Hakuna Fao la Kujitoa NSSF duniani kote - Ramadhan Dau

mlitegemea nini kutoka kwa RAMADHANI? haya huyu hapa nimemzungushia duara yupo kijiweni
 

Attachments

  • ramadhani.jpg
    74 KB · Views: 135
Zomba hebu kua na weledi some times? Kwa nini serikali iwaonee huruma wafanyakazi ambao si zaidi ya m3 wakati kuna watu zaidi ya 15m ambao hawapo kwenye mfumo wa pension? yaani huruma inakuja kwetu tu?....

Sababu ya kukupa like ni hapo nilipo-bold umefikiria zaidi ya uwezo wa kawaida, kweli kabisa kuna babu zetu kule Itabagumba wamechoka na wanaowategemea wamechoka na wengine wanalea yatima ambao wameachiwa na watoto wao, but hakuna juhudi zozote za kuwasaidia na iweje kwa hawa watu wasiozidi milion 3 tena kupitia ajira zao wana uwezo wa kupata mikopo bank kwa makubaliano ya kupitisha mishahara kwenye bank husika ndio serikali iwaonee huruma na kuacha kundi kubwa.

(Wafanyakazi ni zana ya kukuza mifuko ya taasisi ya serikali na ndio maana hata hizi PAYE ni kandamizi mtu analipwa 3m ikija kodi anakatwa karibu laki 8 wakati mfanyabiashara anaweza akawa na biashara kubwa ya milioni kadhaa na halipi kodi kama hiyo).

TATIZO WACHUMI WETU WANANGALIA VYANZO VYA MAPATO VILIVYO WAZI WANASHINDWA KUWA WABUNIFU KWA KUFIKIRIA ZAIDI NAMNA YA KUONGEZA MAPATO NA WANACHAMA WENGINE KATIKA MIFUKO YAO)
 
hatuna wakumtegemea hapa zaidi ya kelele za wabunge wetu wa chadema kikao kijacho...na tafadhari haijalishi mtashinda au kushindwa katika hili pigeni kelele kadri mtakavyoweza ili hawa mbwa wapate headache...mkinyamaza mtatuangusha wakuu...afu hawa viongozi wa vyama vya wafanyakazi wapo wapi? na nini kazi yao mbona hatuwasikii hata wakitoa misimamo yao? kama hoja hii ikitupwa wamobilize migomo na maandamano kupinga huu wizi na udharimu wa magamba...kila nikifikiria jasho langu/michango yangu machozi yananitoka....hivi magamba hawajui wao ndo wametufikisha hapa tulipo? wanataka kuchukua na hichi kiduchu tukichobakiwa nacho? hakika MUNGU yupo na tutashinda tu>>>
 
Zomba hebu kua na weledi some times? Kwa nini serikali iwaonee huruma wafanyakazi ambao si zaidi ya m3 wakati kuna watu zaidi ya 15m ambao hawapo kwenye mfumo wa pension? yaani huruma inakuja kwetu tu?

Sababu ya kukupa like ni hapo nilipo-bold umefikiria zaidi ya uwezo wa kawaida, kweli kabisa kuna babu zetu kule Itabagumba wamechoka na wanaowategemea wamechoka na wengine wanalea yatima ambao wameachiwa na watoto wao but hakuna juhudi zozote za kuwasaidia na iweje kwa hawa watu wasiozidi milion 3 tena kupitia ajira zao wana uwezo wa kupata mikopo bank kwa makubaliano ya kupitisha mishahara kwenye bank husika ndio serikali iwaonee huruma na kuacha kundi kubwa. (Wafanyakazi ni zana ya kukuza mifuko ya taasisi ya serikali na ndio maana hata hizi PAYE ni kandamizi mtu analipwa 3m ikija kodi anakatwa karibu laki 8 wakati mfanyabiashara anaweza akawa na biashara kubwa ya milioni kadhaa na halipi kodi kama hiyo). TATIZO WACHUMI WETU WANANGALIA VYANZO VYA MAPATO VILIVYO WAZI WANASHINDWA KUWA WABUNIFU KWA KUFIKIRIA ZAIDI NAMNA YA KUONGEZA MAPATO NA WANACHAMA WENGINE KATIKA MIFUKO YAO)
 
Zomba hebu kua na weledi some times? Kwa nini serikali iwaonee huruma wafanyakazi ambao si zaidi ya m3 wakati kuna watu zaidi ya 15m ambao hawapo kwenye mfumo wa pension? yaani huruma inakuja kwetu tu?

Unasema nini wewe wakati kwa mara ya kwanza tunaona wakulima wakisaidiwa na mifuko ya pensheni? huyo huyo ambae ameboresha NSSF huyo huyo aliyeleta huo mpango mzuri wa mafao uzeeni huyo huyo ndiye kwa mara ya kwanza tunaona hizo fedha zetu zikijenga madaraja, vyuo vikuu, na zikisaidia wakulima na wafanya biashara, hata Mbowe alikopoa huko mamilioni kibao kuendeleza disko lake la bilicanasa, au hujui?

Kuhusu wakulima soma chini hapa fata na hiyo link, na kwa mara ya kwanza tunaona mifuko ya pensheni ikianza kufikishwa kwa wakulima, ambao ni zaidi ya asilimia 70 ya Watanzania. walikuwa wapi wa kabla ya Dau na Kikwete? kwanini hatukuyaona yote hayo?

Wakulima wahakikishiwa huduma bora
 


Naungana kabisa na Dr Ramadhani Dau kwani nimekaa sana kwenye uongozi wa Fedha sijapatapo kusikia kitu kama hicho.

Hata huku kwetu kuna watu wa mafuta ambao ni sawa sawa kabisa na kwenu huko watu wa madini. Sisi na nchi zote zimeweka utaratibu maalum kwao kuhakikisha haki yao kimsingi ya mafao yao wanayapata pindi wakifikisha muda wa kustahafu. Huku tumeweka mikopo maalum ambapo watu hao wanaweza kukopa na kufanya biashara au shughuli nyingine lakin haki yake ya mafao yake anawekwa kwa ajili ya kustahafu.

Hongera sana Dr Dau kusema hayo tena kwa kubainisha wazi kuwa hakuna kitu kama hicho duniani. Hongera Dr Dau kwa kuonyesha weledi wako na msimamo wako na kutokubali kuumbishwa na wana siasa.
 
NSSF walipoanzisha hilo fao hawakuwa duniani?
 

Nina uhakika ni mfuasi wa CUF wakali kwa kukopi na kupaste!!
(CDM) M4C wao CUF chap chap bila hata aibu wakaja na V4C !!
 
Kauli kama hizi ndiyo zinafaa kutriger maandamano hadi kinuke. Ni kauli iliyojaa dharau kwa wafanyakazi ambao kimsingi ndio waajiri wake.
 
Nimemsikiliza huyu mwishiwa Dau, kweli kaniudhi sana, sasa nilikua na hamu kujua hizo nchi zote duniani alizozisema nikaona anataja, Zanzibar, Kenya na Uganda, kumbe hizi kwake ndio reference point yake? ajabu kweli kweli, anyaway, South Africa wanalipa after 3 days of your termination, Malaysia na Indonesia wanalipa after 2 days after termination, Zimbabwe nao pia wanalipa, kwenye nchi zilizoendelea hizo tuziache kabisa, kwasababu hata wasio kua na kazi pia wanapata posho ya kujikimu, hapa kwetu vipi? Ni aibu kubwa kwa Dr. kama yeye kutolea mifano ya nchi kama Zanzibar, Kenya na Uganda, hivi hawa si huwa wanazunguka duniani kwenda kuona wenzao wanacho kifanya? Wadokta wengine bana!
 
Nimemsikiliza kwakweli nimepatwa na hasira sana, mbaya zaidi anaongea akijichekesha chekesha.
Anadai utaratibu unatakakiwa ukifukuzwa kazi utafute kazi pengine uendelee kuchangia
halafu nikikosa iyo kazi inakuwaje
 

Bwana Barubaru, Ki Jiolojia, Heavy metals and other minerals tabia haziko sawa kabisa na madini (sijui kama nayo yanasifa ya madini) yaitwayo mafuta, Dhahabu, Almasi n.k huwa migodi yake inafungwa, mfano ni Buhemba na Tulawaka plus Nzega, itafungwa very soon! Chukua muda wa kufanya kautafiti kidogo, hilo moja, pili, security ya kazi huko Uarabuni na huku kwetu ni vitu viwili tofauti, wapo wenzetu wengi tu huko wanafanya kwenye migodi ya jinsi hii, hata mshahara tu, mgeni hawezi kumzidi mwenyeji kama wapo rank sawa, huku kwetu sisi sio issue ya rank tu, mgeni hata kama unamzidi Rank, bado atakuzidi tu mshahara, so point yangu hapa ni hii, kulinganisha vitu mjaribu kua fair, angalieni in all angles, sio kuangalia just a single angle only!
 

Hivi huyu Dau ameisoma sheria yote ya mifuko ya jamii ya ULAYA au amechomoa tu vifungu vinavyo mfurahisha?

Ulaya kama ameachishwa/umepunguzwa kazi wakati ukiwa huna kazi unalipwa UNEMPLOYEMENT BENEFIT/ALLOWANCE. Je Dau na NSSF yake wako tayari kutoa hilo fao?

Kama mmeamua kufuata ya ULAYA basi mfuate kila kitu sio kuchomoa vipengelea vinavyo wafurahisha. STUPIDY
 
Tusubirie tuone mwisho wa hizo lobbying na ushawishi wa wafanyakazi wa serikali na SSRA maana wanachokifanya wanajua matokeo yake kwamba nchi itawaka moto kama watashindwa kwenye Bunge lijalo kutatua hili kero inayozidi hata janga la gonjwa la UKIMWI.
Hakika kutakuwepo na Kazi ya ziada na kama walivyosema wafanyakazi wa Migodini kwa kuwakilishwa na Geita God Mine ( GGM) serikali ifanya maandalizi ya kutosha kupambana na Mengi ambayo wanaweza wasiamini kama watayaziba masikio na macho wasione adhali za hili.
Maisha ni magumu kwani kinachopatikana mwisho wa mwezi hakitoshelezi, fgharama za maisha zimepanda kwa hiyo tegemeo lililoko mbele ya wanyakazi hawa ni hizi pesa zao zilizoko mifuko ya hifadhi ya jamii.
Mungu awape MAONO walijadiri swala kwa manufaa ya WATU wake vinginevyo kama iotakuwa ndo kujiandaa na uchakuaji wa hizi FEDHA zetu kwa ajiri ya uchaguzi 2015 Basi tusubirie hilo TIFU.
 

Sa nyingine nashindwa kukuelewa kabisa yaani nishangilie pesa yangu kujengea daraja? na hizo pesa za kodo zinaenda wapi ? Zomba kunawakati nakukubali lakini kwa hapa umechemka unalazimisha hoja
 

Hawa ndiyo wasomi wetu Tanzania,eti wapo kwa maslahi ya wananchi
 

Ukilaza wake ni kusoma bila kuelimika.
 
hata Mbowe alikopoa huko mamilioni kibao kuendeleza disko lake la bilicanasa, au hujui?
Wakulima wahakikishiwa huduma bora
Kila mtu ana haki ya kukopa popote ilimradi akidhi masharti. iwe mimi iwe wewe hakuna shida! ishu hapa nikitaka changu napewe sio eti ninyimwe kisa kinajenga daraja la kigamboni? Kodi zetu mnapeleka wapi? acha ukanjanja Zomba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…