Huu ni ushahidi mwingine kuwa elimu yetu imeshuka sana. Vijana wetu hawafaulu bali wanafaulishwa, wanakariri badala ya kuelimika. Mwendesha mashitaka ña watoa hukumu Kuna vitu vingi hawakuvizingatia kwenye kesi ya aina hii inayogusa sura ya nchi, uchumi wa nchi, italii wa nchi, usalama wa nchi na diplomasia ya nchi. Waliruhusu kuchezea amani, utulivu, uchumi, na dipromasia ya nchi.
Mfano, mahakama ilijiridhisha kuwa akina magoma wanawakilisha watu wangapi kati ya watu wangapi miongoni mwa Wadau wa Yanga? Walijirisha kama akina magoma wanao uwezo wa kuiendesha Yanga ya sasa kama wakimuondoa Hersi na wenzake? Walijirishisha na usalama wa akina magoma baada ya hukumu? Walijirisha kuwa akina Fatma Karume na wenzake wamewakilishwa kwa usahihi kwenye kesi? Walijirisha na matokeo yote ya hukumu kwenye amani na utulivu, uchumi wa nchi, utalii, mpira wetu, wadhamini wa mpira na ajira za wachezaji na wafanyakazi. Maana bila ya Simba na Yanga imara hata Azam media, NBC Bank, TBC, NIC, CRDB, sportpesa, m-bet, nk wasingekubali kujiingiza kwenye udhamini. Ukweli hakimu wa Magoma lazima wahojiwe walikuwa wanakusidia nini kitokee.