Hakuna haja ya kuandika Wosia kama Mahakama inaubatilisha

Hakuna haja ya kuandika Wosia kama Mahakama inaubatilisha

Nashkuru kuzaliwa Muislamu
katika Uislamu hili ni jambo dogo sanaaa wala halihitaji complication ya aina yyte ile

Kamuulize Sheikh yyte yule alosoma dini vizuri hilo suala halina complication yyte ile kwenye Uislamu

Uislamu ni dini yangu
Am proud to be Muslim
Kweli kabisa
 
Kwa Nchi zetu hizi za kimasikini unakuta kila mtu alipewa na kachezea Mzee akivyokua hai ni ngumu kuomba tena wahuni wanabaki kutamani Mali zilizobaki ukiona wanagombana kama kwa Mzee Mrema mara nyingi wengine hata na Marehemu walikua hawaendi sawa ila wanataka mali zake..wahuni hawafanyi kazi wanasubiri kurithi tuu ukiuliza eti mimi mtoto wake..
 
Inapotokea sheria hizi haijafuatwa na mtu amabaye ndio anaandika wosia huweza kupelekea wosia huo kukataliwa na mahakama,

Baadhi ya sababu hizo ni
- kuto kumtaka msimamizi wa mirathi
-Kutokutaka mali zako zote.
-Kutokutaja Watoto/ Mama kama warithi
-Kutokuwa na umri unaoruhusiwa 18+
-Kutokuwa katika hali ya utimamu wa akili wakati ukiandika Wosia (Example mengi case)
- kutokufuata utaratibu wa uandishia wa wosia (example Muslim hutakiwi kuweka mali zako zote Wakfi lazima kiasi cha mali kibaki kwa ajili ya familia.
Nikushukuru kwa ufafanuzi mzuri. Kupitia ufafanuzi huu bado ninayaona mapungufu ktk sheria ya mirathi na wosia.

1. Sheria iko juu ya matakwa ya marehemu. Nimeliona hilo hapa
"Inapotokea sheria hizi haijafuatwa na mtu amabaye ndio anaandika wosia huweza kupelekea wosia huo kukataliwa na mahakama",

Binafsi
ningelipenda kuona sheria inalinda zaidi na kufuata matakwa ya marehemu badala ya kutaka yenyewe ndiyo ifuatwe.
2. Kutokumtaja msimamizi wa mirathi kusibatilishe wosia bali mahakama ichukue nafasi ya usimamizi ama kusaidia kupatikana kwa msimamizi.
3. Kutokutaja mali zote kusibatilishe wosia. Utaratibu ufanyike wa kuzibaini na mahakama ishughulike tu na mgawo wa mali ambazo hazikutajwa na marehemu.

4. Umri (sawa)
5. Utimamu wa akili. Hiki ndiyo kichaka wengi hukitumia kubstilisha wosia. Sheria ishughulike na vipengele vile tu ambavyo vimeongezwa wakati marehemu akiwa kwenye vegetative state. Tunafahamu kuwa wosia hauandikwi mara moja kwa watu wenye mali nyingi na za muda mrefu kama akina Mengi. Huwa wana "update" kwa kuongeza zinazoongezeka.
6. Wosia usibatilishwe kwa kutokufuata utaratibu wa uandishi. Utaratibu wa uandishi ni kama vile upo juu ya matakwa ya marehemu.

Naomba kuwasilisha.
 
Ndugu....watafute zao. Kwann washobokee mali za marehemu?

Wazazi ......hawa muda wao wa kuishi umeisha. Mali wapewe za nn?

Watoto....wale wenye miaka chini ya 25 wapewe kwa kadri marehemu alivyowmua. Lkn watoto wenye miaka 25+ wasipewe hata senti. Wapambane kivyao.
Na wewe tafuta zako why utake za marehemu? Maana kama ni kuchangia utajiri wa marehemu ndugu pia wanachangia sana
 
Kama unaamini kuna kitu unaweza fanya kwa kushurutishwa!, Basi hata wosia unaweza kuandika kwa kushurutishwa! Ndipo tafsiri ya kisheria inahusika kumediate pande zote in a win win situation.
 
Mkuu inategemeana inawezekana muhusika aliandika wosia akiwa juu ya kifua Sasa unakuta sio akili yake ya maamuz yake
 
Naye tajiri akawajibu wale watumishi akisema, 'je, si haki yangu kutumia mali yangu kama nipendavyo'?
Screenshot_20220830-214233.jpg
Screenshot_20220830-214201.jpg
 
Back
Top Bottom