Hakuna anayeupenda umaskini ila suala la kuzipata pesa za mauza uza hapana kwa kweli, wacha tuzisake kibishi turidhike na kidogo tunachokipata

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
Hizo pesa za mauza uza hata waganga wanazikimbia ilhali wao wana uwezo wa kuzipata ila hawazitaki kabisa, hata mhitaji akifanikiwa kuzipata mganga anazikwepa.

Mganga pale anakuwa ni dalali tu anaewaunganisha anaezitaka na majini.

Huyo anaezitaka inabidi atoe kitu muhimu kwake kwa majini ili apewe hizo pesa, inaweza kuwa ni kumtoa kafara mzazi wake, mtoto wake, mke wake na hizi kafara ni endelevu zinazoanziaga kwenye kuku mpaka watu, hakuna kugeuka nyuma ukianza umeanza.

Hata ukifa haufi, si kifo cha kawaida, roho yako inaenda kutumikishwa kwenye shughuli za ufalme wa majini, majinii yanakurahisishia sana njia ya mkato kimafanikio, lakini mwisho wake ni hatari sana kuliko hata mwizi / tapeli.
 
Mwenye namba za mganga konki wa hela za mauzauza aweke hapa
Hao hawanaga namba, kwa mtaalam hadi ufike inabidi uwe umetafuta connection kwa ambao wameshaungwa.

Ukifika kwa mganga huko hakuna kugeuka nyuma, utaambiwa upo tayari kukubali masharti au lah! Masharti utayajua ukikubali na hakunaga kuyabatilisha ukishakubali, ukiwa kiburi wa kuyafata ama kutaka kuyakimbia unakuwa chizi
 
"There's no free lunch at everywhere in the world"

Ndiyomaana hata Mungu anakutaka utoe 10% za zaka na sadaka kadri unavyobarikiwa.

Shetani anakurahisishia njia ya mkato kimafanikio, lakini mwisho wake ni hatari sana kuliko hata maelezo.
 
😁😁😁utelezi mtamu

Pisi zinataka pesa

Na pesa hazikamatiki........... mwenye namba ya mganga naomba
 
MnatAfuta matatizo,tulipata shida sana Kuna mtu alimpa mshua jiwe kinawaka Kama almasi,nakwambia tulipata matatizo yasiyoelezeka mpaka Leo mshua hayupo vyema kivike
 
MBona ukizitafuta kwa halali unazipata tena nyingi haswa, nyingi sana na hautaamini!! Weka imani kwenye nguvu yako tu!!

Na ukishazipata nyingi sana kuna mijuha itakuja kukusema wewe ni freemason hahaaa🤣🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…