Hakuna anayejali kuhusu wewe

Hakuna anayejali kuhusu wewe

Mtu anayejali ataonekanaje mtandaoni na fake IDs ana matatizo aisee.
 
Kuja vitu unakuta hatuwezi kuvifanyia kwa sababu ya macho ya wengine lakini kumbe ni hofu zetu tu
 
View attachment 3216160

Je huwa unaogopa kuishi maisha yako kwa kuhofia watu watakuonaje?

Huwa unaogopa kuchangia mijadala mbali mbali ili usionekana hauna uelewa wa kutosha?

Huwa unaogopa kupost kwakuwa unadhani sio mwandishi mzuri?

Huwa unaogopa kujichanganya na watu kwakuwa unahisi wewe sio mzungumzaji mzuri?

Ngoja nikwambie kitu expert,jua kwamba hakuna anayejali kuhusu wewe,kila mtu ana mambo yake binafsi yanayo mshughulisha,machoni pako na mawazoni mwako unaweza hisi watu wanakufuatilia au wanazungumza kuhusu wewe ila ukweli ni kwamba,kila mtu ana dili na mambo yake

Kwahiyo acha kufikiri kwamba watu wanakufuatilia laa,acha kuwaza kwamba watu wanakuwekea kipaumbele,jibu ni hapana,kila mtu anashughulishwa na mambo yake

Kwahiyo you are in your own,fanya mambo yako na ishi vile unavyoishi maadamu humkwazi mtu,haumvunjii mtu heshima yake,ishi maisha yako

Ni hayo tu!

Salute mkuu 🏋️
 
Back
Top Bottom