Hakuna furaha kwenye uuaji, damu ya binadamu ina roho

Kuna kuua makusudi kwa kudhulumu nafsi. Mfano mtu hana issue yoyote na wewe mara unaenda kumuua, lazima marehemu akuulize kwa nini umeniua? Kama ulitaka kumdhuru na katika kujitetea, nafsi yako inakuwa na jibu kuwa nimekuua ili kujilinda maana ulitaka udhulumu nafsi yangu bila kosa...
Mimi nadhani kuua ni kuua tu na hakuna kinachofanya mauaji ya mwanadamu mwingine yawe halali.
 
Jamaa alimpiga risasi tajiri, huku akitapatapa akamkazia macho na kusema kwa uchungu " Fulani ni wewe kweli unaniuwa sababu ya pesa?" Akakata roho, ila muuwaji mpaka Leo anapeta na pesa ya huyo tajiri. Kisa kilitokea huko Kenya.
 
Kuna kitu wauaji huwa wanajihisi"Upweke"sababu hakuna furaha kwenye kutoa roho ya mtu hasa pale mnapokutanisha macho kwa ghafla wakati wa tukio husika.

Anakutazama kwa macho ya kukuuliza "Kwanini mimi"? Hata unapomvizia kwa ghafla pale mwili wa binadamu anapoanguka chini unajihisi hatia, ukimwekea sumu utajihisi hatia, ukimpiga risasi utajihisi hatia and ect.

Nazungumzia aina zote za mauaji sababu ukitoa uhai wa mtu lazima hisia mkondo(Sindikizi) za uhai wake utazihisi. Hakuna furaha kwa wauaji hata kama hawajashiriki moja kwa moja, nafsi zao huwasuta.

Sijui Mungu aliumba vipi roho ya mwanadamu sababu ukifanya dhambi ya kuua lazima ukose amani ya moyo. Mungu sijui aliweka nini katika hili, wauaji huwa hawana furaha na amani maisha yao yote hata kama walichofanya ni siri.

Asilimia kubwa ya wauaji huwa wanajuta baadae kimoyo moyo kuhusu walichofanya.
@william ruto kwani uongo [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mnakuwaga wakakamavu hivi hivi ila baada ya kutekeleza tukio kila siku kanisani kuitafuta amani ambayo kimsingi hutaipata mpaka unakufa.

Kuua binadamu ni complex issue
Hapa ndicho nachomaanisha kaka.Nilimuona Eric Holder alipoenda mahakamani baada ya kumuua Nipsey Hustle ,alikua hana amani ya moyo hata kwa kumtazama machoni.Lakini wakati anafanya mauaji yale alikua anajifeel shujaa nobody can look down on him.
 
Jamaa alimpiga risasi tajiri, huku akitapatapa akamkazia macho na kusema kwa uchungu " Fulani ni wewe kweli unaniuwa sababu ya pesa?" Akakata roho, ila muuwaji mpaka Leo anapeta na pesa ya huyo tajiri. Kisa kilitokea huko Kenya.
Sidhani kama ana amani ya moyo???
 
Walio idhinisha mtu kama sadamu anyongwe huwa wanajionaje na wale wanyongaji wanaomnyonga mtu ambaye video zake zimetapakaa
 
Kuna kitu wauaji huwa wanajihisi"Upweke"sababu hakuna furaha kwenye kutoa roho ya mtu hasa pale mnapokutanisha macho kwa ghafla wakati wa tukio husika.

Anakutazama kwa macho ya kukuuliza "Kwanini mimi"? Hata unapomvizia kwa ghafla pale mwili wa binadamu anapoanguka chini unajihisi hatia, ukimwekea sumu utajihisi hatia, ukimpiga risasi utajihisi hatia and ect.

Nazungumzia aina zote za mauaji sababu ukitoa uhai wa mtu lazima hisia mkondo(Sindikizi) za uhai wake utazihisi. Hakuna furaha kwa wauaji hata kama hawajashiriki moja kwa moja, nafsi zao huwasuta.

Sijui Mungu aliumba vipi roho ya mwanadamu sababu ukifanya dhambi ya kuua lazima ukose amani ya moyo. Mungu sijui aliweka nini katika hili, wauaji huwa hawana furaha na amani maisha yao yote hata kama walichofanya ni siri.

Asilimia kubwa ya wauaji huwa wanajuta baadae kimoyo moyo kuhusu walichofanya.
Siamini katika jambo hili. Watu wanaua na wanasonga tu na maisha yao wanakula bata tu.
Kuna watu wameua watu wengi halafu hata hawawazii kuhusu hilo.
Nmeshawahi kuona mahojiano ya mabosi wa mexican drug cartels walioko gerezani, wala hakuna wanachojutia wala kuota. Wengine ambao ni hitmen wanakwambia wao walikuwa wanaona kama kazi tu na ukipewa kazi lazima uitimize, ukitumwa kuua lazima utimize huna haja ya kufikiri
 
Japo mimi sio mjuzi ila kuna watu wanachukuliwa tangia wadogo wanakuwa trained wawe assasins / hitmen ..wanaondolewa na kufutwa kabisa roho kwenye kitu kinaitwa upendo, huruma wala hatia tangu wakiwa na umri mdogo ..Muda ukiwa mkubwa unafikiri atahisi nini anapotekeleza jukumu lake. .. ni wewe na mm tu ndo tutahisi hatia ila kuna wauni wanaona kama kaua panya.
 
Ila kuna vipindi wanajihisi hatia.Au ukiua na akili zinavurugiks na kila kitu unaona sawa??
 
Just imagine yule mke wa Cohen yule bilionea mdutch aliyeuawa na yule mama wa kikenya na kutupa maiti yake kwenye septic tank.
Si yupo anapeta na mali kachukua hana habari wa hajutii
Ila hali yake kiakili ni kama hayupo sawa akikumbuka ule ukatili aliyomfanyie yule mzee.Au unamaanisha anapeta kivipi??
 
Just imagine yule mke wa Cohen yule bilionea mdutch aliyeuawa na yule mama wa kikenya na kutupa maiti yake kwenye septic tank.
Si yupo anapeta na mali kachukua hana habari wa hajutii
Kumuona akipeta na mali na magari mazuri haimanishi ana furaha.

Sikiliza ushuhuda wa watu waliookoaka( confess) kutoka kwenye matukio kama hayo watakwambia ukweli wa hali halisi
 
Japo mimi sio mjuzi ila kuna watu wanachukuliwa tangia wadogo wanakuwa trained wawe assasins / hitmen ..wanaondolewa na kufutwa kabisa roho kwenye kitu kinaitwa upendo, huruma wala hatia tangu wakiwa na umri mdogo ..Muda ukiwa mkubwa unafikiri atahisi nini anapotekeleza jukumu lake. .. ni wewe na mm tu ndo tutahisi hatia ila kuna wauni wanaona kama kaua panya.
Una pointi mkuu,ila hata wale assasins pia wana hisia.Au wapo tofauti kidogo na binadamu wengine
 
Back
Top Bottom