Nelson Jacob Kagame
JF-Expert Member
- Dec 26, 2022
- 9,576
- 13,545
Kuna kitu wauaji huwa wanajihisi"Upweke"sababu hakuna furaha kwenye kutoa roho ya mtu hasa pale mnapokutanisha macho kwa ghafla wakati wa tukio husika.
Anakutazama kwa macho ya kukuuliza "Kwanini mimi"? Hata unapomvizia kwa ghafla pale mwili wa binadamu anapoanguka chini unajihisi hatia, ukimwekea sumu utajihisi hatia, ukimpiga risasi utajihisi hatia and ect.
Nazungumzia aina zote za mauaji sababu ukitoa uhai wa mtu lazima hisia mkondo(Sindikizi) za uhai wake utazihisi. Hakuna furaha kwa wauaji hata kama hawajashiriki moja kwa moja, nafsi zao huwasuta.
Sijui Mungu aliumba vipi roho ya mwanadamu sababu ukifanya dhambi ya kuua lazima ukose amani ya moyo. Mungu sijui aliweka nini katika hili, wauaji huwa hawana furaha na amani maisha yao yote hata kama walichofanya ni siri.
Asilimia kubwa ya wauaji huwa wanajuta baadae kimoyo moyo kuhusu walichofanya.