haki,taifa lenye utu.Hii ndio Tanzania ya Tundu Lissu na JPM kama alivykuwa yohana Mbatizaji alikuwa ni Mtangulizi wake.
Aliwahi kusema Mzee Makamba kwamba JPM atatupa ubatizo wa moto kumbe alikosea.Ubatizo wa JPM ni ubatizo wa Maji.Tundu Lissu ataleta Ubatizo wa moto.
Imeandikwa kwamba John Pombe Magufuli atakuwa ni rais wa Muula mmoja Tanzania,Rais Pekee ambaye atakosa kura katika kipindi cha pili, Rais atakayekabidhi serikali kwa Upinzani.Maneno haya ya unabii yameshatimia na yeyote atakayoyapinga ndani au nje ya sanduku la kura atakuwa anatafuta laana ya Watanzania.
Mtazame TUNDU LISU, kauli zake ujasiri wake,upeo wake mkubwa lakini ZAIDI haiba yake.Anajiamni zaidi ya JPM kwa sababu ya upeo wake na upendo wake kwa Watanzania wote.
ndio JPM ni Mtangulizi wa Tundu Lissu na sasa ni wakti wa kwenda na Tundu Lissu
Nawatakia Tafakari njema.
Bado niko Kimbiji-Katika ufukwe wa bahari ya hindi nikibarizi kipupwe.