Hakuna haja ya kuandika Wosia kama Mahakama inaubatilisha

Kweli kabisa
 
Kwa Nchi zetu hizi za kimasikini unakuta kila mtu alipewa na kachezea Mzee akivyokua hai ni ngumu kuomba tena wahuni wanabaki kutamani Mali zilizobaki ukiona wanagombana kama kwa Mzee Mrema mara nyingi wengine hata na Marehemu walikua hawaendi sawa ila wanataka mali zake..wahuni hawafanyi kazi wanasubiri kurithi tuu ukiuliza eti mimi mtoto wake..
 
Nikushukuru kwa ufafanuzi mzuri. Kupitia ufafanuzi huu bado ninayaona mapungufu ktk sheria ya mirathi na wosia.

1. Sheria iko juu ya matakwa ya marehemu. Nimeliona hilo hapa
"Inapotokea sheria hizi haijafuatwa na mtu amabaye ndio anaandika wosia huweza kupelekea wosia huo kukataliwa na mahakama",

Binafsi
ningelipenda kuona sheria inalinda zaidi na kufuata matakwa ya marehemu badala ya kutaka yenyewe ndiyo ifuatwe.
2. Kutokumtaja msimamizi wa mirathi kusibatilishe wosia bali mahakama ichukue nafasi ya usimamizi ama kusaidia kupatikana kwa msimamizi.
3. Kutokutaja mali zote kusibatilishe wosia. Utaratibu ufanyike wa kuzibaini na mahakama ishughulike tu na mgawo wa mali ambazo hazikutajwa na marehemu.

4. Umri (sawa)
5. Utimamu wa akili. Hiki ndiyo kichaka wengi hukitumia kubstilisha wosia. Sheria ishughulike na vipengele vile tu ambavyo vimeongezwa wakati marehemu akiwa kwenye vegetative state. Tunafahamu kuwa wosia hauandikwi mara moja kwa watu wenye mali nyingi na za muda mrefu kama akina Mengi. Huwa wana "update" kwa kuongeza zinazoongezeka.
6. Wosia usibatilishwe kwa kutokufuata utaratibu wa uandishi. Utaratibu wa uandishi ni kama vile upo juu ya matakwa ya marehemu.

Naomba kuwasilisha.
 
Na wewe tafuta zako why utake za marehemu? Maana kama ni kuchangia utajiri wa marehemu ndugu pia wanachangia sana
 
Kama unaamini kuna kitu unaweza fanya kwa kushurutishwa!, Basi hata wosia unaweza kuandika kwa kushurutishwa! Ndipo tafsiri ya kisheria inahusika kumediate pande zote in a win win situation.
 
Mkuu inategemeana inawezekana muhusika aliandika wosia akiwa juu ya kifua Sasa unakuta sio akili yake ya maamuz yake
 
Naye tajiri akawajibu wale watumishi akisema, 'je, si haki yangu kutumia mali yangu kama nipendavyo'?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…