Hakuna jamii iliyolala Tanzania kama watu wa kusini

Labda nikueleze kwa kutumia lugha ya kiuchumi kueleza faida ya serokali ya majimbo ktk zama hizi na kwa jamii ya watu waliolala.
Mkuu mimi nakubali kabisa kwamba serikali ya majimbo ina faida tele sana,sijakataa hilo sehemu yoyote ile naomba unifahamu tena mkui,sijakataa kwamba serikali ya majimbo ina faida sana tu.
kwa Mikoa unayoona imepiga hatua ya maendeleo ni ile ambayo INA vijana waliojiriwa na seikali na sekta binafsi.
Hapa unakubali kwamba kuna mikoa imeendelea kupita kusini,lakini unasahau kuwa mikoa hiyo imeendelea bila hata ya hiyo serikali ya majimbo.

Kwa maana kama mikoa mingine imeweza kupiga hatua bila serikali ya majimbo basi na kusini pia tunaweza kuendelea bila kutegemea mfumo huo wa majimbo ambao mpaka serikali itake au ije swrikali mpya.


Nafasi za kazi serikali 90% zikachukuliwa na wageni. Sio kwa sababu vijana hawana weledi laa, kwasababu ajira wanapeana kwa kujuana na Sera ya nchi ya ajira inaruhusu kufanywa wanayofanya.
Sio kweli kaka.

Angalia takwimu vijana waliokuwa na elimu kusini ni wachache sana ukilinganisha na vijana wasiokuwa na elimu kusini huko.

Shule ambayo mimi nilisoma waliofanikiwa kwenda A level na kumaliza masomo walikuwa ni watu hawazidi 13 na tulikuwa wanafunzi zaidi ya 100,hiyo ni kusini shule ya mjini sio kijijini,na hiyo shule ilijitahidi kufanya vizuri

Shule hiyo hiyo form four wa mwanzo kuhitimu hakwenda hata mmoja form five na kupata elimu ya juu.

Wakati huo huo mpaka hivi leo hakuna utofauti mkubwa wa vijana kwenda A level ukilinganisha na zamani.

Shule mpaka 2009 shule za sekondari mikoa ya lindi zilikuwa ni chache,hii ina maana ya k2amba vijana wengi walikosa elimu na wakakosa na sifa ya kuajirika.

Hivyo kusema kwamba serikali imewanyjma nafasi huu ni uongo wa wazi na haya ni maneno ambayo utazidi kuwafanya watu wa kusini waone kuwa kumbe tatizo sio wao bali serikali,inaonesha hujayaishi maisha ya kusini,mimi nimelelewa kusini kwa zaidi ya miaka 18 maisha tu ndio yamenifanya niwe mbali ila huwa ni nyumbani naenda sana tu mpaka kesho wazazi wangu wapo huko.




Bado tu huoni faida ya serokali ya majimbo
Mkuu hakuna aliyepinga serikali ya majimbo naomba uelewe tena.

Ninachopinga ni kuona kwamba serikali ya majimbo ndio suluhisho la kwanza kwa maendeleo ya kusini wakati kuna mikoa imeendelea bila hizo serikali za majimbo ?

Badala yake tutafute njia ambazo zitakuwa hazisubiri idhini ya serikali,kwa sababu ishu ya majimbo ikiwa itachukua muda mrefu ina maana wana kusini waendelee kubweteka tu wakisubiri miujiza ya serikali ya majimbo ?

Hapana watafute njia zingine za kusolve hii ishu
 
hilo la hospital ya rufaa mbona ishajengwa tayari mkuu. NEnda pale mikindani utaiona.
 
Ndanda hospital ni referral hospital


That's one,nisihangaike tena maana inaonekana unazungumza usilolijua
Hahaha hospital ya rufaa ndio kwanza inajengwa mtwara baada ya miaka 60.

St Benedict Ndanda Hospital si Serikali
 
hilo la hospital ya rufaa mbona ishajengwa tayari mkuu. NEnda pale mikindani utaiona.
Yes. Ni baada ya miaka 60. Na baada ya kumaliza kanda zote kujemgwa. Fikiria reli itakuja mwaka gn ikiwa sasa serikali INA deni la tri 78. Tusubiri kiama kama kusini hawatofanya maamuzi magumu
 

Nafurahi kuona kuwa tunaanza kukubaliana kuhusu umuhimu was Wana kusini kuwa na jukwaa huru la kujiamulia yale tunayoamini ndio mustakbali wetu badala ya kuridhika na kukisubiri kikundi cha watu wengune watufanyie maamuzi kwa niaba yetu.

Kuna mambo machache hatujaelewana au hujanielewa.


1. ..... kama mikoa mingine imeweza kupiga hatua bila serikali ya majimbo basi na kusini pia tunaweza kuendelea bila kutegemea mfumo huo wa majimbo ambao mpaka serikali itake au ije swrikali mpya.

Maoni mbadala: nimesema mikoa yote unayoona imepiga hatua serikali iliwekeza. Serikali ikiwekeza mzunguko was pesa unaongezeka. Hoja yangu hatuwezi jifananisha na mikoa ambayo serikali iliwekeza dhidi ya mikoa ambayo serikali imeisahau. Haya kwenye boxing mabondia hawawezi kupiganishwa kama wana tofauti ya uzito mkubwa. Huwezi kushindanisha shule ya ilboru na madangwa sekondari. Wakati serikali iliwekeza ilboru. Ili nasi tupige hatua lazima tutafute mbadala kwa kuitafuta serikali ambayo itawekeza. Na mbadala huo ndio serikali ya majimbo ambayo kimsingi unaiamini. Sasa kama serialikali inapatikana kila baada ya miaka mitano. Kuna ubaya gn sisi tukajipanga sasa kuanzalisha jukwaa au chama chenye kutetea maslahi ya wana kusini. Ili chama kilicho madarakani kiamue kuendelea kutoipa kipaumbele kanda yetu na wakose kura zetu kwa kukichagua chama tutachosajili chenye kutaka mfumo wa majimbo.?!?!? Nasisitiza tens mikoa iliyoendelea haikuendelea kwa kuwa wao ni hodari na sisi ni wavivu laa! Imeendelea kwa kuwa serikali iliwekeza kwayo na umasikini was wana kusini ni was kulazimishwa watu wawe masikini kutokana na kusahauliwa na serikali. Na tumesahauliwa na serikali kwa kuwa sisi wenyewe tumelala.


Nafasi za kazi serikali 90% zikachukuliwa na wageni. Sio kwa sababu vijana hawana weledi laa, kwasababu ajira wanapeana kwa kujuana na Sera ya nchi ya ajira inaruhusu kufanywa wanayofanya.

Hili kuna malalamiko juu ya upendeleo. Zikitoka nafasi za polisi au jeshi, wengi wanaochukuliwa ni watoto wa maaskari. Hivyo hata kama mapungufu ni ya watendaji, lawama tutazitupia serikali. Niliwahi kuzungumza na MTU mmoja alinambia zilitokea nafasi za 50. Kati nafasi hizo wenyeji waliobahatika hawakuzidi 5.

Kama utakuwa umenielewa naamini utakubaliana na Mimi kuwa milango ifunguliwe kwa kila wazo litakalopelea kusini kusisahauliwe ikiwemo mchakato was kuanzisha chama chenye kupigamia maslahi ya kusini. Ili kila mpiga kuwa apige kura ya maslahi yake badala ya kung'ang'nia vyama viliopo ambavyo havina au havipiganii maslahi yyt ya wana kusini
 
Mtoa mada anatafuta ugomvi ulipo,serikali ndo imelala lakin sio watu was kusini,labda kama kalaliwa yeye!
 
Umeandika pumba kabisa..kwamba nafasi za ajira za watu wa kusini zinachukuliwa na wageni?kwahiyo kusoma hamtaki..elimu mnakomea la saba mnaolewa na kuja kuwa mamachinga dsm..manataka madaktari..wahasibu watokee wapi..?somesheni watoto acheni kulia lia.

#MaendeleoHayanaChama
 
Acha uong Mbinga imeendelea na inaendeled vizuri katika maeneo mengi kuliko wilaya nyingi, japo haijulikani Sana
 
Huyo babu yako angechagua kuishi SOUTH AFRICA kwanini amekaa hapa BONGO. Wewe na mzee wako wote hamko sawa kichwani.
 
Hahaha hospital ya rufaa ndio kwanza inajengwa mtwara baada ya miaka 60.

St Benedict Ndanda Hospital si Serikali
Hujui wewe, nilikuwa huko siku si nyingi, Wana hospitali kubwa na mpya ya Kanda ipo Mikindani, wana soko kubwa liko sawa na la Ndugai kwa kila kitu, bandari imepanuliwa barabara za uhakika, kwenda wilaya zote kasoro kutoka Nanyamba mpaka Newala kutokea Masasi ambapo tayari wamepelekewa pesa. Uwanja wa ndege wanao ambapo hata uko sawa na tu na ule wa Dom, Umeme uhakika, hakuna mikoa yenye uhakika wa UMEME NCHI HII KUSHINDA LINDI NA MTWARA, MAJI HAKUNA MGAO. SIJUI KUSINI MNAMAANISHA WAPI.
MAANA HATA MANYARA NI KASKAZINI NA KUKO HOVYO MARADUFU.
 
Mkuu nikuulize hivi kipindi wachaga walipojazana TRA inamaana makabila mengine yalikuwa hayajasoma?!?!

Au ktk awamu iliyopita pale Sukuma walipojaa kila idara za serikali na ktk nafasi nyeti za kufanya maamuzi INA maana makabila mengine hayakuwa yamesoma?!?!

Suala LA jamii ya kusini kusoma sasa no historia.

Hakuna nafasi yyt ya ajira ambayo kwasasa 90% imeshikwa na wageni ambayo wana kusini hawana vigezo vya elimu kukamata nafasi hiyo.

Tena sio kusini Bali watu was kata moja tu wanaweza kufit ktk nafasi hata 50 zikitangazwa. Familia yangu tu tuko wenye first degree zaidi ya 10 masters zaidi ya 5. Binafsi niliwahi mfundisha mkurugrnzi was wilaya ambae elimu take ilikiwa ni form iv. Ndugu yangu ambae alikuwa akifanya field sehemu, baadae sehemu hiyo wakatangaza ajira. Lkn awamu ya pili ya kuitwa kwenye interview yeye hakuitwa, hadi bosi was ile taasisi tens ya seriksli akashangaa. Akamshauri aandike barua kwa katibu mkuu kupeleka malalmiko yake. Katibu mkuu akatoa agizo aitwe kwenye awamu ya pili ya interview na matokeo take akapata ajira.

Nachotaka kusema kuna asilimia kubwa ya watumishi so waadilifu. Wanafanya upendeleo na ubaguzi. Wachachr sana in werevu.

Kuwepo kwa zaidi ya 90% ya wafanyazi wageni kanda ya kusini si bahati mbaya. Si kwakuwa hakuna wenye kufit nafasi hizo kwa wenyeji Bali kuna upendeleo, kuna kushikana mikono, Luna ugod father. Hats wakusini wasome VP maadam chumba cha interview wamekaa wageni watupu nafasi hizo zitaendela kutwaliwa na wageni. Na hakuna njia nyingine ya kubadili mfumo huu ila kuwepo na serikali za majimbo.
Ambapo mfumo wa ajira unasimamiwa na madiwani. Unaweza kuuliza madiwani wana nafasi gn kuwaintetview watu wenye taaluma zao. Ni hivi wataalamu was fani wanakuwepo lkn wenye kufanya maamuzi in madiwani.
Na sharti kuu wenyeji lazima wawe zaidi ya 75%. Hili ni sharti.

Else mtaendelea kuwazuga wana kusini wajihisi kweli hawastahili kuajiriwa kwa sababu zile zinazojulikana "zilipendwa"

Yuki ndugu yangu aliyoa takwimu za miaka 7 - 10 iliyopita kuwa eti darasani weneji waliofaulu hawakuzidi 10. Kwa takwimu kama hiyo ukizidisha miaka 10 ambayo serikali haikutangaza ajira manake idadi hiyi sasa imefika watu zaidi ya 100 wana taaluma xao lkn hawana ajira.

Kusini inapaswa kuamka kutoka ktk usingizi mzito na macho yaliyojaa matongotongo.
 
Demu wangu mmakua anaboa Kila kukicha kwenye shughuli..lol
 
๐—ช๐—ฎ๐˜๐—ฎ๐—ป๐—ด๐—ฎ๐—ป๐˜†๐—ถ๐—ธ๐—ฎ ๐˜„๐—ผ๐˜๐—ฒ
 
Sijui kama hii article ina ukweli. Unakaa mikoa ya Lindi na Mtwara? Fikiria upanuzi wa bandari ya Mtwara, kiwanja cha ndege, kiwanda cha cement, uchimbaji wa gesi,wakulima wa korosho kupewa pembejeo bure, daraja la mkapa etc
 
Tanzania ni kubwa aisee
Kama vipi iwepo a na b
Itakuwa rahisi kwa maendeleo kupatikana
 
We jamaa kusini ulienda lini?mana kwa mawazo haya naweza sema ulikaa siku moja ukaondoka ndio umekuja na conclusion hiyo.

Kwa uzoefu wangu wa miaka mi4..maji na umeme ni matatizo common kwa watu wa kusini.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hivi unajua hakuna kipindi watu wakusini walijaa serikalini kama kipindi cha mkapa..hususani idara za ulinzi na usalama.

Tukija hoja ya wasomi bado huwezi linganisha watu wa kusini na watu wa kaskazinj katika wingi wa wasomi wenye elimu za juu..

Hii hupelekea nafasi nyingi lts say 100 ukapata watu wa kaskazini 90 na watu wa kusini 10..hapo wenye chance ni kubwa ya kupata ni watu wa kaskazini..sio upendeleo ingawa waweza kuwepo...kama ulivyokuwepo serikali ya mkapa.

Kingine watu wa kusini hambebeki ndiomana hata marehemu mkapa aliamua kuwaacha tu mana mmejaa majungu na fitina..natakana kubebwa hata pasipobebeka.

Hoja ya majimbo ni nzuri sana wala siipingi..tambua serikali ili weka mfumo huu uliopo ili kuunganisha taifa na kuondoa matabaka ya ukabila..udini na ukanda..ambapo leo hii kijana wa newala anaenda kufanya kazi sengerema..

Sasa ukisema tuweke mfumo wa majimbo na kuajairi watu wa eneo husika tu huoni tunataka kurudi kule kule tulipotoka mana hakuta kua nakuchangamana tena...hivyo kutengeneza ubaguzi..hoja ya majimbo naweza iuinga mkono kwenye masuala ya kiuchumi na wala sio ajira..watu waajiriwe popote ndani ya nchi yao.

Wito: watu wa kusini hasa Mtwara na Lindi ondoeni ujinga na wivu kwa wasomi..pelekeni watoto shule wapate elimu waondoe ujinga.

#MaendeleoHayanaChama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ