Hakuna bara lenye uhuru kama Afrika

Hakuna bara lenye uhuru kama Afrika

Narumu kwetu

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2015
Posts
1,888
Reaction score
4,489
Africa kiukweli kuna Uhuru sana wa kufanya shughuli nyingi za kujipatia rizki ,ukilinganisha na mabara ya ulaya na Asia ,mfano hapa bongo ukitaka kufanya biashara yoyote unafanya hakuna vipingamizi vingi ,yaan ,hakuna ufuatiliaji sana.

Mfano kuna jamaa yangu ni gold prospectus hana leseni yoyote anajitafutia dhahabu huko Chunya anaishi maisha mazuri ,wengine ni wamachinga, bodaboda, mama ntilie, waziba pancha, wachota maji, wauza magenge, wapiga rangi, mafundi magari, simu, pikipiki, nyumba, yaani full kujiachia.

Pia unaweza kumiliki usafiri ambao umeshapita mda wake ilimradi linatembea, kiufupi huku waafrika wantembelea magari kuanzia ya mwaka 1996 ,unapeta tuu mradi services.ila sasa nenda uingereza fungua genge, mama ntilie,au uwe fundi tuu huna cheti wala leseni uone, au ukaendeshe hiyo carina yako ya tangu mwaka 1998 au gari lililozidi miaka 5 tangu litolewe kiwandani.

Baba kodi yake unapaki ,kumiliki gari mabara mengi ya ulaya ni ndoto ngumu sana kwa watu wenye kipato cha wastani ,ila bongo watu wenye vipato vya wastani wengi wanapeta mtaani full ac au sasa nenda Australia ukachimbechibe dhahabu yaan kule hata ukikamatwa na kakipande ka point moja ka dhahabu. unakula nondo nyingi.

Yaani ukienda geita hadi watoto wanachenjua vimchanga wanjipatia visent, yaan maisha yakikushinda Africa hutaweza kutoboa popote labda ukauze sembe,ila wanaotoboa kimaisha wakiwa ughaibuni wengi ni wapambanaji kwelikweli ,ukienda ulaya kwa akili ya huku kwetu ambapo mambo mteremko utaomba urudishwe mwez humalizi.

NB; Uhuru upo wa aina nyingi na utumwa upo wa aina nyingi nifikirie unavyojua
 
Enyi wapumbavu jueni ya kwamba huko Ulaya serikali zao zimeweka miundombinu bora na ya uhakika kwa kila mtu tofauti na huku Afrika ambako serikali zetu zimewaacha wananchi wajiendeshe kama mifugo.

Mfano huko Ulaya ukitaka kufungua biashara ya duka la aina fulani, hawawezi kukuruhusu ufungue sehemu ambako tayari hiyo huduma ipo....
Yani wameweka mpangilio na mazingira ambayo ni ya uhakika kwa kila mfanyabiashara kulipa kodi bila malalamiko wala kuonewa.

Huku Afrika mtu akiona umefungua duka ukapata wateja nae anakuja kufungua pembeni yako duka la bidhaa hizohizo jambo ambalo kwa wenzetu serikali zao haziruhusu maana mnakuwa mmekaa kama nyanya kwenye tenga na kuvuruga mpango mzima wa kila mfanyabiashara kufanya kazi ya uhakika huku akilipa kodi ya serikali na huku na yeye akisonga mbele kwa uhakika wa 100%.

Kama kuna watu watano wa kuhudumia mtaa mmoja kwa uhakika hiyo inatosha! Kama umetamani sana kutoa huduma kama hiyohiyo unaweza kutafuta mtaa ambao huduma hiyo haipo au waliopo hawawezi kukidhi mahitaji ya huo mtaa ndipo na wewe uruhusiwe kutoa huduma kama hiyo.

Ubovu wa miundombinu yetu na ukosefu wa ajira sio wa kuufurahia kabisa bali kuulaani... Kumbuka huku mtu anaweza kuweka biashara kama yako mbele ya mlango wa biashara yako na bado serikali yetu ikamlinda 😄😄huu ujinga kwa wenzetu hauruhusiwi

Hatuwezi kuiga ya kwao kwa 100% maana huku ajira ni tatizo kubwa sana!
Kadhalika wao pia hawawezi kuiga ya kwetu maana wao ni binadamu wanaoutendea haki ubinaadamu wao.

TTusifurahie matatizo yetu ndugu zangu bali tuyalaani na kuyapiga vita
 
Sasa kwaini huku kuna lindi kubwa la unaskini kuliko ughaibuni ilhali shughuli za kujipatia kipato huku kwetu ni bwelele??
 
Vipi kuhusu

Bima za afya
Huduma za maji
Huduma za umeme
Unemployment benefits
 
Usitake tuwe ka wZungu sisi ni weusi na tulikuwa na maisha yetu mazuri kulikuwa no criminal records,Wala magonjwa after interaction na wazungu wa Africa tukaharibikiwa, so kujipima na ulaya it's not fair
 
Kama serikali zetu za kiafrika zingeshughurikia baadhi ya changamoto ndogo tu kama mikopo nafuu na usalama ninaamini wazungu wangelazimika kuongea kiswahili & kiha ili kupata VISA
 
Ndio Uhuru huo bwashee pia miundo mbinu siyo haba mfano ukitaka kwenda sehemu nyingi Tanzania miundombinu siyo mibaya angalau inaendana na ufukara wetu,ila tunajivunia Uhuru wa kufanya tunachotaka kwenye kutafuta mkono uende kinywani
 
Sasa kwaini huku kuna lindi kubwa la unaskini kuliko ughaibuni ilhali shughuli za kujipatia kipato huku kwetu ni bwelele??
Huku hatufanyi kazi ,tunataka maisha ya ulaya wakati tuna maisha zaid yao
 
Ndio Uhuru huo bwashee pia miundo mbinu siyo haba mfano ukitaka kwenda sehemu nyingi Tanzania miundombinu siyo mibaya angalau inaendana na ufukara wetu,ila tunajivunia Uhuru wa kufanya tunachotaka kwenye kutafuta mkono uende kinywani
Alafu Ikawaje tukawa nyuma kwa mambo yote mazuri/maendeleo?
 
Back
Top Bottom