Hakuna haja ya kuandika Wosia kama Mahakama inaubatilisha

Kwenye kesi Mzee Erasto Msuya, baba yake ambaye yuko hali alikuwa anadai miongoni mwa Mali zilizoshikiliwa na mashemeji wa marehemu ni Mali zake alizomrisisha marehemu akitegemea zitakuja kuwafaa wajukuu zake lakini ghafla Mali zinahamia ukweni.. Jmn sio Jambo jepesi. Kama mnasema waache kulilia Mali za marehemu watafute zao kwanini na upande mwingine nao wasitafute zao wang'ang'anie Mali za marehemu. Tuwe na huruma kumbuka marehemu ana ndugu, wazazi, watoto iweje wewe uchukue zote?
 
Tuwe na huruma kumbuka marehemu ana ndugu, wazazi, watoto iweje wewe uchukue zote?
Ndugu....watafute zao. Kwann washobokee mali za marehemu?

Wazazi ......hawa muda wao wa kuishi umeisha. Mali wapewe za nn?

Watoto....wale wenye miaka chini ya 25 wapewe kwa kadri marehemu alivyowmua. Lkn watoto wenye miaka 25+ wasipewe hata senti. Wapambane kivyao.
 
Ilikuwa kimkakati..wachaga sio wa ki spot spot 😂 😂 😂 😂 😂 😂
 
Nashkuru kuzaliwa Muislamu
katika Uislamu hili ni jambo dogo sanaaa wala halihitaji complication ya aina yyte ile

Kamuulize Sheikh yyte yule alosoma dini vizuri hilo suala halina complication yyte ile kwenye Uislamu

Uislamu ni dini yangu
Am proud to be Muslim
 
Asante. Hapo ndio unapoona umuhimu wa mirathi kwa waislam
 
Asante umemaliza mkuu. Nami najivunia kuwa muislamu na nitaishi maisha ya kiislamu na. Namuomba Allah anifishe nikiwa muislam. Amiin
 
Nafikiri pesa ndio imebatilisha sio mahakama. Pesa ni kama ccm inachoshindwa ni kumfufu mfu tu.
Dah! Kwa mtazamo wangu naona umekosea sana kuifananisha pesa na hiyo takataka aisee!

Siku zote hiyo takataka huwa inafananiswa na vitu vya uharibifu tu kama fisi, mchwa, ukoo wa panya, majambazi, mafisadi, majangili, nk.

Pesa ina hadhi yake mkurugenzi.
 
Asante umemaliza mkuu. Nami najivunia kuwa muislamu na nitaishi maisha ya kiislamu na. Namuomba Allah anifishe nikiwa muislam. Amiin
Waislam nao wanapelekena Mahakamani siku hizi, ingawa sheria zao za kiislam ziko wazi na zeny mashiko sana, kuliko hizi sheria za mahakama za kawaida.
 
Asante umemaliza mkuu. Nami najivunia kuwa muislamu na nitaishi maisha ya kiislamu na. Namuomba Allah anifishe nikiwa muislam. Amiin
Kwa waislamu ishu ya mirathi sio kubwa sana Kwa sababu zifuatazo;

Sheria ya kiislamu imeweka ukomo wa uhuru wa mtoa wosia kugawa mali zake. Muislamu anaruhusiwa kugawa 1/3 pekee ya Mali zake.

Mgawanyo wa mali zinazobaki unakuwa umeelezwa bayana kwenye Quran na Qiyas etc.
 
Kwani yeye alikuwa kama Dada wa kazi au mke? Maana mke anamhudumia mmewe, Dada wakazi anamshahara na mke vipi, huo muda si angetafuta pesa zake!
 
Ulichokiandika hakina uhalisia wa maisha na ndo mawazo haya yanaleta matatizo nchi nyingi za ki maskini.Kama mtu mwenye mali kaamua kuoa mwenye umri mdogo kuliko yeye na AKENDA KWA MWANASHERIA,na kumuandikia urithi wa mali zote huyo mpenzi wake,wengine inawahusu nin.Mambo ya kuandika urithi ni mambo ya kisheria,inabidi yaheshimiwe hata kama kwa ndugu jamaa na jamii kwa ujumla hatuyaelewi.Hao ndugu kwa nin walishindwa kumwambia awaandikie watoto zake au jamaa zake wengine wakati yupo hai?mali ni zake kama kaamua kuhonga,kupeleka kwenye mizimu,kutupa ni zake hili inabidi lieleweke! Hayo mambo ,sijui alichuma na nani mara ohhh kuna watoto wengine kwani marehemu alikuwa hayajui yote haya au alisahau kama alizaa si alikuwa anajua,na pamoja na yote akaamua kumwachia mimali huyo demu,labda ana sababu zake,matakwa yake yaheshimiwe.
 
Tatizo unaandika Wosia baada ya kupewa mahaba na mchepuko, andika ukiwa na akili timamu
 
Wajasiria mwili wanataka kula bila jasho. Wanakuja jua ndio linazama halafu wapate share nono hapana aisee.
 
Hakuna neno sipendi kulisikia kama WAKRISTU badala ya WAKRISTO
Pitia huu uzi kwanza
[emoji1484][emoji1484][emoji1484][emoji1484]

 
Nimeshangaa sana mtu tajiri anakufa watu wanazozana kuhusu mali. Huu ni ubinafsi wa aliyekufa kwa watoto wake. Angewapa mapema kila mtu chake na mkewe pia kwa ratio.

Naanza kuwa na mashaka na utajiri wa mizimu🤣🤣🤣
 
Sheria kuhusu mirathi na wosia zipo zaidi ya 5 Tanzania, na sheria hizi zote zinaongelea namna ya kuandika wosia na namna ya kugawa mali.

Inapotokea sheria hizi haijafuatwa na mtu amabaye ndio anaandika wosia huweza kupelekea wosia huo kukataliwa na mahakama,

Baadhi ya sababu hizo ni
- kuto kumtaka msimamizi wa mirathi
-Kutokutaka mali zako zote.
-Kutokutaja Watoto/ Mama kama warithi
-Kutokuwa na umri unaoruhusiwa 18+
-Kutokuwa katika hali ya utimamu wa akili wakati ukiandika Wosia (Example mengi case)
- kutokufuata utaratibu wa uandishia wa wosia (example Muslim hutakiwi kuweka mali zako zote Wakfi lazima kiasi cha mali kibaki kwa ajili ya familia.

#CJ
 
Lakini nadhani kuna kipengele kinasema lazima muandika wosia awe na akili timamu ya kujitambua na bila shuruti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…