Narumu kwetu
JF-Expert Member
- Jul 12, 2015
- 1,888
- 4,489
Africa kiukweli kuna Uhuru sana wa kufanya shughuli nyingi za kujipatia rizki ,ukilinganisha na mabara ya ulaya na Asia ,mfano hapa bongo ukitaka kufanya biashara yoyote unafanya hakuna vipingamizi vingi ,yaan ,hakuna ufuatiliaji sana.
Mfano kuna jamaa yangu ni gold prospectus hana leseni yoyote anajitafutia dhahabu huko Chunya anaishi maisha mazuri ,wengine ni wamachinga, bodaboda, mama ntilie, waziba pancha, wachota maji, wauza magenge, wapiga rangi, mafundi magari, simu, pikipiki, nyumba, yaani full kujiachia.
Pia unaweza kumiliki usafiri ambao umeshapita mda wake ilimradi linatembea, kiufupi huku waafrika wantembelea magari kuanzia ya mwaka 1996 ,unapeta tuu mradi services.ila sasa nenda uingereza fungua genge, mama ntilie,au uwe fundi tuu huna cheti wala leseni uone, au ukaendeshe hiyo carina yako ya tangu mwaka 1998 au gari lililozidi miaka 5 tangu litolewe kiwandani.
Baba kodi yake unapaki ,kumiliki gari mabara mengi ya ulaya ni ndoto ngumu sana kwa watu wenye kipato cha wastani ,ila bongo watu wenye vipato vya wastani wengi wanapeta mtaani full ac au sasa nenda Australia ukachimbechibe dhahabu yaan kule hata ukikamatwa na kakipande ka point moja ka dhahabu. unakula nondo nyingi.
Yaani ukienda geita hadi watoto wanachenjua vimchanga wanjipatia visent, yaan maisha yakikushinda Africa hutaweza kutoboa popote labda ukauze sembe,ila wanaotoboa kimaisha wakiwa ughaibuni wengi ni wapambanaji kwelikweli ,ukienda ulaya kwa akili ya huku kwetu ambapo mambo mteremko utaomba urudishwe mwez humalizi.
NB; Uhuru upo wa aina nyingi na utumwa upo wa aina nyingi nifikirie unavyojua