Ndugu mtoa mada, napenda kukupongeza kwa kutoa mada nzuri, Kwa hakika maoni yako ni mazuri sana.
Lakini, Kabla ya kufikia hitimisho lako yatupasa tukumbuke kuwa mara nyingi mahakama za Tanzania zimekuwa zikiheshimu mapendekezo ya marehemu juu ya nani apewe nini kwenye mali zake.
Mara nyingi mgogoro huwa inatokea pale inapoonekana wazi kabisa hata Kwa mtu wa tatu (Reasonable man test) kuwa mgawanyo wa mali aliofanya marehemu ni wa ajabu na mtu yeyote mwenye akili ya kawaida tu asingeweza kufanya hivyo.
Mfano katika hali ya kawaida mtu hawezi kuacha kuwarithisha wanae wa kuwazaa mali zake na badala yao amrithishe Jirani au mke mdogo pekee, katika akili ya kawaida hii inakataa.Ndo maana hata sheria yenyewe mfano sheria za kimila zinakataza kum disinherit mwanao wa kumzaa isipokuwa Kwa sababu zifuatazo; Awe alitembea na mama yake (mke wako),Awe alitaka kukuua Ili arithi Mali,Awe hakukuhudumia wakati unaumwa haliyakuwa uwezo alikuwa nao.
Lakini pia endapo mahakama itajiridhisha wosia ulikuwa una mapungufu ya kisheria au labda mtoa wosia hakuwa katika hali nzuri ya kiakili,mahakama huingilia kati ili kulinda maslahi ya watu wengine waliotakiwa kuwa wafaidika.
KWENYE ISSUE YA MAREHEMU MREMA.
Kwa kuwa bado ni tetesi, Kwa kiasi kikubwa tunazoandika hapa ni hisia tu.
Labda inawezekana wosia wa mzee Mrema umeacha mali nyingi Kwa bi mdogo na haujaacha chochote Kwa Watoto. Kiubinadamu hata kama watoto tayari ni wakubwa na wana mali zao lazima itawauma na watachallenge huo wosia na wanaweza hata kuutilia shaka kama umeandikwa na baba yao.
Lakini pia Kwa sasa Kuna trend mbaya inaendelea ya mabinti wadogo kuolewa na vikongwe, Kwa kiasi kikubwa jamii hutengeneza dhana kuwa mabinti hao hufuata Mali, Kama itakuwa si kweli na badala yake hufuata mapenzi tujaribu kukuuliza kwanini mzee akiondoka tu wanaanza kugombea Mali. Kama ulimfuata mtu na mtu huyo hayupo kwanini usiondoke kimya kimya tu bila kudai chochote?
Wanaume tuache kuandika wosia tukiwa vifuani Kwa wake zetu (Joke).