safuher
JF-Expert Member
- Feb 11, 2019
- 11,837
- 17,412
Mkuu mimi nakubali kabisa kwamba serikali ya majimbo ina faida tele sana,sijakataa hilo sehemu yoyote ile naomba unifahamu tena mkui,sijakataa kwamba serikali ya majimbo ina faida sana tu.Labda nikueleze kwa kutumia lugha ya kiuchumi kueleza faida ya serokali ya majimbo ktk zama hizi na kwa jamii ya watu waliolala.
Hapa unakubali kwamba kuna mikoa imeendelea kupita kusini,lakini unasahau kuwa mikoa hiyo imeendelea bila hata ya hiyo serikali ya majimbo.kwa Mikoa unayoona imepiga hatua ya maendeleo ni ile ambayo INA vijana waliojiriwa na seikali na sekta binafsi.
Kwa maana kama mikoa mingine imeweza kupiga hatua bila serikali ya majimbo basi na kusini pia tunaweza kuendelea bila kutegemea mfumo huo wa majimbo ambao mpaka serikali itake au ije swrikali mpya.
Sio kweli kaka.Nafasi za kazi serikali 90% zikachukuliwa na wageni. Sio kwa sababu vijana hawana weledi laa, kwasababu ajira wanapeana kwa kujuana na Sera ya nchi ya ajira inaruhusu kufanywa wanayofanya.
Angalia takwimu vijana waliokuwa na elimu kusini ni wachache sana ukilinganisha na vijana wasiokuwa na elimu kusini huko.
Shule ambayo mimi nilisoma waliofanikiwa kwenda A level na kumaliza masomo walikuwa ni watu hawazidi 13 na tulikuwa wanafunzi zaidi ya 100,hiyo ni kusini shule ya mjini sio kijijini,na hiyo shule ilijitahidi kufanya vizuri
Shule hiyo hiyo form four wa mwanzo kuhitimu hakwenda hata mmoja form five na kupata elimu ya juu.
Wakati huo huo mpaka hivi leo hakuna utofauti mkubwa wa vijana kwenda A level ukilinganisha na zamani.
Shule mpaka 2009 shule za sekondari mikoa ya lindi zilikuwa ni chache,hii ina maana ya k2amba vijana wengi walikosa elimu na wakakosa na sifa ya kuajirika.
Hivyo kusema kwamba serikali imewanyjma nafasi huu ni uongo wa wazi na haya ni maneno ambayo utazidi kuwafanya watu wa kusini waone kuwa kumbe tatizo sio wao bali serikali,inaonesha hujayaishi maisha ya kusini,mimi nimelelewa kusini kwa zaidi ya miaka 18 maisha tu ndio yamenifanya niwe mbali ila huwa ni nyumbani naenda sana tu mpaka kesho wazazi wangu wapo huko.
Mkuu hakuna aliyepinga serikali ya majimbo naomba uelewe tena.Bado tu huoni faida ya serokali ya majimbo
Ninachopinga ni kuona kwamba serikali ya majimbo ndio suluhisho la kwanza kwa maendeleo ya kusini wakati kuna mikoa imeendelea bila hizo serikali za majimbo ?
Badala yake tutafute njia ambazo zitakuwa hazisubiri idhini ya serikali,kwa sababu ishu ya majimbo ikiwa itachukua muda mrefu ina maana wana kusini waendelee kubweteka tu wakisubiri miujiza ya serikali ya majimbo ?
Hapana watafute njia zingine za kusolve hii ishu