Hakukuwa na sababu ya Profesa Mkenda kuzungumza aliyoyazungumza hadharani. Kiongozi ni kuwa na Kifua na Uvumilivu

Ndugu zangu Watanzania,

Sote tumeyasikia maneno na kauli za Waziri wa Elimu Mheshimiwa Profesa Adolph Mkenda akilalamika kuwa alizungushwa kupata nafasi ya kuonana na Mheshimiwa Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan.

Mimi Mwashambwa nimejiuliza maswali ya je kulikuwa na sababu zipi za kuyaongea hayo masuala hadharani? Yalikuwa na umuhimu upi na sababu zipi? Alishindwa nini kuyaongea faragha alipopata nafasi ya kuongea na kuonana na Mheshimiwa Rais?

Je waziri hana njia nyingine za kuwasiliana na kufikisha ujumbe wake kwa Rais? Je waziri hawezi kuwasilisha jambo hilo kwenye kikao cha Baraza la mawaziri na kutoa dukuduku lake na kero yake ili mambo yazungumzwe na kuonyana humo humo badala ya kuleta hadharani?

Pia soma:
Juu ya Waziri Wa Elimu kuna Naibu Waziri Mkuu, Waziri Mkuu ,Makamu wa Rais kabla ya kumfikia Rais Mwenyewe. Sasa kwanini asingemtumia hata mmoja wapo kati ya hao kupeleka jambo lake na kero yake hiyo?

Hata alipopelekewa kikaratasi mezani kwake kwanini na kulikuwa na sababu gani ya kujibu kwa jeuri kuwa yale aliyokuwa anayaongea yalikuwa ni Sehemu ya hotuba yake? Kwanini alikuwa anaonyesha kana kwamba yupo kwenye mgogoro na wasaidizi wa Rais na sasa anataka kuwachongea na kutunishiana misuli hadharani? Yalikuwa na sababu gani hadi ya kusema kuwa tuliambiwa tuongee kwa saa mbili tu?

Kwanini Waziri ambaye ni Profesa kabisa anakosa kifua na uvumilivu pamoja na subira ya mambo madogo kama hayo? Kama jambo dogo kama hilo linamshinda kuvumilia na kukaa kimya bila kuonyesha hasira zake hadharani,anaweza vipi vumilia mambo makubwa na kukaa nayo mpaka anaingia kaburini? Unapokuwa kiongozi mkubwa ni pamoja na kubeba maumivu na kutunza siri kwa gharama kubwa na Maumivu.

Hivi kama Rais Samia Mama yetu kipenzi asingekuwa na kifua na uvumilivu na kuamua kuzungumza kila kitu hadharani. Unafikiri angezungumza mangapi mazito baada ya kuapishwa kwake kuwa Rais? Au mmesahau ni nini Mkuu wa Majeshi wetu mstaafu Mheshimiwa Jenerali Venance Mabeyo alichokisema na kilichotokea baada ya kifo cha Hayati Mwalimu Daktari John Pombe Joseph Magufuli?

Mmesahau Kauli ya Jenerali Mabeyo kuwa kuna watu walisahau katiba inasema nini na kwamba akawakumbusha Matakwa ya Katiba mara baada ya kufa kwa Rais? Hivi mnaichukuliaje kauli hiyo? Mnaelewa Maana yake? Mnataka niwafungulie mabano ili muelewe?

Je mnafikiri watu hao waliosahau matakwa ya katiba Hawapo hai? Mnafikiri hawapo Tanzania? Mnafikiri hawapo serikalini?? Mnafikiri Mama yetu Mpendwa hawafahamu? Mnafikiri Mama yetu kipenzi hafahamu kilichotokea baada ya kifo cha Hayati? Au mnafikiri amekaa kimya kwa sababu hajui kitu?

Jibu ni kuwa anafahamu kila kitu na ameamua kukaa kimya na kuendelea na kazi kwa sababu anajua maana ya uongozi. anajua maana ya kutunza siri. Anajua Ukubwa ni jalala. Anajua jambo gani linapaswa kuzungumzwa hadharani na lipi halipaswi kuzungumzwa hadharani. Anajua kuna mambo yanapaswa kukaa kifuani na kubakia kama siri mpaka Kifo.

Na huo ndio uongozi. Ndio Ukubwa.Ndio uongozi unavyotaka hivyo kwa kiongozi wa juu kuwa na kifua ,kutunza siri,kuwa na subira, uvumilivu na kujizuia kuongea vitu kwa msukumo wa hasira,jazba, mihemuko na kukurupuka. Kama Rais Samia angetaka kuongea kila kitu hadharani basi Nchi ingesimama. Nasema tena kuwa NCHI ingesimama hii.

Viongozi wetu jifunzeni kuwa na siri,vifua, uvumilivu na subira. Tumieni busara na hekima katika kuzungumza hadharani na chagueni maneno ya kuzungumza mbele ya hadhira. Na ikiwezekana someni hotuba mlizoandaliwa kuliko kutumia hisia bila mantiki kuzungumza na kujikuta mkiharibu na kuleta taswira mbaya kwa jamii .

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Linapokuja swala la ukweli hamtaki kabisa kusikia nyie ni watu wa namna gani
 
Anza na chanzo cha tatizo aka vijumbe wa mama, unadhani waziri atoke huko atokako kwenda oga? Tuwe wakweli bila pepesa macho waliteleza wajirekebishe hilo ndo la msingi
 
Hatuna Rais
20241230_165724.jpg
 
Anza na chanzo cha tatizo aka vijumbe wa mama, unadhani waziri atoke huko atokako kwenda oga? Tuwe wakweli bila pepesa macho waliteleza wajirekebishe hilo ndo la msingi
Unaelewa namna serikali inavyofanya kazi. Unafahamu ya kuwa RAIS ni taasisi
 
Mleta hoja kuna hautendei haki moyo wake ... Za Moyoni mbali ziandikwa mbali...
 
Hivi SUFIANI yupo wapi? Naona ile roho iliyokuwa kwake imehamia kwa mleta mada ....
 
Msaidizi wa Rais sio Rais. Waziri ni mkubwa kuliko msaidizi wa Rais. Mkenda yuko sahihi kabisa kuwanyea hao wapuuzi. Huu upumbavu ukichekewa ndo husababisha watu kuwa na chuki na Rais. Msaidizi wa Rais kumpelekea kimemo waziri wakati anahutubia ni utovu wa nidhamu.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Sote tumeyasikia maneno na kauli za Waziri wa Elimu Mheshimiwa Profesa Adolph Mkenda akilalamika kuwa alizungushwa kupata nafasi ya kuonana na Mheshimiwa Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan.

Mimi Mwashambwa nimejiuliza maswali ya je kulikuwa na sababu zipi za kuyaongea hayo masuala hadharani? Yalikuwa na umuhimu upi na sababu zipi? Alishindwa nini kuyaongea faragha alipopata nafasi ya kuongea na kuonana na Mheshimiwa Rais?

Je waziri hana njia nyingine za kuwasiliana na kufikisha ujumbe wake kwa Rais? Je waziri hawezi kuwasilisha jambo hilo kwenye kikao cha Baraza la mawaziri na kutoa dukuduku lake na kero yake ili mambo yazungumzwe na kuonyana humo humo badala ya kuleta hadharani?

Pia soma:
Juu ya Waziri Wa Elimu kuna Naibu Waziri Mkuu, Waziri Mkuu ,Makamu wa Rais kabla ya kumfikia Rais Mwenyewe. Sasa kwanini asingemtumia hata mmoja wapo kati ya hao kupeleka jambo lake na kero yake hiyo?

Hata alipopelekewa kikaratasi mezani kwake kwanini na kulikuwa na sababu gani ya kujibu kwa jeuri kuwa yale aliyokuwa anayaongea yalikuwa ni Sehemu ya hotuba yake? Kwanini alikuwa anaonyesha kana kwamba yupo kwenye mgogoro na wasaidizi wa Rais na sasa anataka kuwachongea na kutunishiana misuli hadharani? Yalikuwa na sababu gani hadi ya kusema kuwa tuliambiwa tuongee kwa saa mbili tu?

Kwanini Waziri ambaye ni Profesa kabisa anakosa kifua na uvumilivu pamoja na subira ya mambo madogo kama hayo? Kama jambo dogo kama hilo linamshinda kuvumilia na kukaa kimya bila kuonyesha hasira zake hadharani,anaweza vipi vumilia mambo makubwa na kukaa nayo mpaka anaingia kaburini? Unapokuwa kiongozi mkubwa ni pamoja na kubeba maumivu na kutunza siri kwa gharama kubwa na Maumivu.

Hivi kama Rais Samia Mama yetu kipenzi asingekuwa na kifua na uvumilivu na kuamua kuzungumza kila kitu hadharani. Unafikiri angezungumza mangapi mazito baada ya kuapishwa kwake kuwa Rais? Au mmesahau ni nini Mkuu wa Majeshi wetu mstaafu Mheshimiwa Jenerali Venance Mabeyo alichokisema na kilichotokea baada ya kifo cha Hayati Mwalimu Daktari John Pombe Joseph Magufuli?

Mmesahau Kauli ya Jenerali Mabeyo kuwa kuna watu walisahau katiba inasema nini na kwamba akawakumbusha Matakwa ya Katiba mara baada ya kufa kwa Rais? Hivi mnaichukuliaje kauli hiyo? Mnaelewa Maana yake? Mnataka niwafungulie mabano ili muelewe?

Je mnafikiri watu hao waliosahau matakwa ya katiba Hawapo hai? Mnafikiri hawapo Tanzania? Mnafikiri hawapo serikalini?? Mnafikiri Mama yetu Mpendwa hawafahamu? Mnafikiri Mama yetu kipenzi hafahamu kilichotokea baada ya kifo cha Hayati? Au mnafikiri amekaa kimya kwa sababu hajui kitu?

Jibu ni kuwa anafahamu kila kitu na ameamua kukaa kimya na kuendelea na kazi kwa sababu anajua maana ya uongozi. anajua maana ya kutunza siri. Anajua Ukubwa ni jalala. Anajua jambo gani linapaswa kuzungumzwa hadharani na lipi halipaswi kuzungumzwa hadharani. Anajua kuna mambo yanapaswa kukaa kifuani na kubakia kama siri mpaka Kifo.

Na huo ndio uongozi. Ndio Ukubwa.Ndio uongozi unavyotaka hivyo kwa kiongozi wa juu kuwa na kifua ,kutunza siri,kuwa na subira, uvumilivu na kujizuia kuongea vitu kwa msukumo wa hasira,jazba, mihemuko na kukurupuka. Kama Rais Samia angetaka kuongea kila kitu hadharani basi Nchi ingesimama. Nasema tena kuwa NCHI ingesimama hii.

Viongozi wetu jifunzeni kuwa na siri,vifua, uvumilivu na subira. Tumieni busara na hekima katika kuzungumza hadharani na chagueni maneno ya kuzungumza mbele ya hadhira. Na ikiwezekana someni hotuba mlizoandaliwa kuliko kutumia hisia bila mantiki kuzungumza na kujikuta mkiharibu na kuleta taswira mbaya kwa jamii .

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
MANAANZA KUJITAMBULISHA MSIOJULIKANA WA KUFANYA MAMBO GIZANI NYUMA YA MGONGO WA RAIS. Mtasema mliowapoteza wako wapi!!!..
 
Africa ukisema Uongo ndo una hekima, ukisema ukweli huna kifua....shubaamit
 
Msaidizi wa Rais sio Rais. Waziri ni mkubwa kuliko msaidizi wa Rais. Mkenda yuko sahihi kabisa kuwanyea hao wapuuzi. Huu upumbavu ukichekewa ndo husababisha watu kuwa na chuki na Rais. Msaidizi wa Rais kumpelekea kimemo waziri wakati anahutubia ni utovu wa nidhamu.
Naona ni mbumbumbu wa uongozi. Hivi hufahamu kuwa Urais Ni Taasisi inayojitegemea?
 
Kabla ya kutoka nje kuzungumza na hadhara wote watakaopewa nafasi ya kuzungumza mbele ya Rais hotuba zote lazma azupitie na wakati mwengine Huwa wanapangiwa vya kuongea kwahyo alichokiongea Prof Mkenda kina baraka zote za Mh Rais kabla hajasema pale

..Prof.Mkenda aliweka hotuba pembeni akaongea free style.

..mimi nilivyomsikiliza Prof hakuwa amemsema Raisi vibaya.
 
Naona ni mbumbumbu wa uongozi. Hivi hufahamu kuwa Urais Ni Taasisi inayojitegemea?
Mimi mbumbumbu wa uongozi? Komredi unanikosea sana. Futa hiyo kauli yako ya kipumbavu. Mkuu najua Rais ni taasisi ila haimaanishi hao wasaidizi wake wawe na nguvu za kupitiliza hadi kuwa kikwazo kwa waziri. Rais alimteua Waziri Mkenda na kumpa dhamana ya kusimamia elimu ya nchi kwahiyo kwa vyovyote vile waziri hapaswi kuewekewa vikwazo na wasaidizi wa Rais. Hao wasaidizi wanamharibia Rais na kumtengenezea taswira mbaya.
 
Itoshe kusema Kuna watu hawapaswi.kuwa viongozi na kama wanakuwa viongozi basi wapewe semina elwmesi kama zile za JK.

Mtu kama Mkenda maisha yake yote ameishia kufundisha Chuo Kikuu ni Magufuli ndio alimleta kwenye Uongozi ila hakuwa na sifa za uongozi wako wengi sana watu wa hivyo.

..aliyemtoa Prof.Mkenda Udsm ni Rais Kikwete.

..alimteuwa Prof.Mkenda kuwa Naibu Katibu Mkuu wizara ya fedha -- Sera.
 
Kumleta kwenye nafasi za Kisiasa ,hizo Bado ni za utendaji.

Mkenda namfahamu nilimkuta Chuo anafundisha enzi za JK alikuwa anafundisha Chuo.

Kwanza kaoa Mzambia sijui hata kama ni raia yule mama hajui kiswahili kabisa nae ni mwl.wa.uchumi Mlimani.
 
Mimi mbumbumbu wa uongozi? Komredi unanikosea sana. Futa hiyo kauli yako ya kipumbavu. Mkuu najua Rais ni taasisi ila haimaanishi hao wasaidizi wake wawe na nguvu za kupitiliza hadi kuwa kikwazo kwa waziri. Rais alimteua Waziri Mkenda na kumpa dhamana ya kusimamia elimu ya nchi kwahiyo kwa vyovyote vile waziri hapaswi kuewekewa vikwazo na wasaidizi wa Rais. Hao wasaidizi wanamharibia Rais na kumtengenezea taswira mbaya.

..mimi ni mkosoaji mkubwa wa Mama Abduli na serikali yake, lakini ktk suala hili namtetea yeye pamoja na Prof.Mkenda.

..Ratiba ya Raisi inaweza kuwa tight na kupelekea Waziri kukosa nafasi ya kuonana naye kulingana na aina ya appointment aliyoomba.

..Prof.Mkenda katika hotuba yake aliomba kwenda kumuona Raisi akiwa na timu ya wataalamu wa wizara ya elimu.

..Sasa appointment za namna hiyo sio sawa na appointment anayoomba Waziri kwenda kushauriana na Raisi kwa muda mfupi.

..Wengine wamekwenda mbali kusema Waziri anaweza kumpigia simu Raisi. Jambo hilo ni la kweli, lakini sio kazi ya Raisi kuratibu appointments zake.

..Waziri akitaka kuonana na Rais ni lazima aongee na Katibu Myeka wa Rais ambaye ana jukumu la kuratibu appointments za Raisi.

..Ratiba ya Raisi inaweza kuwa open kuonana na Waziri kwa mashauriano mafupi, lakini inaweza kuwa tight kama Waziri anataka kuonana na Raisi akiwa na timu ya wataalamu ili wafanye presentation kwa Raisi.

..Kwa jinsi nilivyomsikiliza Prof.Mkenda hicho ndicho alichomaanisha.
 
Kumleta kwenye nafasi za Kisiasa ,hizo Bado ni za utendaji.

Mkenda namfahamu nilimkuta Chuo anafundisha enzi za JK alikuwa anafundisha Chuo.

Kwanza kaoa Mzambia sijui hata kama ni raia yule mama hajui kiswahili kabisa nae ni mwl.wa.uchumi Mlimani.

..Prof.Mkenda kuoa Mzambia sio kigezo cha yeye kukosa sifa za uongozi.

..pia Prof.Mkenda sio waziri pekee katika serikali ya Mama Samia ambaye mke wake sio mzaliwa wa Tanzania.
 
Back
Top Bottom