Hakimu aliyekuwa akisaimamia kesi ya Sabaya abadilishwa

Hakimu aliyekuwa akisaimamia kesi ya Sabaya abadilishwa

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
6,404
Reaction score
6,969
#UPDATES HAKIMU wa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Salome Mshasha,anayekuwa akiliza kesi namba 66 ya Unyanganyi wa kutumia silaha iliyokuwa inamkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai,Ole Sabaya na wenzake amebadilishwa kusikiliza kesi hiyo, sasa itasikilizwa.
===
HAKIMU wa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Salome Mshasha, anayekuwa akiliza kesi namba 66 ya Unyanganyi wa kutumia silaha iliyokuwa inamkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Ole Sabaya na wenzake amebadilishwa kusikiliza kesi hiyo, na sasa itasikilizwa na Hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo, baada ya kufutwa kwa mashtaka ya awali na kufunguliwa mengine matatu.

Nipashe
 
Acha uongo mkuu. Hilo ni jambo la kawaida na dogo sana katika corridor za mahakama.
 
Hakuna zengwe, inatokea kwa kesi nyingi tu.....
Kwa mwenendo tunaoshuhudia hivi leo kesi ya sabaya ni kiini macho kwa watanzania ,hapo hakuna jipya mbali na ushahidi dhahiri ambao upo na utakaokuwepo na utakao endelea kuwepo.
 
  • Thanks
Reactions: mmh
Sio zengwe ile ni michezo ya ccm watu wamjadili sabaya badala ya kujadili bajeti toka kwa wabunge wa serikali.
 
Sio zengwe ile ni michezo ya ccm watu wamjadili sabaya badala ya kujadili bajeti toka kwa wabunge wa serikali.
Nasema hii ilikuwa danganya toto, ili kuwaridhisha watanzania, kwani madhambi yaliyoratibiwa nao kupitia wakala wao huyo yalikuwa haya mithiliki tena.
 
sasa hivi kipaumbele siyo katiba tena tumetoka kwenye katiba tukaenda kwenye miamala tukitokahapo tunaenda kitu kingine kustukia 2025 hyo hapo wapinzani chali tena hawajauza serazao
 
Kwa mwenendo tunaoshuhudia hivi leo kesi ya sabaya ni kiini macho kwa watanzania ,hapo hakuna jipya mbali na ushahidi dhahiri ambao upo na utakaokuwepo na utakao endelea kuwepo.
Ushahidi upo..ila wanatishwa watu....
 
Sio zengwe ile ni michezo ya ccm watu wamjadili sabaya badala ya kujadili bajeti toka kwa wabunge wa serikali.
Na Raia tumegoma kumjadili huyo sabaya wao na walisubiria siku tozo zikianza ndo wamupeleke mahakamani. Tumechoka na usanii wao
 
Huyu ataachiwa soon kama nawaona watu wakitapika nyongo

Ccm hawajawahi kuwa serious kwa chochote
 
Japo kubadili hakimu ni kawaida lakini sababu lazima itokewe, ila hapa kwa Sabaya dalili zilishaonesha mapema hamna kesi ni usanii tu unaoendelea, watakuwa wameona huyo hakimu alikiwa haeleweki upande wao wameona bora wamuweke mtu wao.
 
#UPDATES HAKIMU wa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Salome Mshasha,anayekuwa akiliza kesi namba 66 ya Unyanganyi wa kutumia silaha iliyokuwa inamkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai,Ole Sabaya na wenzake amebadilishwa kusikiliza kesi hiyo, sasa itasikilizwa..../https://t.co/Hq4VYofwjB https://t.co/EIcEOXfo8Q
We akili zako kama za sabaya tu
 
Back
Top Bottom